Maoni ya wengi, yanashangaza. Hata, baadhi ya wachambuzi Redioni, mfano RFA, nao wameniacha hoi. Wametusikilizisha sauti ya msoma hukumu, inaonyesha kosa la wazi la Manara. Yaani, kile kitendo cha kutoka alikokaa, na kwenda kupiga kelele mbele ya VIP, walikokaa wenye hadhi hiyo. Tunaambiwa, aliambiwa aondoke hapo mbele. Aliondoka, na kurudi tena. Pia akambiwa aondoke, mpaka Karia naye akaingilia kati, kumtaka aondoke hapo mbele.
Sasa, wao wameng'ang'ania kuwa, Karia naye alistahili adhabu! Sijui kwa kosa gani?