Wanasimba tuungane kumuokoa Zamoyoni Mogella

Huyu alikuwa na ghorofa moja kinondoni karibu na shule ya msingi muongo,pia alikua na nyumba pale mkwajuni karibu na baa ya katumba
Sasa zimeenda wapi mpk anadaiwa?
Alifilisiwa na mke wake baada ya kudai wagawane mali
 
Cha kushangaza tulisikia na kuambiwa Mogella yupo fit sana, ana nyumba kadhaa na daladala na nini?!
Hawa Ma Celeb sio wa kuwaamini kabisa, kwamba ana mijumba kumbe kapanga, kwamba ana magari kumbe ya kuazima au ya maneja!
Bure kabisa...
Mke alimfilisi
 
Huyu super star wetu wa zamani si ana mjengo wake pale kinondoni huyu? Halafu huyu jamaa dakika za mwisho alituletea uyanga yanga !!
Utakuta, jengo lake kapangisha kwa bei kufuru,lakini yeye anaenda kupanga kwenye bei nafuu!
 
kweli pesa malala nje! haina uhusiano wa kudumu na mtu! huyu hakuwa tajiri sana lakini hakutegemewa kufikia hapa! pole sana Zamoyoni
 
Afande sele alituambia Jamaa yupo vizuri sana kifedha anamiliki hadi Yard ya kuuza magari.
 
Mchezaji wa zamani wa Simba na Taifa Stars Zamoyoni Mogella yuko mbioni kutimuliwa kwenye kota za Urafiki baada ya kulimbikiza kodi mpaka kufikia deni la Tsh mil 5.

Chanzo - Mwananchi .

Ombi - kutoa ni moyo .
Endeleeni kujipendekeza kwa watu na kuwasahau ndugu zenu wenye matatatizo zaidi ya hiyo kodi.
 
Mogela is gentleman yawezekana alipangisha makazi yake ,naye akapanga urafiki kimkakati zaidi, hawezi anguka vile wengine wanatamani iwe, ikiwa ni anguko true friends watainuka inshalah
 
Huyu si alikuwa na pesa huyu baba yake Mariam Mogella aka get buzy?;Au mke ndo alimfilisi jumla.
[emoji1] [emoji2] nahisi nakujua maana ilo aka la get busy mkuu umenikumbusha A level pale green acres.
 
Zamoyoni Mogella amepanga ofisi ya biashara hapa urafiki ni jirani yangu kiofisi sio makazi na alijihusiha na ujenzi na supplying. Anachodaiwa ni kodi za ofisi zake mbili za biashara sio makazi. Yupo vizuri kuliko wengi wetu humu. Mod fanyeni update sio watu wanachangia tu bila uelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…