Mkuu uko sahihi kabisa. Mimi ni Simba damu ila ukweli lazima usemwe, kwamba:
1.Yanga imeonyesha ina viongozi walio serious sana na mafanikio.Wamedhihirisha kwamba hawana 'uswahili swahili' kama wa akina Sultani Mangungo wa Msovero kutuletea Caesar Manzoki kwenye Uchaguzi.
2.Simba ina viongozi wa hovyo sana. Simba ilifanikiwa kuingia robo fainali ya CL mara 2, kwanini mafanikio hayo yasingewahamasisha kufanya "usajiri wa nguvu" ili waweze kuvuka hatua za robo fainali na hatimaye fainali kwa misimu iliyofuatia? Kama haukuwa ujinga ni nini? Mimi nilipoona Simba inaendelea kuwabakiza wachezaji ambao walishaanza kuflop nikajua Simba kwishney (Maana mchezaji kama John Bocco anahitaji apoteze nafasi 6 za wazi za kufunga, kisha ya 7 ndo afunge. Champions League haihitaji wachezaji wa namna hii).