Tangu awamu ya 4, 5 na sasa awamu ya 6 hali imekuwa kutoa mifano ya Biblia na Koran, Bungeni na majukwaani. Wanasiasa wanaotoa hotuba zinazostahili kuwa msikitini na kanisani.
Leo hii mkuu wa mkoa wa Mwanza anamwita rais Samia ni mtumishi aliyeletwa na Mungu. Sijui anatutisha au anajisemea kumfurahisha rais. Awamu ya 4 Kikwete tuliambiwa ni mteule wa Mungu na akapewa support hata na viongozi wa dini. Ni kweli aliyotenda alitumwa na Mungu? Awamu ya 5 uzi ule ule! Leo hii maumivi hadi kooni.
Huku ni kufilisika kisiasa. Hatukuwachagua wala hamkuteuliwa ili kutufundisha misahafu. Wanasiasa ni wasimamizi wa vyombo vya utawala. Tunahitaji uelewa wenu wa katiba ya nchi, sera pamoja na sheria zake. Hatuhitaji busara za kujua misahafu ambayo usimamizi wake uko chini ya watu wengine.