Kigezo cha mtu kuitwa machinga siyo namna ya ufanyaji wa biashara bali ni kiwango cha mtaji alichokiwekeza kwenye mtaji wake. Justifiably machinga anapaswa kuwa mtu yeyote mwenye mtaji ambao uko chini ya milioni 5 bila kujalisha namna na mahali anapofanyia biashara.
Ila kwakuwa serikali yetu inanjaa kielelezo cha machinga na biashara zake ni namna anavyoteseka katika utafutaji wake. Hata kama ana mtaji wa milioni 6 lakini akawa anauza karanga, mkaa, kuni kavu, mbolea za mafungu, majani ya nguruwe na ng'ombe, dagaa na samaki chanjani kwa kutumia wauzaji tofauti huyo watamuona mchovu na kumuweka nje ya mfumo wa kodi. Lakini kwa mtaji huohuo wa milioni 6 mtu akianzisha duka la vinywaji, TRA na halmashauri lazima watashughulika naye kulipa kodi.
Kiufupi, ukiichanganya serikali umetoboa.