Wanatunga sheria za kuwakomoa wengine wanasahau kuna siku zitawagusa pia!

Wanatunga sheria za kuwakomoa wengine wanasahau kuna siku zitawagusa pia!

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
6,846
Reaction score
10,288
Kuna video moja inayohusu nchi ya mbali kabisa ya Tataipa.

Huko kulikuwa na waziri aliekuwa anapitisha sheria kuhusu mambo ya jela, alipitisha sheria ngumu sana lakini sheria moja ni wafungwa wapewe ugali na mboga chungu.

Lahaula. Siku moja akampinga bosi wake, huku na huku kapigwa miaka 10 bila ya hukumu (yaani haikumpita mahakamani ni amri tu).

Kuingia jela akafungiwa katika chumba cha peke yake, wakati wa chakula kapelkewa dona kwa mboga mbichi.

Siku ya kwanza waziri mfungwa siku hakula, alipoulizwa na mpishi mfungwa mwenziwe akamwambia leo nimeshiba nimekunywa chai nuzri nyumbani.

Mpishi mfungwa akacheka sana, akamwambia kama hukula leo kesho, kesho kutwa , keshokutwa utakula.

akamwambia ulipokuwa waziri umetunga sheria hizi ulidahni hii jela wewe haikuhusu kwa ajili yetu tu.
sasa hicho ndio chakula chako. Waziri mfungwa alilia sana. Hii story ni ya kweli wadau sio ya kutunga

Kila mtu anapaswa kutendewa sawa mbele ya sheria. Surah Al-Ma'idah (5:8) inasema: "Enyi mlioamini, simameni kwa haki kwa ajili ya Allah, hata kama ni dhidi ya nafsi zenu, wazazi wenu, au jamaa zenu."

Tunakumbushana wadau. hii dunia sio yetu, tujitahidi tutendane mema na haki tupeane.
 
Kila mtu anapaswa kutendewa sawa mbele ya sheria. Surah Al-Ma'idah (5:8) inasema: "Enyi mlioamini, simameni kwa haki kwa ajili ya Allah, hata kama ni dhidi ya nafsi zenu, wazazi wenu, au jamaa zenu."
Tunakumbushana wadau. hii dunia sio yetu, tujitahidi tutendane mema na haki tupeane
Kuna mawaziri hapa waliandaliwa vyumba maalumu vya kwenda kufungiwa
 
Back
Top Bottom