Wanasimba hii chungu kumeza, ila hasira zenu msizimalizie kwa Mohamed Dewji!

Wanasimba hii chungu kumeza, ila hasira zenu msizimalizie kwa Mohamed Dewji!

Librarian 105

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
261
Reaction score
356
Yanga ndio huyo Fainali ya Shirikisho. Tambueni tu mtani anachuma alichopanda baada ya msoto mkali.

Uwekezaji, mipango-mkakati na utawala bora, maandalizi mazuri ya msimu, kiu ya mafanikio n.k, vimewafanya jamaa kuandika historia.

Mafanikio hayana uchawi zaidi ya kujipanga. Mtaani apewe kongole zake.

images(11).jpeg

Mwenye kutaka kutema nyongo ateme tu.

images(10).jpeg
 
Sisi Yanga hatu comment post za watu ambao timu zao hazijafika final
 
Mkuu uko sahihi kabisa. Mimi ni Simba damu ila ukweli lazima usemwe, kwamba:

1.Yanga imeonyesha ina viongozi walio serious sana na mafanikio.Wamedhihirisha kwamba hawana 'uswahili swahili' kama wa akina Sultani Mangungo wa Msovero kutuletea Caesar Manzoki kwenye Uchaguzi.

2.Simba ina viongozi wa hovyo sana. Simba ilifanikiwa kuingia robo fainali ya CL mara 2, kwanini mafanikio hayo yasingewahamasisha kufanya "usajiri wa nguvu" ili waweze kuvuka hatua za robo fainali na hatimaye fainali kwa misimu iliyofuatia? Kama haukuwa ujinga ni nini? Mimi nilipoona Simba inaendelea kuwabakiza wachezaji ambao walishaanza kuflop nikajua Simba kwishney (Maana mchezaji kama John Bocco anahitaji apoteze nafasi 6 za wazi za kufunga, kisha ya 7 ndo afunge. Champions League haihitaji wachezaji wa namna hii).
 
Yaan timu iliyoweka Kambi hapo Kigamboni pre season inakusanya makombe yote? Sasa Simba tuache mbwembwe zisizo na msingi.
 
Walichofeli Simba ni kuwapa timu watu ambao ni wanasiasa mtu amekuwa mbunge miaka kibao lakini hakuendeleza Jimbo ndio aje kuendeleza timu
 
Walichofeli Simba ni kuwapa timu watu ambao ni wanasiasa mtu amekuwa mbunge miaka kibao lakini hakuendeleza Jimbo ndio aje kuendeleza timu
Na ukijaribu kuulizia ziko wapi billion 20 unaitwa Utopolo. Kungekuwa na Billion 20 wasingenunuliwa akina Kyombo, Manula, Kanoute, Sakho, Banda, Onyango, Gadiel, Chama, Inonga, Kapombe, Tshabalala, Ntibanzonkiza, Baleke(tena kwa mkopo).
Wangetafutwa wachezaji wenye hadhi ya Simba siyo haya magarasa yanatoka kapa kila mwaka bila hata kikombe.
 
Yaan timu iliyoweka Kambi hapo Kigamboni pre season inakusanya makombe yote? Sasa Simba tuache mbwembwe zisizo na msingi.
Naikumbuka siku ile simba wanaenda Cairo hata gari halijqpakwa rangi za mdhamini kama wanakimbizwa vile.
Utasikia simba ni timu kubwa . Kubwa ya nn sasa?
 
Back
Top Bottom