Wanaume mna tatizo gani?

Wanaume mna tatizo gani?

thubutu!!!
Ngoja wakukimbie kama miaka 2

tutakuona unalibeba kopo kutoka mbagala hadi mwananyamala kwa mguu mchana kweupeee.

sio kwamba hataki relationship ila hataki ndoa kwa sasa,ama ndo mimi sijaelewa?
 
Nilikutana na huyu kaka mwaka 2007 kwenye harusi ya dada wa rafiki yangu.Huyu rafiki yangu ni kipenzi sana na amekuwa kama ndugu yangu,.
Hiyo harusi nakumbuka ukumbi ulikuwa ni pale msasani. Tulipotoka huyu mkaka nampa jina la Y akasema twende tukapate vinywaji sehemu nyingine na kweli tukatoka mimi,huyo rafiki yangu na yeye.,.
Aliniomba namba ya simu nikampa.
Kipindi hicho nilikuwa naishi upanga,akawa ananifatilia sana lakini sikumpenda kwa kweli kwa hiyo sikumkubali.
Alinifatilia mpaka mwaka jana na nilikutana nae mara kadhaa,tunapiga story na kupata drinks then ananirudisha home.
Sasa mwaka huu mwezi wa kwanza kuna rafiki yangu alikuwa anaolewa ikabidi nije dar kwenye harusi.Laa haula bwana harusi ni mr.Y!
Nilishukuru Mungu kuwa sikulala nae na wakati wa kwenda kutoa pongezi,nilipompa mkono akanitekenya nilishtuka kwa kweli nikamchek my friend akawa yuko tu busy kuwahug wageni waalikwa.Wakati wa dancing akanifata kudance na mimi akaniambia bado ananipenda halafu akanikonyeza!nilimshangaa sana.Na mpaka sasa najiuliza maswali mengi hivi wanaume wana matatizo gani?
Kwenye siku ya ndoa yako unamwambia mtu mwingine unampenda je ni sahihi?


Hatuna matatizo. That's how we are, that's our nature.
 
Mahusiano ni headache sana! Unaweza ukawa na amani siku zoote, lakini from no where amani inapotea kwa sababu ya kumpenda mtu ambaye mnamatch kifikra kwa asilimia sitini tu. Good enough siku hizi watu wote tuko busy. Kukutana ni usiku tu na kila mtu anakuwa amechoka, hivyo minimum kero!
Back to the topic: Umechezea bahati dada yangu. Hilo lijamaa lilikuwa linakupenda kweli, hivyo ungekubali kuolewa nalo kama uliwahi kuhisi asilimia angalau hamsini za kulipenda.
 
Mahusiano ni headache sana! Unaweza ukawa na amani siku zoote, lakini from no where amani inapotea kwa sababu ya kumpenda mtu ambaye mnamatch kifikra kwa asilimia sitini tu. Good enough siku hizi watu wote tuko busy. Kukutana ni usiku tu na kila mtu anakuwa amechoka, hivyo minimum kero!
Back to the topic: Umechezea bahati dada yangu. Hilo lijamaa lilikuwa linakupenda kweli, hivyo ungekubali kuolewa nalo kama uliwahi kuhisi asilimia angalau hamsini za kulipenda.

sikumpenda hata kwa asilimia moja ya kimapenzi.
 
Alikupenda, wewe hukumpenda, Alipomaanisha wewe hukua tayari kuona utayari wake, Sasa wenzako wameona na wameshamaliza kila kitu, Mwache aangalie ndoa yake
 
thubutu!!!
Ngoja wakukimbie kama miaka 2

tutakuona unalibeba kopo kutoka mbagala hadi mwananyamala kwa mguu mchana kweupeee.

hahahaha! Mi habari za ndoa sipendi kuzisikia. Hivi inawezekana mkaoana halafu kila mtu akaishi kwake eeh? Au tukaishi pamoja ila kila mwaka tunapeana likizo? Lol.
 
Siku naoa nami ktk kudensi nilimwambia mdada mwingine nampenda akachekelea kweli!....mwalimu wenu mmoja!
 
kawaida hiyo kwani moyo unavyumba vingi vya kuhifadhi mapendo. Ila kimsingi ulimdhulumu kukupenda kwani bado anahitaji nafsi yako. We mpage tu kihalali
 
Ulikuwa unatoka nae out halafu unamdengulia sasa imekula kwako na roho inauma. Thats the game man plays hata kina dada,unakuwa na watu wawili stand by,mmoja akizingua anachukua yule aliyetayari,ni mambo ya sampling tu kabakabana
 
1. Aliniomba namba ya simu nikampa.
Alinifatilia mpaka mwaka jana na nilikutana nae mara kadhaa,2.tunapiga story na kupata drinks then ananirudisha home.
Sasa mwaka huu mwezi wa kwanza 3. kuna rafiki yangu alikuwa anaolewa ikabidi nije dar kwenye harusi. Laa haula bwana harusi ni mr.Y
Kisa chako si cha ajabu kufanywa na baadhi ya wanaume na hata baadhi ya wanawake. Lakini kuuliza "Wanaume mna tatizo gani?" ni kuwachanganya wanaume na hata wanawake wote katika kapu moja.

Katika kuzungumzia "urafiki baina ya wanaume na wanawake", wengi hapa walikuja na wazo kuwa "kitu hicho hakiwezekani", wanaamini ama mnakuwa wapenzi au kila mmoja kivyakevyake; [jambo ambalo mimi ninapingana nalo]. Urafiki baina ya mwanamume na mwanamke unawezekana, cha muhimu ni kuweka mipaka tangu mwanzo, jambo ambalo wewe ulifanya kwenye 1. nyekundu la kumpa nambari ya simu lakini ukakosea zaidi kwenye 2. nyekundu kwa kumfanya rafiki mtu ambaye ulijua kuwa alikuwa hakutaki kama rafiki tu.

Na hiyo 3. nyekundu bado nina mashaka kuwa "rafiki yako" kwa maana ya rafiki anafika hadi anaolewa ukiwa hujui bwana arusu ni nani. Lakini hayo yote ni maangalizo tu, ninachotaka kukushauri, kama walivyo kushauri wengine, kwa heshima ya huyo "shoga yako", achana kabisa kabisana huyo fataki na hata na shoga yako. Kuwa kwako karibu na shoga yako ni sawa na kuwa karibu na huyo jamaa.
 
Wanaume hatuna matatizo ila wakati mwingine tunazidiwa nguvu na hawa wenzetu. Lakini mwanaume kutongoza ni kitu cha kawaida. na je, nauliza wanawake mna matatizo gani kuwakubalia wanaume ambao mna uhakika kuwa wameoa lakini bado mnatoka nao na kuwapa kile wanachotaka?
 
Back
Top Bottom