Wanaume kuweni wa kweli basi dah!

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
3,448
Reaction score
7,972
Kuna wanaume anapokuwa anakuaproach utadhani anayoyasema ni ya kweli

Juzi moja nikakutana na mkaka , kama kawaida akaanza swaga nikamwambia nipe muda kidogo nichanganue maneno yako

Leo nikawa nimetoka kwenda mahali mbali kidogo kwa rafiki yangu,akawa amenipigia sim tuonane nikamwambia nipo mbali kidogo ila muda si mrefu nitakuja mjini

Akaniambia nina usafiri vipi nikufuate..nikamwambia utakuwa umenisaidia sana

Basi baada ya dakika kadhaa akaja akanichukua ,wakati anadrive akaanza hili gari langu siku hizi linatumia mafuta vibaya,..nikadakia ooh kumbe gari hili ni lako"akaniambia yes ni gari langu nilinunua hata miezi mitatu haijapita,,nikamwambia hongera!
Mara akapigiwa sim nikahisi akaulizwa uko wapi akajibu maeneo tulipo,sijui hawakuelewana na aliyempigia akakata sim

Baada ya dakika kadhaa si gari likasimamishwa na mzee mwenye kitambi,acha tuvurushwe kutoka kwenye gari huku mzee anagomba kuwa nani kakwambia uchukue gari langu

Basi kijana akakosa la kuniambia akawa ameinamia kichwa chini,..ikabidi nipande daladala nikamuacha mwenyewe amesimama njiani maana alikoswa la kuniambia

Wanaume kupenda sio lazima ujitape vitu ulivyonavyo,utapendwa tu hata kama huna gari au baiskeli
 
Pole sana hila unaposema wanaume unakosea wengine atuna hayo mambo
 
Mimi nina gari njoo kwangu hutopanda tena daladala
 
Hilo sio tatizo kama wewe ni mwelewa,he just wanted to impress you,
If you were commited to him,it was time to tell him that,"usijali sweetie,I know you wanted to impress me,cause you love me,but our love is not about having or not having a car or material things,it is you I love babies,not a car or whatever....'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…