Wanataaluma Wakristo watoa waraka wa 'Tafakari' kabla ya kuichagua CCM

Wanataaluma Wakristo watoa waraka wa 'Tafakari' kabla ya kuichagua CCM

Kila mtu anayo haki ya kusema na kutoa maoni yake mwenyewe maana kila mtanzania ni haki yake ya msingi
HESHIMA KWAKO, na huo ndo msingi wa haki zooote duniani, hakuna mwenye haki yakuhodhi uhuru wa wengine kufikiri,kutoa mawazo yao, hakuna mwenye haki zaidi ya kujadili mustakabali wa taifa hili......na hayo ndo maisha lazima watu wajifunze kuvumilia mawazo yawengine.
 
Ben, swala moja ni kuwa sio lazima Waislamu waige kila Wakristo wanachofanya, maaana waswahili walisema kumuiga tembo huishia kuchanika msamba !
kwani wao waislamu wanawasiliana vipi na waumini wao ? wao waendelee na taratibu zao katika kujadili ujenzi maridhawa wa taifa hili.
kwa mfano Wakatoliki wamekua na taratibu zao za kupeana nyaraka zao kila baada ya muda fulani, wao wanamambo wanayoamini kuwa ili mtu aweze kuabudu vyema ni lazima mazingira yaletwayo na hali ya kisiasa yawe tulivu, uchumi uwe mzuri na mambo kama hayo.
sasa kukaa nakujadiliana eti na watu wadini nyingine namna yakuendesha kanisa huo ni ujinga, na haukubaliki.
kuna makundi ya watu yanadeka sana nnchi hii, wanapenda kulialia, wanahamishia matatizo yao yakihistoria kwa wengine. kifupi adui yao namba moja ni wao wenyewe.

Ndiyo maana mkuu ni kasema ili kuwa rational ktk matendo na maneno ya taasisi zetu tuepuke kuingia deep ktk siasa hadi kufikia katika uwezekano wa kuleta mtazamo hatarishi

Pia,hebu chukulia katika mazingira hayo hayo ikatokea taasisi pia ya kichaga ikaja na waraka,wahaya na wa kwao,wa kisukuma hivyo hivyo maaanke tumeruhusu hii hali katika itikadi za kidini ,na pia ikitokea katika itikadi za kikabila tutaweza kuyazima haya?

Si lazima waislam waige wakristo lakini kuna uwezekana wa mabo kama hayo kutokea.

Sasa Kwenye Hoja:

Ni kwa nini hawa wakuu walichelewa kutoa huo waraka kabla ya ile bill ya gharama za uchaguzi?
 
Pale ulikomwambia Tumain ,wao waanzishe waraka wao.Yote haya yanachochea udini kama tukiyapeleka ktk siasa ndugu yangu.It's risky!

Hapo nimekupata Mkuu.Kweli nilikosea.Tumain huwa ananiudhi sana,yeye kila siku ni negative tu..Yaani asisikie mambo yanayohusu Ukristo au mambo yanayohusu CHADEMA atatoka huko alikokuwa hata kama ni uvunguni,aje achafue hali ya hewa.
 
Wamependelewa vipi wakati 75% ya viongozi wetu ni waislam

G.T. umeona jinsi mnavyotawala nchi na bado mnalalamika kuwa nyie sio watawala; bado mnataka na NHC, TPA, TRA na BOT!! Haya sisi ni washangiliaji mpaka hapo parapanda itakapolia ndio mtajiju.
 
Sasa Kwenye Hoja:

Ni kwa nini hawa wakuu walichelewa kutoa huo waraka kabla ya ile bill ya gharama za uchaguzi?
unajua kuna mambo ya kisanii ambayo JK na makundi ya watu wake wa CCM wanayafanya, ikiwemo kuutumia mwanya wa Watanzania wengi kutokujua hakizao na uvivu wa Watz wengi kufuatilia mambo.
Yeye anapaswa kutuomba radhi kwakuruhusu kampeni zake kutumia pesa chafu tena chafu sana , kabla yakuibuka na porojo za sheria ya kuzuia fedha chafu.
nakwambia hawana nia , uwezo wala moyo wakuisimamia sheria hiyo.
kama sheria yakuanzishwa takukuru ingeweza kusimamiwa vyema hakuna ambae angeweza kutumia rushwa kwenye chaguzi.
sasa wanataaluma hao, wanaposema kuwa JK na WanaCCM wenzake waje wasimame watueleze 2005 walitumia mamilioni mangapi kununua kura, hakuna kosa, wala haichochei udini, wala waislamu wakisema hawatakua wanachochea udini.
Ben, tusihodhi haki yakujadili mustakabali wa taifa letu, waacha watu waseme, ili mradi hawavunji sheria.
 
HESHIMA KWAKO, na huo ndo msingi wa haki zooote duniani, hakuna mwenye haki yakuhodhi uhuru wa wengine kufikiri,kutoa mawazo yao, hakuna mwenye haki zaidi ya kujadili mustakabali wa taifa hili......na hayo ndo maisha lazima watu wajifunze kuvumilia mawazo yawengine.

Mkuu,

Ishu ya Msingi ni kuepuka hoja za kuonyesha kuunga mkono au kupinga chama fulani kwa taasisi za dini au taasisi zilizojifunga katika dini fulani.Hapo ndipo kwenye hoja ya msingi

Hebu angalia hii katiba yetu inasema nini

20(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) haitakuwa
halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho
kutokana na Katiba au sera yake-
(a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya-
(i) imani au kundi lolote la dini;
(ii) kundi lolote la kikabila pahala watu​
watokeapo, rangi au jinsia

Sasa swali linaweza jitokeza hapa,je kundi fulani likiamua kuunga mkono au kuhamasisha wanachama wake wapigie kura kundi fulani ni kosa?Kama si kosa ina maana hapa katiba haikuona athari zozote?

So far katiba inatamka vipi kuhusu haki za chama ktk kuungwa mkono?
 
Hapo nimekupata Mkuu.Kweli nilikosea.Tumain huwa ananiudhi sana,yeye kila siku ni negative tu..Yaani asisikie mambo yanayohusu Ukristo au mambo yanayohusu CHADEMA atatoka huko alikokuwa hata kama ni uvunguni,aje achafue hali ya hewa.

Mkuu,GS tuko pamoja
 
wanataalum au udini mtupu..blah blah ...anzisheni chama cha siasa..au jiungeni na CCJ maana tunafahamu imetokana na waraka wenu ...msisumbue watu ...hakuna jipya kutoka kwa wakatoliki zaidi ya kupenda kupendelewa na kupenda kupita kutawala watu wenginee.. ...tunafahamu mmeshaanza kampeni zenu kanisani lakini.hadangayika mtu..siku hizi..

Tumaini long time! mkuu uko wapi?

Nakubaliana na wewe japo unapata upinzani mkali;

Sijaona sababu, utashi ,wala any reasonable explanation ya mtanzania kujitokeza kutaka haki au kupigania haki ya mtanzania kwa kutumia kimvuli cha kikundi fulani.

Vyama vya siasa, wanaharakati tumewapa hili jukumu. However, I am not saying they should not perticipate or advice anything no! but why are you saying 'mkristo'

Tanzania haina udini kama wengine mnavyotaka ionekane.

Tuma hoja yake ni ya msingi, japokuwa ameenda mbali sana (kwa mfano kusema wakatoliki kupendelewa na wameanza kampeni makanisani -hii kwangu I can testify kuwa si kweli)

Hoja ya msingi ambayo kila mmoja anapaswa kulaani ni kuwa hawakupaswa hawa watu kujitokeza kwa kivuli cha wana taaluma wakristo. Hivi wakristo wanataaluma wana chama? mbona mimi mkristo na niko tayari kumpigia kura mtanzania yeyote ninayeona anafaa! Hivi kwa nchi ya TANZANIA ukishasema mkristo, mwingine akasema mwislamu, then tutaenda mbali tutaanza kubaguana kwa madhehebu ambako kuna mgawanyiko mkubwa.

Fuatilieni na angalieni hao wanataaluma wakristo ni wa madhehebu gani? mimi mwenyewe ni mkristo na nimesoma, ala! mbona sikijuia hicho chama?

je wakiona mambo hayaendi watafanyaje? sio ndio wataona waanzishe chama cha siasa ambacho kita-comprise wakristo?? common tell them they are DEAD WRONG!

-Hebu tuajadili hii hoja bila ushabiki wa kidini.mimi kwa kusema kweli sikupenda hii kitu ambayo watu wamejitangaza wanataaaluma wa kikristu,sasa hapa ndipo udini unapokuja.

Mimi napinga hiyo taasisi kujihusisha na masuala ya kisiasa coz casuality yake ni kubwa kuliko wanavyofikiria.Tuacheni hizi elements za ubaguzi

Kwenye Hoja:

Hawa wanataaluma wangefanya jambo jema sana kama wangewaamsha tu wananchi na kuwapa elimu ya Uraia bila kuishambulia CCM.

Well said Ben, let us discuss facts here, ushabiki wa ukipofu hautalisaidia lolote taifa hili.

Hatuna matabaka ya kidini serikalini wala katika ngazi za uongozi, dini zao waziweke makapuni wao na familia zao. sikatai wana haki ya kusema na kufanya lolote lile kama wananchi, lakini why are you introducing as christian?

wakisema watanzania, haitoshi? what are we up to????
 
unajua kuna mambo ya kisanii ambayo JK na makundi ya watu wake wa CCM wanayafanya, ikiwemo kuutumia mwanya wa Watanzania wengi kutokujua hakizao na uvivu wa Watz wengi kufuatilia mambo.
Yeye anapaswa kutuomba radhi kwakuruhusu kampeni zake kutumia pesa chafu tena chafu sana , kabla yakuibuka na porojo za sheria ya kuzuia fedha chafu.
nakwambia hawana nia , uwezo wala moyo wakuisimamia sheria hiyo.
kama sheria yakuanzishwa takukuru ingeweza kusimamiwa vyema hakuna ambae angeweza kutumia rushwa kwenye chaguzi.
sasa wanataaluma hao, wanaposema kuwa JK na WanaCCM wenzake waje wasimame watueleze 2005 walitumia mamilioni mangapi kununua kura, hakuna kosa, wala haichochei udini, wala waislamu wakisema hawatakua wanachochea udini.
Ben, tusihodhi haki yakujadili mustakabali wa taifa letu, waacha watu waseme, ili mradi hawavunji sheria.

Mkuu

Nakuelewa,ofcourse huo usanii walioingia nao akina JK sikubaliani nao.Kimsingi JK kafanya hivi ili kuzuia watu wengine kuingia kama yeye kwani anaweza pata changamaoto ambayo hajawahi kuifikiria

Pia,Mkuu sijahodhi huu mjadala.hata mimi najadili jambo la muhimu kwa mustakabali wa taifa langu
 
Kila mtu anayo haki ya kusema na kutoa maoni yake mwenyewe maana kila mtanzania ni haki yake ya msingi

Josh hata sisi tumetumia uhuru huo huo katika kumkosoa na kujaribu kumuweka sawa, sasa imagine watu wangeanza kuafata mawazo yake si mantiki ya mada ingepotea kabisa?

Back ktk hoja:

Hawa jamaa mi naona wamechelewa sana kuileta hiyo "tafakari" yao kama wanavyodai hapa kuhusu lengo lao; “Lengo hapa ni kutaka kujua kwa nini sheria hii imekuja sasa, inamlenga nani, madhumuni ya gharama za uchaguzi ni nini na nani atafaidika.”

Na kisha wakakubali kuwa wameshachelewa "Hata hivyo, alisema ‘tafakari’ hiyo ilitoka muda mrefu kabla hata rasimu ya sheria ya uchaguzi haijaenda bungeni, lakini ilichelewa kutolewa na kusambazwa."

Sasa swali hii tafakari inajadili bill u sheria? Manake inaonekana kama wlishaiandaa kabla ya huu muswada kupelekwa BUNGENI. Sasa hawaoni kuwa wanaturudisha nyuma kwa kuchelewa kwao? Nasema kuwa wamechelewa kwa kuwa uchaguzi ni Oct sasa tusitegemee mabadiliko ya sheria hiyo ndani ya wakati na hii ni kusema kuwa hii sheria itatumika katika huo uchaguzi na ndio maana wenzao CCM wakawajibu kuwa hawana muda wa kujadili wa kuwa kama ni mbinu za kushinda kwa kupitia huo mswada basi wamefanikiwa kwani umeshapita. So just to say it s too late for this "tafakari" for the Oct. Labda wajaribu kufikiria uchaguzi mwengine.
 
Tumaini long time! mkuu uko wapi?

Nakubaliana na wewe japo unapata upinzani mkali;

Sijaona sababu, utashi ,wala any reasonable explanation ya mtanzania kujitokeza kutaka haki au kupigania haki ya mtanzania kwa kutumia kimvuli cha kikundi fulani.

Vyama vya siasa, wanaharakati tumewapa hili jukumu. However, I am not saying they should not perticipate or advice anything no! but why are you saying 'mkristo'

Tanzania haina udini kama wengine mnavyotaka ionekane.

Tuma hoja yake ni ya msingi, japokuwa ameenda mbali sana (kwa mfano kusema wakatoliki kupendelewa na wameanza kampeni makanisani -hii kwangu I can testify kuwa si kweli)

Hoja ya msingi ambayo kila mmoja anapaswa kulaani ni kuwa hawakupaswa hawa watu kujitokeza kwa kivuli cha wana taaluma wakristo. Hivi wakristo wanataaluma wana chama? mbona mimi mkristo na niko tayari kumpigia kura mtanzania yeyote ninayeona anafaa! Hivi kwa nchi ya TANZANIA ukishasema mkristo, mwingine akasema mwislamu, then tutaenda mbali tutaanza kubaguana kwa madhehebu ambako kuna mgawanyiko mkubwa.

Fuatilieni na angalieni hao wanataaluma wakristo ni wa madhehebu gani? mimi mwenyewe ni mkristo na nimesoma, ala! mbona sikijuia hicho chama?

je wakiona mambo hayaendi watafanyaje? sio ndio wataona waanzishe chama cha siasa ambacho kita-comprise wakristo?? common tell them they are DEAD WRONG!

Well said Ben, let us discuss facts here, ushabiki wa ukipofu hautalisaidia lolote taifa hili.

Hatuna matabaka ya kidini serikalini wala katika ngazi za uongozi, dini zao waziweke makapuni wao na familia zao. sikatai wana haki ya kusema na kufanya lolote lile kama wananchi, lakini why are you introducing as christian?

wakisema watanzania, haitoshi? what are we up to????

Ohoo Waberoya umeturudisha kule kule tena! sasa kama wenyewe ni CPT na wametaka kutoa mawazo yao wangebadilisha identity yao? Yaani JF kwa kuwa ina mlengo fulani tukitoka kutoa mawazo kwa umma tubadilishe identity yetu eti kisa watu watafikiria kuwa tupo ktk mlengo ule? NO, hiyo ni organization na there is no need for them to hide their identity? Pengo akitaka kuhoji serikali aifche identity yake kama ni Askofu wa RC?

Bolded is the line to take an account of
 
Usitake kubadili mwelekeo kama kawaida yenu...wanataalum wanahangaika kutoka waraka si upuuzi mtupu si wajiunge na vyama vya siasa..blah blah...

Sijaona wakitoka waraka wa kulaini ushoga kanisani ..kama siyo upupu ni nini?

Wewe upeo wako ni mdogo sana na umetawaliwa na fikra za udini. Leta hoja yako kuhusiana na hiyo tafakari (sio waraka). Kwa maoni ya CPT hawa CCM ndio wanaokwamisha demokrasia. Wewe unaonaje? Suala la dini hapa linatoka wapi? Nyie watu mna matatizo sana.
 
Ohoo Waberoya umeturudisha kule kule tena! sasa kama wenyewe ni CPT na wametaka kutoa mawazo yao wangebadilisha identity yao? Yaani JF kwa kuwa ina mlengo fulani tukitoka kutoa mawazo kwa umma tubadilishe identity yetu eti kisa watu watafikiria kuwa tupo ktk mlengo ule? NO, hiyo ni organization na there is no need for them to hide their identity? Pengo akitaka kuhoji serikali aifche identity yake kama ni Askofu wa RC?

Bolded is the line to take an account of

Mkuu unaweza ku-compare waraka wa wakatoliki na ule wa waislamu? upi kwa mawazo yako unafikiri ulikuwa positive kwa jamii ya kitanzania? Pengo akijitokeza kutoa maoni atayatoa kama Pengo, na akisema RC wamemtuma atasema ni RC. huwezi ukaficha identity yako , lakini hiyo identity nani anakupa?
 
SIDHANI KAMA hawa wanataaluma wantumia taaluma yao vema kwani kama wanazuoni watanzania wenye nia njema na nchi hawana sababu ya kutahadhalisha kuichagua CCM kwani CCM ni chama chenye wakristo na wasio wakristo, wenye taaluma na wasio na taaluma sasa iwaje wao waone kama wana haki saaaaaaaaaana ya kuwaambia watanzania nini cha kufanya kama vile wao YESU?
nadhani ni wakati muafaka kuibadilisha CPT kuwa chama cha siasa badala ya kile kinachofanya sasa!
binafsi naweka wazi ni Mkristo na mwana taaluma lakini si member wa hicho chama kwa maana vikundi vingi vya kikristo aibu vinatutia hebu angalia mifano michache
1. ndo walianzisha DECI; ilipofutwa na mwanzilishi kuwekwa luzanga 'no one has a right information 'AIBU'
2. mnakumbuka sakata la SAM NUJOMA ni kivumbi
3. Hivi sabato masalia si ndo kikundi chao kiko professional kwenye injili wataka kwenda ulaya kama hewa Mungu wangu!
4. ubungo pale ndani nenda utakuta kuna bango la tangazo la mwisho wa dunia, ni kikundi cha wakristo wakitaka kuhadaa ulimwengu tumekwisha
na mengine unayoyafahamu; yanatosha kutilia shaka kila mwongozo wa vikundi vya wakristo labda mtu akisimama na kusema mwenyewe kwa nafasi yake nitamwelewa; si mnamwona mrema augustino lyatonga amejitolea mhanga na mahakama ya kadhi na yeye ni mkristo naweza kumsikiliza.
wana jamiiforum amkeni
 
Mkuu unaweza ku-compare waraka wa wakatoliki na ule wa waislamu? upi kwa mawazo yako unafikiri ulikuwa positive kwa jamii ya kitanzania? Pengo akijitokeza kutoa maoni atayatoa kama Pengo, na akisema RC wamemtuma atasema ni RC. huwezi ukaficha identity yako , lakini hiyo identity nani anakupa?

Kuhusu waraka upi ulikuwa positive inategemea mind yako iko free kiasi gani katika kufikiria bila kubase ktk imani yako. Waraka uliofata ulitumia waraka uliopita as background. Point ni kuwa hakuna haja ya kuficha identity kwa watu wenye fikra finyu ndo watahamisha hoja kwasababu wao wakisikia jina la dini nyingine kwa chochote kile tayari kwao ni kama danger alarm
 
Mkuu unaweza ku-compare waraka wa wakatoliki na ule wa waislamu? upi kwa mawazo yako unafikiri ulikuwa positive kwa jamii ya kitanzania? Pengo akijitokeza kutoa maoni atayatoa kama Pengo, na akisema RC wamemtuma atasema ni RC. huwezi ukaficha identity yako , lakini hiyo identity nani anakupa?
briliant nadhani tunaweza kuwa na macho na tukaona lakini tusielewe kuchambua kujua ule ni mkia lile sikio, ile miguu na mengine. nyaraka zije lakini huu sijui kama waweza itwa waraka wa CPT siwezi kukubali. kama CPT wanasema watanzania watafakari kabla ya kuichagua CCM waseme wametumwa na nani. JF haijatumwa na ndiyo maana humu ndani tunafikia kipindi twatoleana hata lugha chafu lakini jahazi laenda, NGOs kama CPT zinapotokea na kudirect watanzania cha kufanya JF haikai kimya na katika huko ndipo tunaibua hoja na kujua ni nani na nani wanasema nini na hata mtazamo wao ukoje;
CPT ni NGO kama NGO zingine unazozifahamu halafu naomba waseme wamesajiliwa na msajili wa vyama vya hiari au wanafanya kama fellowship fulani. kwa masilahi ya TAnzania na watanzania siwezi hata dakika moja kuwaunga mkono CPT na waraka wao hata kama wakisema anayeunga mkono waraka huo anakwenda mbinguni immediately.
Mungu ibariki Tanzania na Mungu wabariki wanaoitaka tanzania moja isiyo na ubaguzi wa aina yoyote. AMEN
 
Wamependelewa vipi wakati 75% ya viongozi wetu ni waislam

..very true

wanataalum au udini mtupu..blah blah ...anzisheni chama cha siasa..au jiungeni na CCJ maana tunafahamu imetokana na waraka wenu ...msisumbue watu ...hakuna jipya kutoka kwa wakatoliki zaidi ya kupenda kupendelewa na kupenda kupita kutawala watu wenginee.. ...tunafahamu mmeshaanza kampeni zenu kanisani lakini.hadangayika mtu..siku hizi..

...vague and narrow minded thinking, if any thinking at all. Need I say, a formulation of an evil eyed, intellectually bankrupt animist. This is the 21st Century and not the dark ages reminiscent of the culture of your own devilsh faith. Eventually, just marginalize yourself whilst, we forge ahead in our diversity!
 
Hapo nimekupata Mkuu.Kweli nilikosea.Tumain huwa ananiudhi sana,yeye kila siku ni negative tu..Yaani asisikie mambo yanayohusu Ukristo au mambo yanayohusu CHADEMA atatoka huko alikokuwa hata kama ni uvunguni,aje achafue hali ya hewa.
hii ya kutafuta asilimia ya viongozi na kuibuka eti ni 75% ni ujenzi wa chuki, hivi kweli unachosema au unachojua kiongozi maana yake ni rais, waziri, mbunge na pengine mkuu wa mkoa. acha unafiki, acha chokochoko, acha uzandiki, acha majungu jenga nchi. sorry
 
Wewe upeo wako ni mdogo sana na umetawaliwa na fikra za udini. Leta hoja yako kuhusiana na hiyo tafakari (sio waraka). Kwa maoni ya CPT hawa CCM ndio wanaokwamisha demokrasia. Wewe unaonaje? Suala la dini hapa linatoka wapi? Nyie watu mna matatizo sana.
mmmh sometime nachoka na hizi hoja sigana
 
Ohoo Waberoya umeturudisha kule kule tena! sasa kama wenyewe ni CPT na wametaka kutoa mawazo yao wangebadilisha identity yao? Yaani JF kwa kuwa ina mlengo fulani tukitoka kutoa mawazo kwa umma tubadilishe identity yetu eti kisa watu watafikiria kuwa tupo ktk mlengo ule? NO, hiyo ni organization na there is no need for them to hide their identity? Pengo akitaka kuhoji serikali aifche identity yake kama ni Askofu wa RC?

Bolded is the line to take an account of
RAY B, sina shaka unajua identity yaweza tumika kuangamiza taifa. hivi kusema wanataaluma wakristo, mbona watu hatuijui. halafu imeibuka tu. ni kikundiambacho kilianzia kati ya makanisani au katika fellowship na kwa vile ni cha wakristo lazima watakuwa wa madhehebu fulani tu; uhakika nilio nao wakatoliki hwamo kama wanabisha waambie CPT waweke humu JF katiba yao na mwongozo, waweke na taarifa zao zote na ni vema wakatuwekea na orodha ya wanachama wao kwa maana wanawafahamu kama JF ilivyo kila mmoja anajifahamu kuwa uanachama wake ni wa rank ipi, mie leo nimepata kuwa senior member. nao watupe orodha, walianzishwa lini na malengo ni yapi. itakuwa njema wakiupload costitution na memoranda of association including certificate of registration isije tukawa wana JF tunajadili mambo kumbe watu wenyewe wako wawili (aliyejitambulisha mwenyekiti na mke wake. hapo wakifanya hayo JF tutakuwa right. si kila kitu cha kutuweka attention wakubwa.
kwa jinsi hii anayesema hapa kuna udini na tutaenda kwenye udhehebu ana haki kwa maana waliopo humo kwenye hii NGO a.k.a CPT ni wakristo pekee tena wa baadhi tu ya madhehebu. ieleweke jamani
 
Back
Top Bottom