Wanaume sio ATM!!!

Wanaume sio ATM!!!

Umenena vema Keren sijui Hapuch.....damn majina mengine magumu sana,

Ukioa mwanamke aliyekuzidi vifuatavyo hiyo ndoa ujue ni mshike mshike:
1. Elimu
2. Kipato
3. Umri
4. Ubabe

Ombi....Keren naomba uwe mmoja wa wajukuu zangu.

Natanguliza hii hapa kwanza, kwa msisitizo.


The Following User Says Thank You to Keren_Happuch For This Useful Post:

Asprin (Today)

Babu Aspirin... unajua siwezi kukataa kuwa mjukuu wako maana unajua yako maneno matamu uliyofundisshwa na babu yako...na kwenye hayo maneno matamu..haikosekani hekima kwa babu.... pata kahawa kwanza babu hapa.....:coffee:
 
Haya mamito nimekusoma...sio mi peke yangu mwenye kiu ya kujua hili hebu msome na huyu hapa chini...!!

Nimekusoma ila sitaki kulijibu hadharani nitakwambia ukipitia dukani kwangu jioni sawa???
 
Hii mtindo wa kuwaita wanaume ATM unawaboa sana kusema ukweli...hata mimi kama mdada siufagilii.Achili mbali huwaita hata kuwatumia kama ATM nayo inatufanya wadada tunadharauliwa wakati mwingine.

Kuna marafiki zangu wawili niliwatambulisha wiki chache zilizopita.Mkaka wa watu akawa amedata haswa....kila saa kumuulizia binti.Kiukweli kaka alikua anataka mahusiano yanayoeleweka na sio kuchezeana.Wakakutana mara mbili tatu mkaka akaendelea kudata.

Siku ya siku kaka akamwalika mdada chakula cha jioni ali wapate muda wa kuongea kidogo...mdada akaja na shoga yake.Yule kaka akaboreka ila akapotezea tu.Hata akijaribu kuongea na mambo ya maana mdada akili yote kwenye mambo ya starehe tu...nayo akapotezea.Alipokuja kuharibu ni kuanza kuulizia vocha...tena kwa kudemand....yani yule kaka alichoka.Kwasababu kumpigia hampigii...akitaka kuongea nae anaweka utoto mwingi ila wakati akitaka lift na vocha ndo haishi kubeep apigiwe.
Yule kaka alikuja kuniambia yule rafiki yako kwakweli nimemshindwa.Naweza kuelewa kwamba bado hajaweka maisha yake kwenye mstari ila atleast angekua anaonyesha nia badala ya kushinda akiomba pesa ningempa muda.

Newayz nnachojaribu kusema hapa ni kwamba wadada fanyeni kazi...na hata kama huna sio mtu hata bado hamjawa karibu sana tayari umeshaanza kua omba omba.Unajipotezea mwenyewe bahati....mwanaume mwenye nia anataka mwanamke mwenye nia na anae eleweka!!Acheni kuwatumia wakaka wa watu...mpende kama umempenda na sio kumendea vijisenti vyake alivyotolea jasho!!!

Nawakilisha!!!
Great piece of thought....Una haki ya kupata bia mbili leo(japo zimepanda bei)
 
Hahahhaa.Hili jina bomba sana,Haya na mie nisalimie...
ATM's Kaizer,kimey,Aspn ,TF..Hmjambo wote kwa ujumla??
We mamito ivi ile Account number ya Bank ya Uswiss mbona hujanitumia number?
Nimekumiss ujue?
 
We mamito ivi ile Account number ya Bank ya Uswiss mbona hujanitumia number?
Nimekumiss ujue?
Nasikia wameiblock ilikuwa inafanya transactions kutoka kwenye account ya Mubarak wa Misri l.o.l
 
Kimey siku hizi kuna ATM za kuweka na kutoa kama zile za CRDB sasa mimi ATM yangu inaweka tu haitoi....
 
Back
Top Bottom