Wanaume kuweni wa kweli basi dah!

Wanaume kuweni wa kweli basi dah!

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Sipati picha mlivyovurumushwa
 
Kuna wanaume anapokuwa anakuaproach utadhani anayoyasema ni ya kweli

Juzi moja nikakutana na mkaka , kama kawaida akaanza swaga nikamwambia nipe muda kidogo nichanganue maneno yako

Leo nikawa nimetoka kwenda mahali mbali kidogo kwa rafiki yangu,akawa amenipigia sim tuonane nikamwambia nipo mbali kidogo ila muda si mrefu nitakuja mjini

Akaniambia nina usafiri vipi nikufuate..nikamwambia utakuwa umenisaidia sana

Basi baada ya dakika kadhaa akaja akanichukua ,wakati anadrive akaanza hili gari langu siku hizi linatumia mafuta vibaya,..nikadakia ooh kumbe gari hili ni lako"akaniambia yes ni gari langu nilinunua hata miezi mitatu haijapita,,nikamwambia hongera!
Mara akapigiwa sim nikahisi akaulizwa uko wapi akajibu maeneo tulipo,sijui hawakuelewana na aliyempigia akakata sim

Baada ya dakika kadhaa si gari likasimamishwa na mzee mwenye kitambi,acha tuvurushwe kutoka kwenye gari huku mzee anagomba kuwa nani kakwambia uchukue gari langu

Basi kijana akakosa la kuniambia akawa ameinamia kichwa chini,..ikabidi nipande daladala nikamuacha mwenyewe amesimama njiani maana alikoswa la kuniambia

Wanaume kupenda sio lazima ujitape vitu ulivyonavyo,utapendwa tu hata kama huna gari au baiskeli
Hahahaha
Nimecheka sana

Ahsante kwa story

Tofauti
Mimi nikimtongoza dada sijisifii na akiniuliza unafanya kazi huwa nadanganya namweleza kazi tofauti mfano deleva wa guta ili hali nimeajiriwa Kampuni flani... maisha ninayoishi magumu n.k so huwa wanakata tamaa.
tatizo moja tu ambalo Mimi ninalo na huwa hawanikubalii ni aibu
 
Mimi sio muongo,nakwambia cute kazi yangu ni kuuza maji kwenye madumu hapa soko la magomeni dar,njoo nikulav basi..
 
Ndiyo maana nimejizoelea daladala.Mtu akija na bajaji na namheshimu tu .
 
Mabinti mnapenda magari
Ndiyo maana nimeamua kuweka cctv
 
Back
Top Bottom