Wanaume kuweni makini sana kuoa wanawake waliotoka Vyuoni

Inasikitisha Sana 😥
 
Kweli ila bado naipinga hiyo hoja eti utii umebase kwenye uchumi tu. Uchumi ni nyenzo tu ila kutomtii mwanaume kumechimbuka ndani zaidi ya uchumi.
 
Basi ifike pahala muiambie jamii kwamba na ninyi ni weak, na mnaweza kuwa victims kama wanawake tu, hamko strong kama mnavyoiaminisha jamii ili ijulikane moja
Unaona sasa, kumbe mawazo yako ndo haya! Umejificha wee kumbe unawaza eti mwanaume awe weak kama mwanamke? That'll never happen, men are becoming weak kutokana na mifumo inayo wabeba wanawake, masculinity inazidi kuwa toxifeid ila kamwe mwanaume kuwa kama mwanamke.
 
Hata biashara msiwafungulie
 
Na hadi leo Baba aliwaasa kaka zangu na wadogo zangu wa kiume akasema oa mwanamke mwenye elimu ya kawaida wanawake wenye elimu kubwa ndoa kudumu mtihani aisee niliamini
najaribu kufikiria kama nawe una elimu kubwa au kama mzee ana watoto wengine wa kike anataka kutufundisha nini?
Kwamba
1. Msisome
2. au hamtakiwi kuolewa

Lakini vyovyote iwavyo,
ndoa ni swala mtambuka, aghalabu tumeona wengi wakioa hao la saba, tena pengine kijijin kabsa huko lakin baadae hukengeuka na wapo walio oa wasomi na maisha yanaenda; na kinyume chake pia
Kwahiyo naweza kusema, yamkini ndoa ni bahati na kuweza kutumia ubongo wako vizuri, ila sion kama kuna kanuni kuhusu hili jambo zinaweza kutengenezwa abadani.

Hata hivyo, ni vizuri kujifunza kutoka katika jamii.

Wassalam.
 
Hii comment inatakiwa kuwa pinned 📌 📌
 
Malipo ni hapa hapa duniani unaweza usione ama ukaona lkn majibu lazima upate baadae
 
Huyu mwanamama anastruggle sana kuangusha kingdom ya kiume.

Akifanikiwa atapandisha jinsia ya kike pale juu
 
Upo sahihi sana, ila usahihi wako utaendelea kuongeza single mothers wengi mitaani
 
Basi ifike pahala muiambie jamii kwamba na ninyi ni weak, na mnaweza kuwa victims kama wanawake tu, hamko strong kama mnavyoiaminisha jamii ili ijulikane moja
Tunazungumzia kutendeana haki, sasa mwanamke akinivizia nimelalala akaniwahi kunidhuru hata kama nina miguvu nitamzuiaje? Utasema mimi ni weak?
 
Kweli ila bado naipinga hiyo hoja eti utii umebase kwenye uchumi tu. Uchumi ni nyenzo tu ila kutomtii mwanaume kumechimbuka ndani zaidi ya uchumi.
Hili nafikiri nimeshakujibu kule siwezi kuandika jambo lile lile kila mara
Aiseee mnasikitisha sana sasa hiyo mifumo inayowabeba wanawake inaendeshwa na kina nani na kwa faida ya nani, na kwanini wanaume wanaruhusu wanawake wabebwe ilihali wao ndio watawala na wana uwezo na nguvu kuliko wanawake, huwa nashindwa kuelewa inakuwaje mnalalamikia matatizo ambayo mmeyaruhusu wenyewe (maana wanawake ni dhaifu) sasa mnamlalamikia nani ayarekebishe mbona mnafurahisha
 
Tunazungumzia kutendeana haki, sasa mwanamke akinivizia nimelalala akaniwahi kunidhuru hata kama nina miguvu nitamzuiaje? Utasema mimi ni weak?
Na unadhani ni kwanini mwanamke akudhuru kwa kukuvizia yani mnachoshindwa kuelewa (au pengine mnaelewa ila hamtaki kukubali) ni kwamba haya wanayofanya wanawake sasa hivi waliyapandikiza wanaume wa zamani waliokuwa na mfumo dume wa kipuuzi, haya ni matokeo ya kuwakandamiza na kuwanyima sauti na uhuru wanawake kwa muda mrefu na matokeo yake walipoanza kutetewa na kupata upenyo wakatake advantage ya hilo, tatizo lenu ninyi hili jambo mnaliangalia juu juu tu hamtaki kujua mzizi wake mnadhani eti linaanzia hapa au liliibuka tu out of nowhere na mkiambiwa ukweli mnakimbilia kuita watu mafeminist
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…