Wanaume mnaowasemea wanawake huko tik-tok muwe mna-balance story

Wanaume mnaowasemea wanawake huko tik-tok muwe mna-balance story

Matteo Vargas

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2019
Posts
803
Reaction score
1,329
Kumekuwa na wimbi la video za tik tok ambazo asilimia kubwa wasimuliaji wake ni wanaume, video hizi ukizisikiliza muaudhui yake zimekuwa zikiwananga mno wanaume km watu ambao hawana huruma na kazi yao ni kucheza na hisia za wanawake na kuwaumiza.

Na wanaume wenzetu hawa wameenda mbali hadi kutulaani sisi wanaume (kana kwamba wao sio wanaume) kwa kuwatesa wanawake kihisia bila huruma (inaweza kuwa ni kweli lakini jaman sio wanaume wote). 😏

Lakini takwimu zinaonesha wanaume ndio wanaongoza kwa kuwa na msongo wa mawazo na hata kujiua/kuua linapokuja swala la mahusiano. Sasa sijui wanaume wenzetu hawa wanatumia vigezo gani kutupa hizo hukumu za kuwaumiza wanawake kihisia.

Umoja wa Mataifa, UN unasema, mauaji baina ya wapenzi yanaongezeka hasa kutokana na wivu wa kimapenzi. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha wanawake ndio waathirika zaidi wa mauaji hayo, ambapo 82% ya waliouawa mwaka 2017 walikuwa wanawake na 12% tu walikuwa wanaume (BBC).

'Swali kwanini wanaoumizwa kwenye mapenzi ndio hao hao wanauouawa zaidi kwa issue ya wivu wa mapenzi?'🤔

Nafikiri wanaume ndio waathirika wa hili ila shida ya wanaume ni watu ambao hawasemi na kampeni hii mnayoifanya inatengeneza picha mbaya kwenye kizazi hiki kinachokua kwamba wanaume ni viumbe hatari kwenye mahusiano.

Wakichepuka wanaume 20 msihukumu wanaume 200,000 kwani wanawake hawachepuki? au wao hawaonekani? mjaribu kubalance story tuliyonayo wanaume yanatutosha na tumechoka.😔😔
 
.
IMG_20220601_081944.jpg
 
Kwakweli muandamane tu mdai haki sawa, wasiwaonee.
 
Mama Mkwe akiona hiyo comment ataninyima kale katoto [emoji23]

Legeza sharti tafadhali
Kuwa na amani jopo la utetezi tupo. Tutamwambia mama mkwe hukuwa una maanisha😁😁😁
 
Kuwa na amani jopo la utetezi tupo. Tutamwambia mama mkwe hukuwa una maanisha[emoji16][emoji16][emoji16]
Kwa kuwa umekataa kunielewa, bora niungane na wana Tik Tok tu - nifungue akaunti halafu nikuchane uache kuchepuka ili uandike uzi mwingine [emoji2960]
 
Kwa kuwa umekataa kunielewa, bora niungane na wana Tik Tok tu - nifungue akaunti halafu nikuchane uache kuchepuka ili uandike uzi mwingine [emoji2960]
😀😀😀 Mimi si miongoni mwao wachepukaji. Mimi ni mtetezi wao waonewao ambao hawachepuki.

Ila zile video sio poa tunaonekana tunatesa wanawake wakati wengine tumeumbwa kuwapa furaha wanawake 😘
 
[emoji3][emoji3][emoji3] Mimi si miongoni mwao wachepukaji. Mimi ni mtetezi wao waonewao ambao hawachepuki.

Ila zile video sio poa tunaonekana tunatesa wanawake wakati wengine tumeumbwa kuwapa furaha wanawake [emoji8]
Unajitetea e?

Kwa hiyo statement yako ya pili lazima upate mchumba humu [emoji23]
 
Unajitetea e?

Kwa hiyo statement yako ya pili lazima upate mchumba humu [emoji23]
Huo ndio ukweli wengine tupo hivyo tu tukisikia tunasemwa tofauti lazima tu-react kuweka uhalisia 💯👫
 
Back
Top Bottom