Dogoli kinyamkela
JF-Expert Member
- Nov 21, 2024
- 618
- 1,440
Ikifika hatua mwanamke wako akasema havutiwi tena nawe, hiyo ndio kengele kamili inayokujulisha kuwa penzi limeisha na hakuna chochote unaweza kufanya kurekebisha uhusiano huo usife.
Utakua kiumbe mpumbavu na wa ajabu kuwahi kutokea duniani ikiwa utaanza kumpigia magoti kwa kumwomba asikuache wala hupaswi kumuuliza anakwenda kwa nani.
Na wala hupaswi kuuliza kwanini anakufanyia hivi. Ruhusu hilo zoezi lifanyike haraka mara moja, maana hukuachwa leo; alishakuacha kitambo. Alikua anafanya intelijensia zake taratibu, sasa ameshajiridhisha na ana kiburi.
Hupaswi kuchukia. Wala hupaswi kulia. Ruhusu upanuzi wa barabara ukafanyike.
Ni upumbavu wa hali ya juu sana kumwomba abakie maishani mwako. Kiumbe ambaye alishakuacha miezi 6 nyuma, kwa kuwa wewe ulikuwa usingizini, akikulisha maneno ya "I love you too" pale ambapo ulimweleza hisia za "I love you."
Acha hiyo biashara haina faida, itakuumiza na kukugharimu ukiishikilia.
Ni heri kutafuna mawe kuliko kujaribu kurekebisha mahusiano yaliyovunjwa na mwanamke mwenyewe.
Kama amemaliza biashara na wewe, kamaliza. Funguka, funga ukurasa, ondoka mahali hapo.
Haijalishi umewekeza kiasi gani. Hesabu hiyo ni kama hasara. Amka hapo ondoka zako, kung’uta matako, anza zako.
Hata kama ulisomesha, hiyo ilikuwa ni kazi ya baba yake, lakini kichwa cha mwendawazimu kiliamua kuingilia mradi. Hivyo ni haki yake baada ya kuhitimu masomo kuolewa na msomi mwenzake. Kung’uta matako, anza zako.
Hata kama ulimjengea kwao.
Hata kama uliwawezesha wadogo zake.
Hayo hayakuwa katika mapatano, uliingilia mradi.
Kung’uta makalio, anza zako hata kama inauma.
Najua inauma sana hiyo. Sasa itumie hiyo iwe nguvu ya kukufanya mwanaume shupavu tena.
Itumie kama gia ya kukusukuma toka bondeni. Tumia kama njia ya kuamka mtu mpya ambaye hautarudia upumbavu tena.
Maumivu na hisia za kuchoma ndizo humjenga mwanaume. Acha hili likujenge.
Man up.