Imalamawazo
JF-Expert Member
- Jul 27, 2021
- 1,343
- 3,269
Je ulishawahi kujiuliza familia inayoibiwa mtoto inaishi katika mateso ya namna gani? Usiombe yakukute! Ukiweza yaepuke kwa kuchukua tahadhari zote. Sisi tulinusurika kubadilishiwa mtoto akiwa labour. Nitajaribu kueleza kwa ufupi kwa lengo la kufikisha ujumbe. Hivyo nitapunguza utambulisho wa hospitali, na baadhi ya majina ya watu na mahali siyo majina yao halisi. Karibuni.
Kipindi hicho mimi na mke wangu tulikuwa tunaishi Tabata Dar es Salaam. Mke wangu mdogo mdogo, sura ya kitoto asipokwambia umri wake unaweza kudhani ni below 18. Baada ya muda kadhaa wa kuwajibika, mke wangu alikosa siku zake na kujisikia kichefuchefu. Chapu chapu nikachukua kipimo cha buku tukapima mkojo. Ngoma ikatiki. Tukapanga siku, nikaambatana naye tukaenda zahanati ya serikali mtaani.
Kadri siku zilivyoyoyoma, tulianza mikakati ya kumpokea kichajo. Jambo la kwanza lilikuwa ni kuchagua hospitali yenye huduma nzuri ya kujifungulia. Kulingana na vipato vyetu tulielekezwa hospitali moja isiyo ya serikali. Iko wilaya ya Ilala. Umbali wa kutokea hapo nyumbani hadi hapo hospitali ni parefu kidogo lakini tulijipanga kuweka mambo sawa mapema. Tukaamua kuanza kudhudhuria kiliniki pale ili tuyazoee mazingira.
Mke wangu alifanya vipimo vya ultrasound hapo hapo hospitalini. Mtaalamu wa wa ultrasound alipotukabidhi picha ili tuipeleka kwa daktari nikamuuliza, mbona picha haionyeshi popote jinsi ya mtoto? Akanijibu kuwa picha inaonesha lakini mimi ndo sijui kuitafsiri. Tukacheka. Akanifafanulia nikaelewa. Mtaalamu huyo alituambia kuwa mara nying hawaambia watu jinsi ya mtoto ili kuepusha kuvuruga malezi ya mimba na mtoto. Kwamba kuna baadhi ya familia zinaweza kuwa inauhitaji wa jinsi flani lakini picha ikaonyesha ni jinsi tofauti. Ikitokea hivyo familia inaweza kupoteza mzuka wa kumsubiria mtoto. Akatuambia picha inaonyesha tunatarajia kupata binti. Tukaachana naye tukaenda kwa daktari naye akatuambia hivyo hivyo. Picha inaonyesha tunamtarajia mtoto wa kike. Kwa hiyo tukafanya maandalizi ya kumpokea mtoto wa kike ikiwemo kuanza kusaka jina zuri la kike lenye usasa.
Siku za kujifungua zikatimia. Mke wangu akakimbizwa hospitali majira ya saa tano hivi. Mi nikapigiwa simu nikatoka kazini kuelekea hapo hospitali. Nimefika hospitali nikakuta tayari ameshapelekwa chumba cha kujifungulia. Hivyo tukakaa kwenye msingi ya vibara karibu kabisa na chumba cha kujifungulia.
Kilichoendelea chumba cha kujifungulia.
Wakati mke wangu anaingizwa kule labour, alimkuta mjamzito mwingine anapambana na uchungu. Umri wake kama miaka arobaini na eshee, huyu mmama nimuite Anita. Hatimaye Anita alijifungua salama, mtoto wa kiume. Lakini alivyoonyeshwa akakuta ni mtoto wa kiume alinung’unika. Akasema, yeye na mume wake tayari wana watoto wa kiume kadhaa (akitaja idadi) lakini hawajabahatika kupata binti. Na kwamba alitamani sana mara hii ajifungue binti. Anita aliendelea kusema kuwa mume wake anatamani kupata mtoto wa kike. Lakini yeye akijiangalia umri wake aliamini huenda huo ukawa uzao wake wa mwisho. Anita alihofia mumewe kwenda kuzaa nje ya ndoa ili walau apate mtoto wa kike. Wivu ndio ulikuwa unamtafuna Anita.
Mida ya saa nane hivi, mke wangu naye akajifungua. Yeye akajifungua mtoto wa kike. Anita alivyosikia mwenzake kajifungua mtoto wa kike, alisogea kumwangalia mtoto. Akaanza kumsifia mtoto eti mzuri na blaabalaah kibao. Tukiwa hapo nje, mkunga mmoja aliniita na kuniambia nimpatie chupa ya chai. Akaniambia, hongera mkeo amejifungua mtoto wa kike. Nikamjibu, Tumshukuru Mungu. Nikampa chupa ya chai akarudi tena labour. Baada ya muda mfupi, yule mkunga alitoka tena. Akatuaga kuwa anaondoka. Pia akatuambia kuwa mzazi atasalia humo labour kwa muda maana vyumba vya kupumzikia vinafanyiwa usafi bado.
Basi mle labour wakabaki mkunga Jack, Anita na mke wangu pamoja na vichanga vyao. Anita akahisi mke wangu amelala usingizi. Ndipo alipoanza kumshawishi Jack afanye mpango ambadilishie mtoto. Akamuahidi kumpa kiasi cha pesa milioni moja cash. Mke wangu alivyosikia hayo maongezi ya Anita na Jack, aliaamka ili Anita na Jack wasiendelee mipango yao miovu. Akamuomba Jack amuchukulie tena chai.
Anita bila kujali aliaamua kufunguka. Akamuuliza mke wangu, ‘eti mdogo wangu mumeo yuko wapi?’Kabla hata hajajibiwa, akaendelea, mumeo anajua utajifungua mtoto wa kike? Akajibu ndiyo, tulipiga ultra sound. Jack (mkunga) akadakia, lakini ultra sound huwa wakati mwingine zinadanganya. Inaweza ikasema mtoto wa kike akitokea wa kiume. Anita akajibu, mdo wangu naomba tubadilishane, nikupe wa huyu mtoto wa kiume mimi nichukue wa kike. Nitakupa pesa ya kumtunza sasa na kila mwezi ntakuwa nakulipa. Akamsema kazi yake na kazi ya mume wake, akataja hadi mtaa wanakoishi pamoja na namba ya nyumba. Akasema huyo Jack atampa milioni moja atutunzie siri. Mke wangu akamjibu kwa hasira, we dada, unafikiri mimi hizo pesa sina? Kama nisingekuwa na pesa hapa hospitali nimefikaje? Jack akajibu, kama una nia ya kumsaidia mwenzako unasema, kama hutaki pia unasema, lakini haya maisha ni kusaidiana.
Majira ya saa kumi na moja hivi Jack akatoka chumba cha kujifungulia akiwa amebeba mtoto. Lakini kwa kuziangalia zile kanga nikajua kuwa siyo mtoto wetu. Baada ya muda akatoka Anita na ndoa na chupa ya chai mkononi. Hakukuwa na ndugu yeyote aliyekuwa anamsubiria Anita. Hata mume wake hakuwepo. Lakini kwa umri wake alionekana shuruba za uzazi hazikumtesa sana. Jack akampeleka Anita chumba cha mapumziko. Kumbe walienda kusuka vizuri mipango ya kuiba mwanetu.
Jack alivyorudi kule labour akamuambie mke wangu alale apumzike, chumba chake bado hakijawa tayari. Mke wangu akamwambia hata sina usingizi. Jack akamwambia kama huna usingizi twende nikakuonyeshe chumba chako. Halafu nitarudi nikuletee mtoto, na ndoo hii ya nguo chafu. Mke wangu akagoma akasema tukitoka tutaongozana, wewe utabeba mtoto mimi nitabeba ndoo.
Baada ya majadiliano hayo kugoma mke wangu alimuomba Jack amchukulie pochi yake. Jack akatoka mlangoni akaita, ndugu wa flani (mke wangu) leteni pochi yake. Nikampelekea naye akaipeleka ndani. Mke wangu kachukua simu kaanza kunichatisha.
Baada ya muda mfupi rafiki zangu wawili wakafika. Wote ni maaskari, hivyo walikuwa na magwanda yao. Tukawa tunapigia stori hapo nje. Kumbe Jack alipita akaniona niko na maaskari. Jamaa yangu akaniambia huyo nesi (Jack) mbona ameshtuka kutuona. Tukamjibu kwa utani labda ameogopa magwanda ya askari. Kumbe uwepo wangu na maaskari pale ulivuruga mipango ya Jack na Anita.
Jack akarudi labour akamwambia mke wangu amka nikupeleke wodini. Jack alitoka labour amebeba mtoto, na mke wangu anamfuata kwa nyuma huku akiwa amebeba ndoo ya nguo chafu. Nilipo muona nikampokea mke wangu hiyo ndoo tukafuatana na Jack kwenda kwenye chumba cha mapumziko alichoandaliwa. Yeye mbele sisi nyuma kidogo lakini tuliweza kuona aliko Jack na mtoto.
Vyumba vilitengwa kwa kuta za vioo na aluminium. Hivyo Jack alivyokuwa anasogea, Anita alitoka kuonana naye. Lakini Jack alimjibu kwa ukali, ‘nisubiri nakuja’. Jibu lile lilimfedhehesha Anita. Lakin alipogeuka akaona magandwa ya polisi. Naye naye pia ni kama alishtuka. Tukampita hatukumjali sana. Tukaongozana hadi kwenye alichopelekwa wanatu.
Nikamwambia Jack anipe tangazo la mtoto kuzaliwa. Akasema ofisi zimeshafungwa, nisubiri kesho. Lakini akaniambia ataniandika notisi kutoka labour ambacho nitawapa wahusika waniandikie tangazo. Akaniambia nimtajie jina la mtoto.
Basi nikampa wife mazaga zaga na marafiki zangu wakatoa misimbazi kadhaa wakamkabidhi. Baada ya stori za hapa na pale tukaondoka, huku tukimuacha mama na mtoto wapumzike. Kesho yake nikapita hospitali nikawajulia hali. Pia nikachukua tangazo nikaenda kujaza likizo ya siku tatu kazini. Mida ya saa nne hivi, tukaruhusiwa kuondoka.
Tulivyofika nyumbani mke wangu akanisimulia mkasa wa labour. Nilipandwa na hasira. Nilitamani nirudi hospitali nikamchanechane Jack. Lakini bahati mbaya sikuwa na ushahidi. Mke wangu akanituliza, nikatulia, maisha yakaendelea.

Upvote
2