Wanaume mnaocheza vikoba mnatia aibu

Wanaume mnaocheza vikoba mnatia aibu

Wanawake wanadharau wanaume wasiokuwa na pesa.

Miaka ya 90's Jiji la Dar ndio lilianza kupokea vijana wa kimakonde kutoka mikoa ya kisini na ndio wakaasisi jina la Wamachinga.

Nakumbuka Wamachinga wa mwanzo kwa sisi Watoto wa Dar tuliwaona kama mafala Fulani kwa biashara walizofanya kumbe walipiga sana pesa na Watoto wazuri mtaani wakawa wanawapenda wao kwa sababu wana pesa sisi tuna sound za uzawa tu kumbe ujinga mtupu.

Inawezekana wengi hawana elimu ya village community bank au hata hao washiriki huenda baadhi yao hawana uelewa wa namna ya uendeshaji wa Vicoba, kuna vicoba aina mbili Vicoba Endelevu na Vicoba vya kuvunja.
Wengi hawajui,wanafikiria vicoba ni ile michezo ya kinamama yakupeana ela kireja reja nakuzulumiana.Hawajui kama vicoba ni bank kama bank zingine local community.Tatizo ni elimu na uelewa duni kuhusu hili swala.
 
Ila wanaume mna limits za kingese

Shida ya vicoba ni ipi
Hao sio wanaume.mwanaume halisi alitakiwa awe anajua vicoba ni kitu gani.Lakini pia uku afrika wanaume wengi wanafikiri kua mgumu ndio kua mwanaume halisi.wakati huo ata kuisimamia tu jamii yetu kama wanaume hili jukumu limetushinda.Tunaangaika na ugumu na misimamo isiyo na manufaa.
 
Sawa Bilionea Sinoni.
Sio bilionea au dhihaka ndugu, mbona ni ukweli. Pesa utakayokopa hata iwe mara 3 ya uliyoiwekeza bado still utairudisha. Yaani sijaona kipya ila ni kwamba umejisaidia kupata pesa kubwa kwaharaka ambayo still utairudisha hiyo iliyozidi kwakuwa still bado ni akiba yako ileile. Hapo ndipo tunapoongea nakusema ni uwezo wa nidhamu ya pesa. Naweza kuweka 1M per month, pesa inakuwa polepole kufanya vitu kwa haraka haraka vinacost maana siitaji mikopo maishani mwangu, yaani hata iweje. Pia inadhihirisha udhaifu kwenye kujisimamia maishani mwako, yaani unahitaji kitu kikuforce ili uweze kusave money. Discipline ya pesa na maisha ni muhimu sana maishani.
 
Kwa akili kama hii yako bado nchi ina safari ndefu sana kiuchumi. Hatuchukui hela ili tukae nazo na kuzirudisha. Tunachukua hela tufanyie biashara na sio vinginevyo. Nikichukua 1M nikazungusha na kupata 1.5m kisha nikarejesha 1.2m huoni nitabakiwa na 0.3m? Au wewe ni wale mnachukua mkopo kwenda kujengea nyumba ya kuishi? Na wengine wanachukue kulipa mchango wa harusi. Kama ni rahisi kupiga hatua kwa kutumia hela zako mwenyewe watu wengi mnaosema hamtaki mikopo mngeshapiga hatua nyingi kimaisha. Ila cha kushangaza wengi waliofanikiwa wanachukua mikopo. Pia ishu ya kutunza pesa ni complex sana kuielezea... kutunza tu pesa huku huna vyanzo vya mapato ni upumbavu wa hali ya juu na ni suala linalohitaji kukemewa kupitia katiba mpya.
 
Ila wanaume mna limits za kingese

Shida ya vicoba ni ipi
Kanuni ya msingi kwetu sisi Wanaume, ni kule kujifananisha na Wanawake. Huenda Vicoba vikawa havina tatizo lolote kwa lengo lake, ila jambo linalo onekana katika jamii limeshikiliwa sana na Wanawake, mwisho wa siku huonekana lao. Ndio maana mwanaume ukijiingiza katika jambo hilo inaonekana umefanya jambo la kike.

Kinachokataliwa kwa mwanaume ni kutojifananisha na mwanamke kwa hali yoyote.

Mfano Mimi binafsi, huwa situmii maneno ambayo mara nyingi hutumiwa na Wanawake.

Kingine madhara yake ni makubwa, ukikaa sana na watoto wa kike, unaanza kuiga tabia zao, mwisho wa siku unaona kawaida hata kuzitumia.
 
Nawaza Hapa,

1. Hivi mwanaume unapata wapi ujasili kucheza kikoba Kama wanawake? Lengo lako Ni Nini hasa? Unajiskiaje kwa mfano.

2. Tena wengine utashangaa kabisa, anakuaga hadharani mwanaume mwenzie kua Anaenda kwenye kikoba! Unabaki unamwangalia Mara mbili mbili humpatii picha.

3. Hivi wanaume wanaocheza vikoba, nao upitia Changamoto kama hizi wanazopitia dada zetu na mama zetu ktk kusaka pesa za marejesho ya vikoba kila baada ya siku kadhaa za wiki au mwezi?

Bro maisha ni Bahar. Kila cku unajifunza Chief. Kama mtu kwa kucheza kikoba anafanikisha malengo yake mwache apambane Mzee. Kikubwa mtu asikae ikiwezekana tambaa kama ndio style inayokuwezesha kusogea. Mi nitamuona mtu ni mjinga pale anapodharau jitihada za wenzie kutoka. Fanya chochote aisee watoto waende shule.
 
Bado maana peke yake haitoshelezi kumfaa mwanaume acheze kikoba.

Kwanini mwanaume ucheze Kikoba?

Unashurutika hadi kulipa faini ukichelewa, hela ya faini ambayo hata haiwekwi kwenye akaunti yako nawe unaona fresh?
Izo faini siku ya kuvunja tunagawana
 
12M X 5 years = 60 M

ila ni kweli 60M ni kuelekea 100M
Hongereni sana ila pitieni katiba yenu vyema ya Ushirika wenu maana kadri fedha zinavyoongezeka Shetani wa Tamaa na migogoro anaanza vikao kazi

njia pekee ya kumdhibiti ni kuimarisha STK ( 'Sheria, taratibu na kanuni) za umoja wenu
Asante sana mkuu, kwa ushauri wako mzuri. Tunaendelea kuzifanyia kazi changamoto kama hizo. Lakini pia hiyo pesa tangu mwanzo tulikuwa tunakopeshana kwa riba na masharti nafuu kwa hiyo tunaikaribia M100 kama nilivyoandika
 
Kwa akili kama hii yako bado nchi ina safari ndefu sana kiuchumi. Hatuchukui hela ili tukae nazo na kuzirudisha. Tunachukua hela tufanyie biashara na sio vinginevyo. Nikichukua 1M nikazungusha na kupata 1.5m kisha nikarejesha 1.2m huoni nitabakiwa na 0.3m? Au wewe ni wale mnachukua mkopo kwenda kujengea nyumba ya kuishi? Na wengine wanachukue kulipa mchango wa harusi. Kama ni rahisi kupiga hatua kwa kutumia hela zako mwenyewe watu wengi mnaosema hamtaki mikopo mngeshapiga hatua nyingi kimaisha. Ila cha kushangaza wengi waliofanikiwa wanachukua mikopo. Pia ishu ya kutunza pesa ni complex sana kuielezea... kutunza tu pesa huku huna vyanzo vya mapato ni upumbavu wa hali ya juu na ni suala linalohitaji kukemewa kupitia katiba mpya.
We imekushinda nini kutumia hiyohiyo pesa uliyonayo kuanzisha biashara au kuizungusha. Kwamba ukiingia tu kwenye vikoba ndio wanakupa mkopo, siunasubiri kwamuda. Kinachokushinda kusave basing on your own salary mpaka kufikia muda kama huo kisha ufungue biashara ni nini? Your jumping to high levels of business investment huku ukiwa your main flow ni mkopo wa kikoba😂😂😂. Wajinga wengi, ndio maana tunaandikishwa mikataba ya kijinga hivhivi kwasababu we don't take time to plan and invest bali tunataka turukie. Aisee kuna watanzania wajinga sana. Pia nimekaa naniliofanikiwa😂😂😂, nikikwambia wanayoongea juu ya mikopo hutaamini. Mkopo unakupa a false mirage that your wealth but actually thats not your money. Jijenge kwa utulivu, unapaparika unakufa, halafu tunanguvu ya kuwasema dada zetu wakijiuza nawao wakitaka mafanikio ya haraka. Confused citizens😂😂
 
Nawaza Hapa,

1. Hivi mwanaume unapata wapi ujasili kucheza kikoba Kama wanawake? Lengo lako Ni Nini hasa? Unajiskiaje kwa mfano.

2. Tena wengine utashangaa kabisa, anakuaga hadharani mwanaume mwenzie kua Anaenda kwenye kikoba! Unabaki unamwangalia Mara mbili mbili humpatii picha.

3. Hivi wanaume wanaocheza vikoba, nao upitia Changamoto kama hizi wanazopitia dada zetu na mama zetu ktk kusaka pesa za marejesho ya vikoba kila baada ya siku kadhaa za wiki au mwezi?

Hujielewi ww!!
Una kasumba ya neno vikoba

Ni mfano tu wa Mfuko wa ukoo, vijana,wafanyakaz nk
unaonekana kama bado unakaa kwenu au hujawai fanya kazi una akili za kitoto!
 
Back
Top Bottom