WanaSimba wenzangu kuringia sana kiwango cha Jean Baleke, ni kama mtu kuringia gari la mkopo

WanaSimba wenzangu kuringia sana kiwango cha Jean Baleke, ni kama mtu kuringia gari la mkopo

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Ni kweli isiyokuwa na shaka Jean Baleke ni moto wa kutisha, wanaobisha ni wivu tu

Lakini pia tusisahau Jean Baleke sio mchezaji wetu, ni mchezaji wa TP Mazembe na yupo Simba kwa mkopo

Kuringa sana ni kama mtu anateringia gari la mkopo kama vile ni lake

Huku tukijisahaulisha ukweli mchungu kuwa tumesajili magarasa ya kudumu kama Sawadogo, Okwa, Okrah na Akpan ndio wachezaji wetu ambao watatugharimu mamilioni ya hela kwenye mikataba yao.
 
Kwani magoli anafunga ni ya mkopo? we are living today ya mbele yatajulikna huko
Too late kwa sasa mkuu, hayawezi kutupa ubingwa wa ligi.

Labda Kombe la Shirikisho

Ila pointi ni kuwa wachezaji ambao tulitakiwa kusajili kwa mkataba wa kudumu tumechukua kwa mkopo na ambao tulitakiwa kuchukua kwa mkopo tumewapa mikataba ya kudumu
 
Too late kwa sasa mkuu, hayawezi kutupa ubingwa wa ligi
Labda Kombe la Shirikisho

Ila pointi ni kuwa wachezaji ambao tulitakiwa kusajili kwa mkataba wa kudumu tumechukua kwa mkopo na ambao tulitakiwa kuchukua kwa mkopo tumewapa mikataba ya kudumu
Tuambiane ukweli tu, Simba ya Sasa ni mbovu' na inahitaji 'overhaul', ama sivyo itabidi ikae miaka kurudi kwenye viwango!
 
Ni kweli isiyokuwa na shaka Jean Baleke ni moto wa kutisha, wanaobisha ni wivu tu...
Sijawahi kuona mchezaji wa kudumu toka nazaliwa, labda utoe mfano. Gigs mwenyewe ilifika hatua muda ukamuacha man u. Au fei toto?
 
Mkuu kwani tunaringia mkataba au matokeo? Kama soka ni mchezo wa furaha unataka watu wakifurahishwa wafanyaje?
Kwa lugha nyingine unawaambia fans kwamba Jean akipiga goli pale jukwaani watulie kwa sababu ni wa mkopo?! Imewahi kutokea wapi hiyo hapa duniani
 
Back
Top Bottom