Kabakabana
JF-Expert Member
- Aug 5, 2011
- 5,550
- 1,165
- Thread starter
-
- #121
Ooh! Nimehairisha kuolewa.
Kabakabana unanikumbusha nilivyokuwa Copacabana Beach.
Mi napita njia tu !
thubutu!!!
Ngoja wakukimbie kama miaka 2
tutakuona unalibeba kopo kutoka mbagala hadi mwananyamala kwa mguu mchana kweupeee.
jamaa dah! Kwa kweli ni mkali haswaa. Mpaka alikukonyeza?
Are you sure? Then hujaona hii dunia ilivyo na ubaguzi....so are u supposed to close ur eyes?
Nilikutana na huyu kaka mwaka 2007 kwenye harusi ya dada wa rafiki yangu.Huyu rafiki yangu ni kipenzi sana na amekuwa kama ndugu yangu,.
Hiyo harusi nakumbuka ukumbi ulikuwa ni pale msasani. Tulipotoka huyu mkaka nampa jina la Y akasema twende tukapate vinywaji sehemu nyingine na kweli tukatoka mimi,huyo rafiki yangu na yeye.,.
Aliniomba namba ya simu nikampa.
Kipindi hicho nilikuwa naishi upanga,akawa ananifatilia sana lakini sikumpenda kwa kweli kwa hiyo sikumkubali.
Alinifatilia mpaka mwaka jana na nilikutana nae mara kadhaa,tunapiga story na kupata drinks then ananirudisha home.
Sasa mwaka huu mwezi wa kwanza kuna rafiki yangu alikuwa anaolewa ikabidi nije dar kwenye harusi.Laa haula bwana harusi ni mr.Y!
Nilishukuru Mungu kuwa sikulala nae na wakati wa kwenda kutoa pongezi,nilipompa mkono akanitekenya nilishtuka kwa kweli nikamchek my friend akawa yuko tu busy kuwahug wageni waalikwa.Wakati wa dancing akanifata kudance na mimi akaniambia bado ananipenda halafu akanikonyeza!nilimshangaa sana.Na mpaka sasa najiuliza maswali mengi hivi wanaume wana matatizo gani?
Kwenye siku ya ndoa yako unamwambia mtu mwingine unampenda je ni sahihi?
Mahusiano ni headache sana! Unaweza ukawa na amani siku zoote, lakini from no where amani inapotea kwa sababu ya kumpenda mtu ambaye mnamatch kifikra kwa asilimia sitini tu. Good enough siku hizi watu wote tuko busy. Kukutana ni usiku tu na kila mtu anakuwa amechoka, hivyo minimum kero!
Back to the topic: Umechezea bahati dada yangu. Hilo lijamaa lilikuwa linakupenda kweli, hivyo ungekubali kuolewa nalo kama uliwahi kuhisi asilimia angalau hamsini za kulipenda.
thubutu!!!
Ngoja wakukimbie kama miaka 2
tutakuona unalibeba kopo kutoka mbagala hadi mwananyamala kwa mguu mchana kweupeee.
hehe na lile gauni langu nilivae wapi?
utalivaa kwenye besdei. Lol.
Kisa chako si cha ajabu kufanywa na baadhi ya wanaume na hata baadhi ya wanawake. Lakini kuuliza "Wanaume mna tatizo gani?" ni kuwachanganya wanaume na hata wanawake wote katika kapu moja.1. Aliniomba namba ya simu nikampa.
Alinifatilia mpaka mwaka jana na nilikutana nae mara kadhaa,2.tunapiga story na kupata drinks then ananirudisha home.
Sasa mwaka huu mwezi wa kwanza 3. kuna rafiki yangu alikuwa anaolewa ikabidi nije dar kwenye harusi. Laa haula bwana harusi ni mr.Y
iko wapi hiyo?
sikumpenda hata kwa asilimia moja ya kimapenzi.