Wanasiasa (Zitto na Kitila) acheni kuingilia mambo ya mipira, Mnategemewa kuwa mfano katika kuheshimu mamlaka

Kabisa
 
Kanuni ziko wazi
 
Manara aliwahi kufungia mpira miaka 7, uongozi wa KARIA ndiyo uliukuja kumtoa kwa kusikiliza rufaa!
Hivyo manara ni sikio la kufa
 
MJINGA ni yule anayetoa maoni yake lakini anakashifu maoni ya wengine kwa vile tu yanakinzana na utashi na matamanio yake!

Katika hilo hata ngumbaro anadiriki kumkebehi mtu kama Prof Mkumbo na Msomi Zitto kabwe kuwa ni wajinga! huku akishindwa kukosoa ama kujadili haja walizotoa kimantiki!

Katika misingi ya asili ya haki mlalamikiwa na mlalamikaji wote huitwa na kutoa maelezo yao mbele ya kamati au mamlaka ya kutoa haki, kabla ya kuchambua maelezo ya pande zote mbili pamoja na ushahidi wao, hatua ambayo itaiwezesha kamati kutoa uamuzi wa haki kutokana na nguvu za hoja!
Huo utaratibu wa mshitaki kuwa ni huyo huyo, muendesha mashtaka awe ni yuleyule na mtoa hukumu ni yuleyule tunabananga natural justice!

Ni mwelekeo tenge na usio na afya, unaopaswa kusitishwa kwa kwa nguvu zote.
JADILI!
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…