Mwanamke anakuheshimu, anakuwa na msimamo pamoja na vishawishi anavyokutana navyo ila sasa mume aliyenaye ni pasua kichwa.
Jana usiku mwanaume kaondoka kapata dharula kasahau simu ya smart, kwa bahati mbaya kasahau kulock si kawaida yake, maana kakurupushwa na kaondoka na simu ndogo kaacha smart.
Nilikuwa nimekua kiakili kwamba sitashika simu ya mwanaume hata iweje na sijui ni shetani gani kanishawishi nikaishika.
Nikaenda Messenger ya FB nikakutana na chat zaidi ya 200 ya wanawake, wengine akiwatongoza, wengine "Mambo mrembo wangu" pande zipi? Hizi ndio text kwa kila mwanamke kwa kila mwanzoni mwa chating.
Nikagundua friendlist kati ya 4552 alionao FB wanaume ni 20 tu, hivo hivo kwenye Instagram, amewafollow wanawake kuliko wanaume na inbox huko sms zile zile.
Na cha ajabu ni kwamba katika kufuatilia kila wakichati na hao wanawake anawaomba namba za Whatsapp au anawatumia namba, na nilichogundua kupitia mitandao ya kijamii anatembea na wanawake zaidi ya 15 wawili wapo wilaya ya jirani, wanawake zaidi ya 2000 wanaitana my.
Wanawake 57 wanalalamika kuwa alitembea nao mara moja au mbili na kuachana nao bila sababu.
Anatembea au alitembea na wanawake wawili kutoka nchi ya Botswana kulingana na chating zao.
Nikataka niende WhatsApp, mikono ikatetemeka nikaacha.
Loh! Unamuona mwanaume yupo bize mtandaoni, ukimuuliza mbona bize sana, anakujibu biashara, mara betting, kumbe michepuko!
Sina hamu.