Wanaume na kujihami...!

Wanaume na kujihami...!

ni kweli kabisa
Na mie hapa huwa sielewi
akishalipuka nyumbani
ndo anaweza sema ana matatizo kazini
lakini hawezi fika tu na kukwambia

men bana!

kusema kuwa nina tatizo hapo ni ngumu
na kuanza kusema kuwa tatizo ninalo ni ngumu
 
akiwa na hasira

angusha hata kijiko
maneno yatakayomtoka utashangaa
ataingizwa hadi mama ako humo

unabaki na swali
hivi ugomvi huu ni hiki kijiko tu?

Ole wako ujaribu
kuclarify situation
utaimba haleluya
ni bora ukajisemea 'pole'

baadae muulize
ni nini kinakusumbua?
Utasikia 'aah, unajua ile dili yangu nimedhulumiwa'
so nina mood sana.
Kama anapiga ulabu hakikisha nyumbani kuna chupa kadhaa za red label.
Ukiona kakasirika unammiminia four fingers kwa glass
Mwenyewe utaona anatabasamu.

Kumbe hamtujulii wanaume wanywaji eh?
 
Hiyo ni mbinu nzuri sana, na kwa wanawake huwasaidia kuondoa stress, lakini kumbuka kwamba wanaume mara nyingi ni wasiri sana, na wao kuzungumzia mambo ya kunyanyaswa kazini, ni sawa na kukiri udhaifu mbele ya wake zao, na ndio maana huumia ndani kwa ndani na mwisho wa siku hulipukwa na hasira hata kwa jambo dogo kiasi gani na wanaoathiriwa na hali hiyo ni wake zao au watoto kwa ujumla.
uzuri mume wangu ni rafiki yangu, haoni shida kunisimulia mambo yanayomwangusha na mara nyingi huniomba ushauri kwa vitu vingi sana, siwezi kusema vyote, labda vingine haniambii, mara nyingi akiwa na kitu kinamsumbua lazima ataniambia, anaweza kusema this is embarrassing lakini naomba nikuambie. nadhani na mimi nampa confidence ya kunisimulia sababu nitajitahidi kwa lolote atakaloniambia asijisikie vibaya baada ya kufanya hivyo na namwambia hilo mbona la kawaida......
 
Ndo maana binti yangu ataenda kwenye mikono salama. Mie pia nimeoana na rafiki yangu asee. Vinginevyo kandoa kangu kangeshavunjika siku nyiiiiingi!
 
niliwahi jaribu kuishi namna hiyo ikifikiri kuwa ndio itasaidia mwenzangu ajue niko kwenye wakati mgumu lakini ndio ilikuwa mwanzo wa matatizo nimejifunza kunyamaza kimya hata nikiwa napita kwenye magumu kiasi gani.
wakati mwingine wanawake hawataki kujua kuwa mwanaume ana matatizo maana wanatuonaga kuwa sisi ni kma vyuma yaani hatupaswi kulia lia, kila siku wewe unamlilia mwenzako anakuona **** pengine kuna wengine wangependa wasikie labda kuna mtu alikuudhi na ukampiga kibao atasema yes huyo ndio mwanaume.
Pia wanawake wanashindwa kujua ni wakatio gani wa kuelezea jambo fulani kwamfano mtu anakuja hajajua uko kwenye mudi gani anaanza kuropoka kuwa katongozwa leo kazini na bosi wake ebu niambie halafu yeye kila siku ndio wa kutongozwa? inamaana ni mzuri sana au ndio ananitishia kuwa nisipokaa vizuri atawakubalia. unaweza ishia kulambwa kibao
huyo alikuwa mkeo au GF? kule kwa GF huwa hamtakiwi kueleza weakness zenu, ila kwa mke? sasa atakusaidiaje kama humwambii nini kinakusibu?
 
Hongera kwa kuolewa.
Sasa mme anakuwaje awe rafiki yako wakati mmeunganishwa na kuwa kitu kimoja?
hivi mnakuwa kitu kimoja?
sisi bado kila mtu ana feelings zake, maamuzi yake,........ ndo maana tunaendelea kuwa marafiki.
Asante
 
Ndo maana binti yangu ataenda kwenye mikono salama. Mie pia nimeoana na rafiki yangu asee. Vinginevyo kandoa kangu kangeshavunjika siku nyiiiiingi!

ha haaaaaaaaaa, rafiki, yaani binti atakuwa salama kabisa, au ahamie kabisa kwetu ili tuanze kukalea tangu saa hizi? ni strategy nzuri
 
hivi mnakuwa kitu kimoja?
sisi bado kila mtu ana feelings zake, maamuzi yake,........ ndo maana tunaendelea kuwa marafiki.
Asante

Basi huyo mme ni B/F na sio mmeo utakubaliana na mimi kwa hilo?
 
Ndo maana binti yangu ataenda kwenye mikono salama. Mie pia nimeoana na rafiki yangu asee. Vinginevyo kandoa kangu kangeshavunjika siku nyiiiiingi!

Mpwa mama nanihii ni rafiki yako?
 
ha haaaaaaaaaa, rafiki, yaani binti atakuwa salama kabisa, au ahamie kabisa kwetu ili tuanze kukalea tangu saa hizi? ni strategy nzuri
Nahofia huyo rafiki yako hachelewi kumbadilishia mwanao kibao. Binti mwenyewe ushamuona lakini? Ni vile tu hairuhusiwi, ningemuoa mwenyewe.
 
Nahofia huyo rafiki yako hachelewi kumbadilishia mwanao kibao. Binti mwenyewe ushamuona lakini? Ni vile tu hairuhusiwi, ningemuoa mwenyewe.
rafiki, mtake radhi rafiki yangu.................
 
Back
Top Bottom