Wanaume tukome kuwekeza kwa mahawara!

Wanaume tukome kuwekeza kwa mahawara!

Hapana, nilikuwa najaribu kuonesha umuhimu wa kinamama kujiandaa na situation kama hizi, sio unafuma meseji ya hawara hata pa kutokea huna, una makucha marefu mikononi tu na malipustiki ya India.

Kama malipustiki ya Ufaransa jee?
 
Lakini kumbuka kuna theory inayosema usiweke mayai yako yote kwenye kapu moja. Nakumbuka niliambiwa na mwalimu wangu wa portfolio Analysis

fafanua mkuu,hapa nani kajaza mayai,mke,mme au hawara?
 
mi

Rocky my friend ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni, haya mambo yanatokea duniani chini ya mbingu hii hii tunayoishi. Hata mimi nimekuwa shocked na ujasiriamali huu wa kuwekeza kwa hawara. Kusoma nisome mimi, kazi nifanye mimi halafu hela zangu aje kuzila lijananke ambalo hata si mama, dada , binti wala mke wangu? This is ridiculous na ma kweli wanaume tunatofautiana!!!!!!!!.


Mkuu kweli ya Musa ni madogo sana
Na bei anatuma kabis ana unaambiwa utoe haraka kabla bei haijapanda na mwanaumu alivyo zumbukuku atakimbilia benki kudraw that amount kwa ajili ya hawara
 
Kama malipustiki ya Ufaransa jee?
heheh mwalim, nimetoa mfano wa bei rahisi ili kila mtanzania aweze kumiliki.
Nadhani sasa utagundua kwamba mimi nafaa kuwa Rais wa Tanzania.

Bek to ze topik: Huyu ndugu yake Bishanga anahitaji calculator katika shughuli zake za kuhonga. Khaaa! nimejarib kutumia kichwa kitupu kujumlisha hayo mahela hakyaPAW nimeshindwa
 
Hii sms jana mke wa ndugu yangu kaibamba kwenye simu ya mumewe ambaye alisevu jina la mtuma meseji kuwa anaitwa ' Mose fundi bomba':
'Mpenzi leo nimepita madukani Kariakoo.Bei ya vifaa ni hizi: Stima (500,000._), Draya(400,000.-), Stima ya fasho(200,000.-), viti (60,000.-) na sinki(600,000._). Fanya hima kesho (yaani leo) unipatie hizo pesa maana nasikia bei karibu zitapanda.Ukinipa milioni mbili na nusu zitanitosha na kununulia dawa za kuanzia.mmmmmwwwaaaa i love you,ikamalizia hiyo sms.

Wakuu timbwili linaendelea,na tatizo kubwa bi mkubwa mradi wake wa kuku umesimama mzee anasema hana hela na wanaishi nyumba ya kupanga. Kinababa haya mambo ya kuzima moto kwa jirani huku kwetu kunaungua matokeo yake ndo haya.
Nawasilisha.

Wanaume kwa jinsi walivyo mahodari kukanusha, utasikia............."Hii meseji itakuwa ni Wrong Number"
 
Mkuu Bishanga, haya hayajakukuta wewe kweli???
 
heheh mwalim, nimetoa mfano wa bei rahisi ili kila mtanzania aweze kumiliki.
Nadhani sasa utagundua kwamba mimi nafaa kuwa Rais wa Tanzania.

Bek to ze topik: Huyu ndugu yake Bishanga anahitaji calculator katika shughuli zake za kuhonga. Khaaa! nimejarib kutumia kichwa kitupu kujumlisha hayo mahela hakyaPAW nimeshindwa

Kloro na F yako ya maths nahisi hapo umeona nyota nyota tuu
Ila wanaume ndio tulivyo
 
hili ni tatizo kwa wanaume wanaotumia Mb** badala ya kutumia bongo(akili)!! tena asilimia kubwa ya wanaume kama hawa eti wanajiita wasomi!
 
Inauma sana jamani ingawa tunasisitizwa tusiwe tunapekuwa simu za wapendwa wetu ..lakini kwa swala hili inabidi mama watoto apewe hiyo 2.5 ainue mradi wake wa kuku .
 
Wanaume kwa jinsi walivyo mahodari kukanusha, utasikia............."Hii meseji itakuwa ni Wrong Number"
Si bora hata aseme ni wrong number? Utasikia kuna jamaa yangu ofisini aliniazima simu yangu.. Daaah..! Inauma aisee mradi wa kuku umesimama mwenzio saluni hiyooo! Dawa ya siku hizi ni kujenga nyumba kimya kimya, ili ikitokea siku unakutana na sms ya fundi bomba, unasepa kimya kimya kuepusha msongamano, visukari, presha na ulcers zisizo za lazima! Biashara ya kufuga kucha na kuvaa mawigi ya kichina kusubiria upewe hela za mradi wa kuku zishapitwa na wakati zamani sana!..
 
hehehe tusitajane mkuu, tukianza kutajana hapa, kuna Mods kama wanne (majina yapo) wanaingia hapo red.

Hapo uchune mkuu maana wako wengi na huo ni ugonjwa wa wengi
Ila inaelekea na huyo mwanaume nae ana F ya maths kabisa maana yeye analetewa tuu mahesabu wala haulizi yamejumlishwaje
 
Mkuu kweli ya Musa ni madogo sana
Na bei anatuma kabis ana unaambiwa utoe haraka kabla bei haijapanda na mwanaumu alivyo zumbukuku atakimbilia benki kudraw that amount kwa ajili ya hawara

'wanaume tumeumbwa mateso...kuhangaika...' alijiimbia marehemu TX Moshi William (RIP).
 
Back
Top Bottom