Wanaume Sikia hii

Wanaume Sikia hii

jozee jose

Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
52
Reaction score
120
Kuzaliwa mwanaume ni zawadi ya kipekee sana ambayo hukuichagua ila ulipewa kwa mapenzi ya Mungu.
Tutambue ya kwamba Mwanaume hakuumbwa MATESO bali mateso yalichaguliwa na Mwanaume mwenyewe.

Mwanaume ni mlezi mkuu wa familia nzima yeye ni kama Mwenyekiti na mkewe ni kama katibu, taasisi hii inajengwa na vijenzi vitatu( UPENDO, FURAHA NA UVUMILIVU)

Mwanaume ni kuhani wa Familia ambaye huunganisha Maombi/sala zake na za Familia kwa Muumba wake

Mwanaume ndiye mkuu wa Huduma zote nyumbani ikiwa mahitaji yote ya familia, Mkuu wa ulinzi na Usalama na la ziada ukumbuke ya kwamba unalea familia tatu yaani ya kwako, wazazi au walezi wako pamoja na Familia ya mkeo.

Kuna siku nilisika Mzee mmoja akijitapa kuwa na watoto kumi na TATU nkatamani kujua kama kwanza, Je hao watoto wote anaishi nao,

Pili. Je, hao watoto wote ni mama mmoja?

Majibu aliyatoa mwenyewe ya kwamba ni mama watano tofauti.
Nikiwa surprised nikatafakari kwa kina Namna ya malezi ya hao watoto yapoje?

Kitu kingine alisema kwamba anaishi na Mwanamke mmoja na watoto 2 tu, maana yake watoto 11 wapo mbali naye wakiwa na Mama zao
Binafsi nikajiuliza anawezaje kuprovide huduma za mahitaji yeye kama Baba kwa watoto hao pamoja na mamaze?

Cha kuchekesha ni mzee ambaye muda mwingi yupo kwenye draft na kunywa GAHAWA.
Kwa kisa kidogo hapo juu huo sio Uanaume ni UJINGA uliombatana na UPUMBAVU

• Mwanaume wa kweli hatakiwi kuwa mbinafsi wa kuwazalisha wanawake hovyo mitaani na kuwaachia wanawake walee peke yao.
• Mwanaume Bora ni lazima ajihusishe kwenye malezi ya watoto DIRECT and INDIRECT kuwalipia karo na madaftari ya Shule haitoshi
• Mwanaume Makini ni lazima awe karbu na wanawe kujua HISIA na MWENENDO wa watoto wao, kuna namna fulani mwanaume ameumbwa kwa na power ya Usimamizi hivyo itasaidia.
Nahitimisha kwa Kusema Matokeo ya kile tunachokipata Leo kimetokana na Uchaguzi wetu mbaya au mzuri,
Hivyo tuchague Familia ili tuwe na Kaya bora na Taifa makini
 
Haya,yakikuta urudi hapa na shuhuda!
 
Back
Top Bottom