Wanaume nasi tuna mizengwe!

Wanaume nasi tuna mizengwe!

UmkhontoweSizwe

Platinum Member
Joined
Dec 19, 2008
Posts
9,454
Reaction score
8,894
Wanajamvi,
Kuna mdada hapa anahitaji masaada wa kimawazo ili imsaidie kuwaelewa wanaume.
Anasema kuna siku kaka mmoja ambaye wamezoeana, wanaongea, sms, email nk, kiasi kwamba wamekuwa marafiki wazuri tu.

Siku moja huyo kaka akamwomba watoke ona date. Dada bila tatizo akakubali na siku ilipofika wakaenda.Walikuwa pamoja huko kama masaa matatu na ushee hivi, na outing kwaujumla ilikuwa nzuri.

Lakini, kinachomsumbua huyu dada nikwamba, ktk masaa hayo matatu ya outing, muda walioutumia pamoja kwamaongezi ni kama masaa mawili hivi, au pungufu ya hapo! Muda mwingine uliobaki huyo kakaalikuwa kwenye hamsini zake, mara atoke akaongee na simu pembeni,mara yuko busy anatext, mara anablogi (sijui kama JF!) – yaanialitumia muda mwingi kwa mambo ambayo hayakuhusiana kabisa na “date”yenyewe. Hilo lilimpa shida huyo sister kujua kama hiyo ndo tabia wa wanaume au ni tabia ya huyo mkaka tu.

My take:
Gentlemen, nadhani tunapaswakuwa sensitive tunapokuwa kwenye mambo kama haya na tuonyeshe kujali.Kama kweli umempa mtu date halafu unatumia karibu nusu ya mudamtakaokuwa pamoja kwa mambo mengine, ambayo yawezekana siyo ya muhimukiasi hicho, nadhani inaonyesha kutokujali. Tuthamini na kujalimahusiano yetu na muda wa hao watu.

Wanajamvi, najua penye wengihapaharibiki neno. Nyie mnalionaje hili?
 
Mkuu the way inavyoonekana uhusiano wao haukufikia kuwa ni mtu na girl friend wake. May be jamaa alijua ni date ya kawaida ya marafiki na hakuna sensitive issue ya kuongea ndo maana alikuwa busy na mambo yake
Date ya wapenzi mkuu inakuwa ni issue. Yaani huwa hata muda hautoshi
 
Kiujumla jamaa hana noma. Tatizo lipo kwa dada hakuweza kufunguka ili jamaa amsome fresh ili awe busy nae.
 
Mkuu the way inavyoonekana uhusiano wao haukufikia kuwa ni mtu na girl friend wake. May be jamaa alijua ni date ya kawaida ya marafiki na hakuna sensitive issue ya kuongea ndo maana alikuwa busy na mambo yake
Date ya wapenzi mkuu inakuwa ni issue. Yaani huwa hata muda hautoshi

Yeah, urafiki haujafikia kiwango cha GF/BF, ingawa kuna prospective ya development.
 
aiseee umenikumbusha zamani
nilitoka na mdada mmoja.....dah...
kutwa anapokea simu,yaani mazungumzo yakianza kunoga tu..simu imeingia..
ananyanyuka huyooo pembeni anaongea kama dakika kadhaa
akirudi,anakuja na mazungumzo ya simu....sijui mama dogo kafanya nini na nini...arghhh...

halafu tulikuwa Sinza ambapo wamachinga wako weengi wanapita pita kwenye mahoteli na ma bar kuuza bidhaa

yaani kero juu ya kero....
 
Duh, itabidi kama kuna mdau anaweza atupe notisi wengine tukajisomee jinsi ya kwenda date
 
aiseee umenikumbusha zamani
nilitoka na mdada mmoja.....dah...
kutwa anapokea simu,yaani mazungumzo yakianza kunoga tu..simu imeingia..
ananyanyuka huyooo pembeni anaongea kama dakika kadhaa
akirudi,anakuja na mazungumzo ya simu....sijui mama dogo kafanya nini na nini...arghhh...

halafu tulikuwa Sinza ambapo wamachinga wako weengi wanapita pita kwenye mahoteli na ma bar kuuza bidhaa

yaani kero juu ya kero....

Kweli mkuu, mazungumzo hata hayawezi kunoga, maana hayatakuwa connected. Mnazungumza kidogo, mara mtu anatoka kwenda kuongea kwenye simu dk 10, akirudi huko zinaanza stori za kwenye simu kwanza, mnasahau hata mlikoishia.
 
Aisee hiyo ni mbaya sana hata kama ingekuwa date yao ya 1000 mkaka hakupaswa kubehave hivyo.
Hiyo ni dharau na inaonesha uwepo wako hauna thamani.

Kweli, hata yeye huyo mkaka angetendewa hivyo sijui kama angejisikia vizuri.
 
Kweli mkuu, mazungumzo hata hayawezi kunoga, maana hayatakuwa connected. Mnazungumza kidogo, mara mtu anatoka kwenda kuongea kwenye simu dk 10, akirudi huko zinaanza stori za kwenye simu kwanza, mnasahau hata mlikoishia.

kuna mtu alichukua simu ya msichana na kuitumbukiza kwenye glass ya maji kwa hasira lol
 
kaaaaaaaaaazi kweli kweli.......!km mmechat,simu mmepigiana mara kwa mara,then date ni kupoteza muda tu! ongeeni yote mmalizane huko huko kwa njia zenu za mwanzo za mawasilianao! ikiwa ni date inakuwa kila mtu tayari anajua mustendi ulipo km ni kibla au lah!
 
Mkuu, mtaishia kwenye maongezi ya simu, text, na email tu bila kuwa na muda wa kukutana kukaa pamoja na kuongea? Mtafahamina namna gani tabia zenu bila kukaa na kuwa pamoja kwa muda fulani?
 
Lol! Si bora alikua busy na simu,kuna mwingine nusu ya muda anaongelea ex wake,robo anajiongelea mafanikio yake na hiyo robo iliyobaki nusu yake anaongelea chadema na nusu unakua unachomekea vicheko! Kazi!
 
Ha ha, hii ni nzuri zaidi

Lol! Si bora alikua busy na simu,kuna mwingine nusu ya muda anaongelea ex wake,robo anajiongelea mafanikio yake na hiyo robo iliyobaki nusu yake anaongelea chadema na nusu unakua unachomekea vicheko! Kazi!
 
kwa kweli inakera sana maaana inatakiwa mtu uelewe kwa nini uko pale na uko na nani na nini nafasi yake .... na kama ulikuwa una mamabo mengine zaidi ya hayo fanya ustaarabu mapema kuwaambia hao unaochat nao utakuwa busy kwa muda fulani ili maana ya kutoka na mwenzako iwe na maana
 
Back
Top Bottom