Wanaume kupika na kupakua ni ushamba jamani??

Wanaume kupika na kupakua ni ushamba jamani??

Hausaidii,bali mnasaidiana(that's what i said)..Ni sawa na kusaidiana katika matumizi ya home,kusaidiana kufua nguo...Nk...Ndo maana nikasema mimi(maana ishajengeka,hasa Tanzania na Afrika kwamba wababa wao hupikiwa tu ama na mke ama na house maid) so narudia tena mimi mara nyingi weekend huandaa chakula twala mimi,mke wangu na mtoto wetu pia na msaidizi wetu wa kazi za nyumbani...So si vibaya kusaidiana kupika bana(narudia tena kusaidiana kwa maana ya kwamba kila mtu ana wajibu ya kupika,simaanishi kufuata ratiba hapa)
Mkuu Bala inamaana siku hiyo wewe ukiiingia jikoni... ni mwanzo mwisho mpaka kiive wengine wanakua hawapo jikoni?
 
birigita mbona "status"yako haiendani na maneno yako?kaazi kweli
lugha ya kuelezea jinsi mwanamke (mwenye akili)anavojisikia jinsi mwezie anavomsaidia nyumbani,HAIELEZEKI KABISA kwa jinsi ya kibinadamu!!
 
Du! Wacha nikachukue kozi ya upishi!🙄

hahaaaaaaaaaaaaaa, mkuu umenichekesha aisee!!! yani hadi leo kupika nehi che?? we haya we...

wenzako huwa wanalamba hata vya watu kwa kuwapikia tu.. si umesikia tangazo la simu lile jamaa kavuta mzigo sababu ya kupika tu?
 
Culture (utamaduni) wa mataifa mbalimbali - kuna mataifa mengine wanapeana zamu kupika - baba na mama - lakini culture yetu ya Kitanzania sijui imeigwa toka wapi??? ndio imeletea mwanamke awe mpishi na kwamba kupika ni kazi ya wanawake - Hata hivyo environment - hebu twende kwenye nyumba ya kupanga - vyumba sita - watu wote wanapika kwenye corridor au kwenye jiko moja maalumu - imagine wife yuko chumbani na husband ndio yuko pale jikoni na kina mama nanihii - dada fulani - wanapika kila mtu na jiko lake???? unapata picha gani???? Otherwise - turudi kwenye msahafu (Bible) "Mungu akasema nitamfanyia adamu msaidizi" - so mke ni msaidizi tu - jamani kupika kazi ya mwanamme - ila kwa vile anazidiwa na majukumu sometimes inabidi mama asaidie baadhi ya majukumu e.g. kupika
Wanaume wengi wana mfumo dume - hivyo wanataka wakae waambiwe tu chakula tayari.. wale waondoke - hawagusi chochote - huo ndio ushamba - ila katika familia mwanaume kupika na mwanamke kupika siku ingine - inaonyesha:
- umoja, upendo, democracy (genderwise), mapenzi, maendeleo, social - na hali ya kuleta different tastes - hata kwenye mlo
angalizo: tuwafundishe watoto wetu (wakike na kiume) kazi zote ikiwemo kupika - ili waepukane na mfumo dume - na wazazi wote tuwe mfano.
all in all mwanaume kupika sio ushamba
 
Mkuu Bala inamaana siku hiyo wewe ukiiingia jikoni... ni mwanzo mwisho mpaka kiive wengine wanakua hawapo jikoni?

Mangi...Kuna siku huandaa kila kitu na kuna siku husaidiwa(na mama) kuandaa vitu(kulingana na recipe ya siku hiyo) kama kumenya nyanya,kukata vitunguu ,capsicum,carrots,kuandaa vyombo n.k...Ndo maana nikasema mara nyingi husaidiana na mama wa mtoto wangu kwenye mambo ya upishi(hasa weekend maana mimi mara nyingi weekend hushinda nyumbani na familia)...So siku nikiingia jikoni,huwa ni mimi na Mrs tu,house maid huwa anakaa mbali na jiko mida hiyo
 
Msiposaidiwa shida, mkisaidiwa shida na mnatuona washamba na labda tumeshalambishwa limbwata! sijui tukimbilie kambi gani! Labda njemba hapendi ugali unaopikwa na mkewe.....just thinking aloud 🙂

Hawana jema! Ukirudi mapema nyumbani shida, ukipita baa shida, ukimdekeza mwanamke kupita kiasi anakuita zoba, ukiwa mkali anasema you don't care!

Yaani wanawake ni jipu la kwapa aisee!!!
icon10.gif
 
Mkuu Bala inamaana siku hiyo wewe ukiiingia jikoni... ni mwanzo mwisho mpaka kiive wengine wanakua hawapo jikoni?

hahaha lakini nyie mbona mnatoa tafisiri kivingine..
maisha ni kusaidiana hata kukata nyanya kuosha mchicha ...ni mambo ya kusaidiana tu hayo
 
hahaha lakini nyie mbona mnatotafisiri kivingine..
maisha ni kusaidiana hata kukata nyanya kuosha mchicha ...ni mambo ya kusaidiana tu hayo

yaani wengine wanalifanya suala la kupika jukumu la mwanamke tu....
starehe ya maisha kusaidiana bana
 
Hawana jema! Ukirudi mapema nyumbani shida, ukipita baa shida, ukimdekeza mwanamke kupita kiasi anakuita zoba, ukiwa mkali anasema you don't care!

Yaani wanawake ni jipu la kwapa aisee!!!
icon10.gif

ukinyanyua mkono linauma, ukishusha ndo kabisaaaaa

hivi huyo mwanamke wa hivo kweli yupo Masaki?
 
Sawa nimekusoma.............mnasaidiana
tofauti hapa ni kewamba mimi nina passion ya kupika vitu flani flani....for the family na ndo maana kuna wakati nikisema nitapika, ninaulizwa utapika nini? kama unapika nanihiii.(sikisemi hapa) niwashtue na wakina flani waje kushinda huku leo?

(mkuu, 90% ya wakina dada wanaofanya kazi ziwe za kuajiriwa au kujiajiri ambazo zipo tight.........hawaingii jikoni kabisa, wasichana wa kazi ndo wanapika, sasa wewe ukisema mnasaidiana, unakuwa unasaidiana na msichana wa kazi au?)

Nami nimekusoma mkuu,Naona hujanielewa kabisa mkuu wangu,nimekwambia mara nyingi siku za weekend mimi huingia jikoni kuandaa chakula(si kila siku),nielewe hapa kwanza...Siku nikiingia jikoni House maid yeye hupumzika(ama hufanya kazi nyingine) sana sana mke wangu ndo huja jikoni kunisadia kazi ndogo ndogo za jikoni,mimi ndo huwa starling siku hiyo...Halafu,binafsi napenda sana kula chakula kilichoandaliwa na mke wangu,wote tunafanya kazi so mlo wa mchana hatuli nyumbani...Kwa mlo wa usiku hata kama Msaidizi wa nyumbani anaandaa mama watoto yeye hujitahidi kumuelekeza nini aandae kwa ajili yangu na mara nyingi huandaa chakula cha kula mimi baba watoto wake....Yaani ni aina fulani tu ya mapenzi(hasa kwa sisi wapendanao)....
 
ukinyanyua mkono linauma, ukishusha ndo kabisaaaaa

hivi huyo mwanamke wa hivo kweli yupo Masaki?

Rejea kwenye mada hapo juu. Kuna mwanamke kamcheka huyo mwanaume waliyemkuta anamsaidia mkewe kupika ugali. Unatemea nini kutoka kwa mwanamke kama huyo kama siyo maumivu ya jipu la kwapa?
 
Hakuna ubaya kumsadia mamaa kupika. Ni namna f'lani ya kuonyesha upendo na kujali. Hongera kwa wote wenye ratiba hiyo.
 
Rejea kwenye mada hapo juu. Kuna mwanamke kamcheka huyo mwanaume waliyemkuta anamsaidia mkewe kupika ugali. Unatemea nini kutoka kwa mwanamke kama huyo kama siyo maumivu ya jipu la kwapa?

mambo mengine huwa nahisi ya kusadikika zaidi..........
 
yaani wengine wanalifanya suala la kupika jukumu la mwanamke tu....
starehe ya maisha kusaidiana bana
bht mie nimeweka na ratiba jtatu mpaka Jpili msije kunimeza jamani tunasaidiana tu
 
Sielewi ajabu iko wapi mwanaume kupika na kupakua chakula. Mwanaume anapooa anatafuta msaada juu ya mambo ambayo hana uwezo nao, tena anataka uhakika wa kuwpata msaada huo wakati wowote anapoutaka. Kama ni kupika, mwanaume anao uwezo wa kupika kwa ladha anayoitaka na pengine anaweza kupika kumzidi mwanamke.

Msaada anaoutaka kila mtu mzima anaujua. Hana ufariji ambao ni mwanamke tu aliyejaaliwa kuwa nao. Adam alipoumbwa ilionekana wazi atauhitaji na ndio maana Hawa ilibidi afanyike kuwapo. Ni ustaarabu wa binadamu unaomfanya aoe, vinginevyo angekuwa mbuzi asingeoa lakini faraja bado akaipata.
 
Kama yepi? Mwanaume kupika ugali wakati mkewe anasoma gazeti sebuleni au?

hapana, hayo ya mke kumwona mume zoba kwa kuwa anamsaidia shughuli za nyumbani.....
 
hapana, hayo ya mke kumwona mume zoba kwa kuwa anamsaidia shughuli za nyumbani.....

Kwa jamii na utamaduni wa sisi Waafrika ndivyo atakavyoonekana kwa walio wengi!
 
Back
Top Bottom