Wanasiasa Wanatudanganya kuhusu Katiba

Wanasiasa Wanatudanganya kuhusu Katiba

Kifaurongo

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2010
Posts
4,221
Reaction score
2,359
Hatua iliyofikia ya mchakato wa kipata Katiba mpya si hatua ya wananchi kushirikishwa tena bali ni hatua ya kuwakilishwa.

Wanasiasa ili kuungwa mkono wanatudangaya tuingie ktk migongano ya kudai serikali kutushirikisha hali kuwa wakijua nafasi hiyo imeshapita ktk mchakato wa awali wa Tume ya Katiba kupokea maoni ya Wananchi.

Kwa bahati mbaya hao wanaotuwakilisha sasa (Wanasiasa, viongozi wa dini na NGOs) wakati wa mchakato wa awali wako waliojaribu kuwalisha wananchi nini cha kuongea, wako waliowatisha wananchi wasijitokeze mbele ya tume kwamba haiaminiki. Leo wanajaribu kututumia kuwa tunaougomea mchakato ni wananchi ati hatujashirikishwa!!

Huu ni uhuni Tulishatoa maoni na rasimu ya kwanza ya maoni yetu imesha toka nasasa rasimu ya marekebisho yatokanayo na mabaraza ya katiba inaandaliwa wananchi hatuna nafasi tena. Tunasubiri bunge la Katiba (Watuwakiliahw) watumalizie kazi
 
Ukikubali kudanganywa na mwanasiasa, basi ujijue kuwa ni janga!
 
Wanasiana waone kama walivyo wewe nenda zako wengine pasua kichwa ,
wengi wao wanafiki na wambea lazima wapuuzwe.
 
Hatua iliyofikia ya mchakato wa kipata Katiba mpya si hatua ya wananchi kushirikishwa tena bali ni hatua ya kuwakilishwa.

Wanasiasa ili kuungwa mkono wanatudangaya tuingie ktk migongano ya kudai serikali kutushirikisha hali kuwa wakijua nafasi hiyo imeshapita ktk mchakato wa awali wa Tume ya Katiba kupokea maoni ya Wananchi.

Kwa bahati mbaya hao wanaotuwakilisha sasa (Wanasiasa, viongozi wa dini na NGOs) wakati wa mchakato wa awali wako waliojaribu kuwalisha wananchi nini cha kuongea, wako waliowatisha wananchi wasijitokeze mbele ya tume kwamba haiaminiki. Leo wanajaribu kututumia kuwa tunaougomea mchakato ni wananchi ati hatujashirikishwa!!

Huu ni uhuni Tulishatoa maoni na rasimu ya kwanza ya maoni yetu imesha toka nasasa rasimu ya marekebisho yatokanayo na mabaraza ya katiba inaandaliwa wananchi hatuna nafasi tena. Tunasubiri bunge la Katiba (Watuwakiliahw) watumalizie kazi

Umeshavurugwa ? Maana hizi si akili za kawaida .
 
Mtafaruku wa sasa hauhusu Mchakato bali mswada wa marekebisho ya sheria! Tofautisha!!!
 
Mtafaruku wa sasa hauhusu Mchakato bali mswada wa marekebisho ya sheria! Tofautisha!!!

Wanaojua kuwa mtafaruku wa sasa ni wa mswaada ni wachache wenye uelewa kama wewe, lakini yanayohubiriwa na wanasiasa nikuwa 'wananchi tusikubali tuandamane sababu katiba lazima itokane na mawazo yetu' kana kwamba bado kuna nafasi ya wananchi kufanya hiyo, lengo likiwa moja tu kupata kuungwa mkono ili kutimiza malengo yao.
 
Katiba iseme ni lazima kwa viongozi wote kulipa kodi, rais aondolewe/kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye kwa wananchi zaidi ya million moja kuweka saini, kasha kupigiwa kura hiyo na wananchi wote over 18years
 
Ili kupunguza msongamano dar, wizara zigawanywe kwenye kila kanda, na rais ahamie Dodoma, yaani ikulu kuu iwe dodoma
 
majimbo ya uchaguzi yapunguzwe kuwa sawa na mikoa, kila mkoamajimbo mawili tu.
 
ni kweli wanasiasa wameharibu mchakato mzima wa katiba badala ya watu kujadili mambo ya maana wamejikta kwenye muundo wa muungano pia wakati bunge la katiba likitakiwa kubeba wawakilishi wa makundi mbali mbali wao ndio wamechukua sehemu kubwa hii sijui ni uroho wa posho hii katiba itakuwa bomu zaidi
 
WaTz wajanja kweli kweli! Wanadhani kujulishwa hatua kwa hatua kuhusu mchakato wa Katiba Mpya ndiyo kushiriki kutoa maoni. Niambie hili kama jibu unalo: Kifungu cha kwanza tu kinabainisha hivi: "Tanzania ni Jamhuri. Ni Shirikisho la Tanganyika na Zanzibar". Ujinga wangu mimi unanijulisha kuwa Jamhuri ni nchi yenye utawala usiokuwa na majimbo yanayojitemea. Ukimwuliza Mwingereza atakwambia nchi yeyote inayojitenga na Ufalme wake huanza kujiita Jamhuri, ili itoke katika utawala wake---kama Nchi. Shirikisho ni muungano wa nchi au majimbo huru yanayojiendeshea serikali za ndani bila kuulizwa na Serikali Kuu. Uthabiti wa Marekani unatokana na kuwa shirikisho, uthabiti wa Waingereza ni kutokana na kuwa Jamhuri. Mbona Tanzania tunaendesha usanii wa kutaka kuichanganya mifumo hii miwili kwa lugha ya ubabaishaji na kuvumiliana wakati migogoro haina mwenye. Hili mnalitaka liendelezwe na Katiba Mpya?

Hongereni nyie ni Watanzania bara bara, mnao uwezo wa kupanga migogoro na kuamua miafaka.
 
Back
Top Bottom