Wanatakiwa kuweka tangazo kuwa unywaji wa soda kupita kiasi ni hatari kwa Afya yako

Wanatakiwa kuweka tangazo kuwa unywaji wa soda kupita kiasi ni hatari kwa Afya yako

Dah....! Sijui tukimbilie Wapi? Niliwahi Kusoma Sehemu Daktari Mkubwa kabisa pale Jakaya Muhimbili anaonya Unywaji Wa Maji kupita Kiasi ni Hatari Kwa Afya Yako....!
Yani nilishangaa kwa kweli,wakati kuna Dr mmoja nilikuwa nikiiuguliwa na watoto ghafla na hatuwezi kwenda Hosp usiku huo nikikuwa nikimpigia simu kutaka ushauri Wa haraka,ye alikuwa ananishauri nisipanic ila nimpe mtoto maji ya kutosha mpaka pakuche nimlete Hosp.
 
Wote mtakufa lakini wewe ambae hujali afya kisa kigezo cha utakufa tu, utakufa kifo cha mateso mno, maisha kwako yatakuwa mafupi.
Naona uko na umri sahihi wa mtu kuishi hapa duniani..kwamba sote tufe sawa sawa na unavyotka wewe..uhai na uzima ajuaye mola..unaweza uishi maisha yote ya kiafya..ila kesho ukagongwa na pikipiki ukafa.

Kwa kusema hivyo sijakataa watu wasishi maisha ya kiafya..ila kupangia uhai wa kuishi humu duniani ndio sitaki.

#MaendeleoHayanaChama
 
Soma kwenye soda Kuna baadhi wameandika 60g/500ml. Kijiko kimoja Cha chakula ni kama 10g. Ukinywa soda moja ya take away jua umebugia kama vijiko 6. Ikumbukwe kwamba mwili ukipokea sukari basi kongosho huachia insulin kuchakata sukari. Utumiaji kupita kiasi ni hatari kwa afya yako.
 
Zaman mgonjwa wa moyo tulikariri ni yule mnene, hivohivo presha na kisukar tulidhani wanene ndio wenye hiyo hatari, lakin saizi ata uwe kimbao mbao hayo magonjwa hayachagui.

Kikubwa kuzingatia mlo mzr tu. Maji ni kinywaji fulani kitamu lakini hakina sukari.

Mimi naelekea kumaliza mwaka sasa sijatumia soda yoyote au juice yoyote 😁, najua kuna mtu atakuja kusema ni ukata nilio nao, ila ndiyo nakubali😁😁 ila huwa sipo interested na hivyo vinywaji.
Upo mkoa gani .
🤣😂Karibu siku ya Christmas upate soda
 
Ya kutosha ni tofauti na kupita kiasi.

😂😂😂Kupita kiasi ni kama yale unameza ukizama majini, unakufa.
Sasa boss maji ni Dawa,ukiweza kwa we we MTU mzima kupata walau Lita tano daily hata kama uko addicted na soda hayo maji yata flash sumu zote mwilini kwa njia ya mkojo.

Iko kitu inaitwa mo pawa,au azam energy drink nimekuta kule kanda maalum eti watoto wanazinunua Dukani kawaida.
 
Baada ya WWII dunia ilikumbwa na mtikisiko wa uchumi. Chakula kilitolewawkwa lesheni. Wakulima na wafugaji ndiyo walimudu kunywa chai ya maziwa na mayai vionjo vingine kama bacon.

Wakati huo ukiinekana na tumbo kubwa unapata heshima kuwa maisha umeyapatia.

Dunia inakwenda haraka sana.
 
Magonjwa ya figo etc yanatamalaki sasa
 
Soda na Soft drinks zote ni hatari kwa afya ya binadamu. Binadamu hakuumbwa kubugia sukari nyingi namna anayobugia leo. Sukari nyingi huleta unene wa kupitiliza, kitu ambacho huleta kisukari, magonjwa ya moyo nk.

Ni wakati sasa, kama ilivyo kwenye bia; Kwa matangazo yote ya vinywaji laini na kwenye chupa zao kuwa na tangazo la onyo kuwa unywaji kupita kiasi ni hatari kwa afya yako.
Tambua ya kwamba kitu chochote anachotumia binadamu ni hatari pia kwa afya yake.
 
Back
Top Bottom