Wanaume mnaowasemea wanawake huko tik-tok muwe mna-balance story

Wanaume mnaowasemea wanawake huko tik-tok muwe mna-balance story

Kawaida ya wanaume huwa hatuongei popote, ukiona hayo majitu yanayotetea wanawake ndo hayohayo yatakuja kutetea na mashoga.

Kwanza mwanamke hahitaji kutetewa coz jamii inamuamini zaidi mwanamke kuliko mwanaume, yeye tu kua mwanamke ni utetezi tosha kabisa.
Sasa hao wanaume wanaojitia kimbelembele siku yakiwakuta, watalia na kusaga meno.
 
Kumekuwa na wimbi la video za tik tok ambazo asilimia kubwa wasimuliaji wake ni wanaume, video hizi ukizisikiliza muaudhui yake zimekuwa zikiwananga mno wanaume km watu ambao hawana huruma na kazi yao ni kucheza na hisia za wanawake na kuwaumiza.

Na wanaume wenzetu hawa wameenda mbali hadi kutulaani sisi wanaume (kana kwamba wao sio wanaume) kwa kuwatesa wanawake kihisia bila huruma (inaweza kuwa ni kweli lakini jaman sio wanaume wote). [emoji57]

Lakini takwimu zinaonesha wanaume ndio wanaongoza kwa kuwa na msongo wa mawazo na hata kujiua/kuua linapokuja swala la mahusiano. Sasa sijui wanaume wenzetu hawa wanatumia vigezo gani kutupa hizo hukumu za kuwaumiza wanawake kihisia.

Umoja wa Mataifa, UN unasema, mauaji baina ya wapenzi yanaongezeka hasa kutokana na wivu wa kimapenzi. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha wanawake ndio waathirika zaidi wa mauaji hayo, ambapo 82% ya waliouawa mwaka 2017 walikuwa wanawake na 12% tu walikuwa wanaume (BBC).

'Swali kwanini wanaoumizwa kwenye mapenzi ndio hao hao wanauouawa zaidi kwa issue ya wivu wa mapenzi?'[emoji848]

Nafikiri wanaume ndio waathirika wa hili ila shida ya wanaume ni watu ambao hawasemi na kampeni hii mnayoifanya inatengeneza picha mbaya kwenye kizazi hiki kinachokua kwamba wanaume ni viumbe hatari kwenye mahusiano.

Wakichepuka wanaume 20 msihukumu wanaume 200,000 kwani wanawake hawachepuki? au wao hawaonekani? mjaribu kubalance story tuliyonayo wanaume yanatutosha na tumechoka.[emoji17][emoji17]
Huko tiktok hakuna wanaume, kuna mashoger.
 
Kawaida ya wanaume huwa hatuongei popote, ukiona hayo majitu yanayotetea wanawake ndo hayohayo yatakuja kutetea na mashoga.

Kwanza mwanamke hahitaji kutetewa coz jamii inamuamini zaidi mwanamke kuliko mwanaume, yeye tu kua mwanamke ni utetezi tosha kabisa.
Sasa hao wanaume wanaojitia kimbelembele siku yakiwakuta, watalia na kusaga meno.
Wanawake wanatetewa kila kona. Ila wanaomia zaid ndio hawatetewi
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Wa kahama yeye kaua halafu katawanya viungo vyote then kila kiungo kakizika separate huko majarubani....mbususu tu ndio imepata bahati ya kuzikwa nyumbani
Kanda ya ziwa wanawake watakimbia wote kwa hali hii
 
Back
Top Bottom