Wanaume ni wa ovyo sana

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
3,448
Reaction score
7,972
Mwanamke anakuheshimu, anakuwa na msimamo pamoja na vishawishi anavyokutana navyo ila sasa mume aliyenaye ni pasua kichwa.

Jana usiku mwanaume kaondoka kapata dharula kasahau simu ya smart, kwa bahati mbaya kasahau kulock si kawaida yake, maana kakurupushwa na kaondoka na simu ndogo kaacha smart.

Nilikuwa nimekua kiakili kwamba sitashika simu ya mwanaume hata iweje na sijui ni shetani gani kanishawishi nikaishika.

Nikaenda Messenger ya FB nikakutana na chat zaidi ya 200 ya wanawake, wengine akiwatongoza, wengine "Mambo mrembo wangu" pande zipi? Hizi ndio text kwa kila mwanamke kwa kila mwanzoni mwa chating.

Nikagundua friendlist kati ya 4552 alionao FB wanaume ni 20 tu, hivo hivo kwenye Instagram, amewafollow wanawake kuliko wanaume na inbox huko sms zile zile.

Na cha ajabu ni kwamba katika kufuatilia kila wakichati na hao wanawake anawaomba namba za Whatsapp au anawatumia namba, na nilichogundua kupitia mitandao ya kijamii anatembea na wanawake zaidi ya 15 wawili wapo wilaya ya jirani, wanawake zaidi ya 2000 wanaitana my.

Wanawake 57 wanalalamika kuwa alitembea nao mara moja au mbili na kuachana nao bila sababu.

Anatembea au alitembea na wanawake wawili kutoka nchi ya Botswana kulingana na chating zao.

Nikataka niende WhatsApp, mikono ikatetemeka nikaacha.

Loh! Unamuona mwanaume yupo bize mtandaoni, ukimuuliza mbona bize sana, anakujibu biashara, mara betting, kumbe michepuko!

Sina hamu.
 
Mwenye kosa ni wewe, kwanini umeingilia privacy ya mtu, ujue akijua na akaamua kukushtaki atakufunga.
Kuolewa na huyo jamaa haimaanishi una uhuru wa kuingilia privacy yake.
Ushauri wangu: Muombe msamaha huyo mshikaji, na Mungu wako kwa hilo kosa, na usirudie tena.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Duh, hadi leo una maumivu ya yule kijana muhuni aliyekutoa Mwanza kisha kukuachia 7,900/- Msamehe bure dada yangu.
Huyo hawezi kabisa kubadilika kwani mimi mwenyewe nilimshuhudia akiwaomba namba za simu wale wanawake masanamu wanaotumika kuonyesha nguo zinazouzwa.
 
Si ajabu na wewe alikupata kupitia social media! Dirisha lile lile uliloingilia nadilo hilo hilo wengine wanapitia!
 
Sawa
 
Najua baadhi ya wanaume watamtetea mwenzao, na iwe chai ama ukhalisia ila ukweli ni kwamba kuna wanaume ambao ni very cheap, some men are just for every woman, yaani standard ni kitu hawajawahi kuwa nacho kabisa..!!

you guys, can't you save your energy and time for sth better and worth for..??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…