Hello JF,
Wanaume kwanini mnakuwa hamjiamini ukiwa kwenye mahusiano Na mwanamke au ukioa mke aliyekuzidi kipato ingawa unakuta anakuheshim vizurii.
inferiority inampelekea mpaka mwanaume kuanza kumnyanyasa mwanamke kimwili,kiakili Na kihisia....why ebu mtusanue
Wengi mnakimbilia kwenye weak inferiority, sijui nani kawadanganya!
Iko hivi, kwa asili mwanaume anapenda mwanamke mwenye haiba za kike(tabia za asili za kike).
Heshima, kujishusha, utii hivi ni vitu vya kawaida kwa wenye haiba za kike. (haitaji semina toka kwa chris mauki)
Hata mashoga wako more romantic kuliko wanawake sijui walio soma, au wenye pesa.
Ni ngumu kwa mwanaume kuishi na mwanamke mwenye sifa za kiume, hiyo ni ngumu mnoooo,
Bila kujali una pesa, elimu au uzuri, cheo.
Hata kama utakuwa naye ni suala la muda tu, lazima atafute mwenye ukike kike zaidi.
Atakwenda kule uanaume wake unako kamilishwa.
Kukosa haiba za kike, ni kukosa kuwa na radha kitandani pia.
Sasa ya nin kuhangaika kufukuzia mtu ambaya najua hata utamu hana?
Wewe ongea yako ni kama kamanda wa jeshi na makuruta wake,
Unapenda kukasirika ovyo,
kupenda ugomvi kila wakati
kusababisha kelele za kila wakati,
wewe ndio mtungaji na mtoaji wa sheria, na mwanaume ni mtekelezaji
yaani mwanamke mflame mwanaume mtumwa!
Wakati huo huo kuna mtoto;
anaongea kwa sauti nyororo
Ana aibu zile za kike kike,
yuko natural
Ana lugha rafiki(hakuna ubabe)
mvumilivu wa mambo
Ni chanzo kikuuu cha faraja.
hata kulalamika ana lalamika kwa mahaba!!!
Pesa haitaki kelele!