PostGE2025 Wanatumia nguvu nyingi kuondoa uhai wa raia ili kupata madaraka na kufanya ANASA

PostGE2025 Wanatumia nguvu nyingi kuondoa uhai wa raia ili kupata madaraka na kufanya ANASA

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

ChekoFagia

Senior Member
Joined
Sep 20, 2025
Posts
115
Reaction score
339
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Roma Mkatoliki, ameshangazwa na kile anachoeleza kuwa ni matumizi makubwa ya nguvu, including kuua watu, yanayofanywa na baadhi ya viongozi wa Tanzania kwa lengo la kulinda madaraka wanayoyatumia kujinufaisha badala ya kuwahudumia wananchi.

Roma anasema fedha zinazopatikana kutokana na wizi wa mali ya umma hazitumiki kujenga msingi wa maendeleo, bali zinatupwa kwenye anasa na starehe zisizo na mchango kwa jamii.

Katika ujumbe wake, Roma anaibua maswali mazito ya uwajibikaji: viongozi wanawezaje kujivunia madaraka ambayo msingi wake ni uhai wa maelfu waliopotea? Anaeleza kuwa wengi wa viongozi hao husafiri mara kwa mara kwenda Dubai, Uingereza na Marekani, na kuona kwa macho yao maendeleo ya mataifa mengine, lakini bado wanarudi nchini bila hasira ya kubadilisha chochote.

Kwa miongo miwili sasa, anasema, jiji la Dar es Salaam halijaongeza Mall kubwa ya kisasa zaidi ya Mlimani City na iko vile vile miaka yotr; jambo analoliona kama ishara ya kukwama kwa fikra za maendeleo.

Roma pia anazungumzia ukosefu wa uwekezaji katika sekta muhimu kama michezo. Anaamini ujenzi wa sports academies ungeweza kuwaokoa vijana wengi wanaozagaa mtaani na kuingia kwenye vitendo viovu, huku akisisitiza kuwa fedha zinazopotea kwenye anasa za viongozi ni kubwa kuliko gharama za miradi kama hiyo.

Ujumbe wake unagusa pia taasisi za usalama: anahoji ni vipi katika mwaka 2025, taasisi kubwa na nyeti kama Polisi bado zinatumia daftari kuhifadhi taarifa za watuhumiwa, wakati mifumo ya kisasa kama RMS ina gharama ndogo kuliko hata gari moja linaloendeshwa na kiongozi wa juu. Kwa mtazamo wake, hili ni mfano halisi wa kipaumbele kilichopotoka.

Kauli hizi zimewasha mjadala mkubwa kuhusu uwajibikaji, matumizi ya fedha za umma, na uongozi unaotanguliza maslahi ya wananchi. Wananchi Forum inaendelea kufuatilia hoja hii ambayo imeibua hisia nzito na maswali ambayo bado hayajapatiwa majibu rasmi.
1763982801391.jpeg
 
Back
Top Bottom