Wanaume tuliowahi kutongozwa tujuane

Pisi kali anakutega ushoboke akupasue. Mademu wabovu ndio wanajitongozeshaga hao!
Kizuri cha jiuza kibaya cha jitangaza huu msemo una apply hapa.

Hapa nilipo nimetongwaza na mtoto mkali wa kichagga simu zake anapiga kila saa, uzuri niko mbali na mke.
yaani nimekuja moshi nimekutana naye, kachukua simu kaweka namba.

Daaah ila simtaki mazee, toto zuri nyeupe daah macho sasa, demu ana wivu ataharibu mahusiano yangu na mke wangu ni mjamzito na mke wangu naye ana wivu kunywa sumu dakika 0 tu.
 
Hahahahahaha ishi nae tu
 
Mi uwa nakutana na visa vya kuitwa na mademu njiani , kuna siku natembea zangu na shangaa msichana mkubwa tu yupo na mdogo wake wa kike wakaniita we kaka, nikageuka yule mdogo akasema dada anasema anakupenda na wakawa wanafurahi sana uku wanaondoka, na kuna nyingine napita zangu mtaa demu anaanza kuniita kupitia dirishani kwao anapiga zile pssss pssss😀😀nilijisikia vibaya kinoma, achana na OLEVEL aisee nilikuwa na mazali ya kutongozwa😀😀
 
Nakumbuka kitambo kidogo Kama 2017 hivi kwenye pilika pilika zangu za Kila siku huwa Kuna huyo dada Kila siku asubuhi lazima tuonane barabarani , miezi inazidi kukatika tunaonana Kila siku asubuhi akuna story wala Nini. Siku moja nimekaa zangu kwenye bench nafatilia vitambulisho vya NIDA posta ghafla nikashangaa nashtuliwa na mzee mmoja nilikaa nae kwenye foleni kijana kijana unaitwa chap !! Nikageuza macho nikamwona mrembo wa barabarani nikaacha na foleni yenyewe akachukua documents zangu chap nikapiga picha na akaniambia nimsubilie kwenye ngazi .
Nikasubiri Sana mpaka nikataka kuondoka zangu ile nakaribia kutoka namuona anatembea faster ananijia hata hakupoteza muda nikapewa hagi matata Sana na ufupi wangu kwakweli siku enjoy Sana like hug maana bibie alikuwa mrefu Sana kunizidi.
Akaniambia Leo ndio Leo lazima twende nyumbani kwangu , nilicheka Sana nikamwambia huogopi wanaume wafupi wewe, vicheko vilikua vingi lakini nikajikuta nipo kwake , aliniuliza vitu vingi about my past na Kila kitu kwakweli siku mficha kitu lastly akaniambia yupo tayari kunifanya mpenzi wake pekee mpaka atakapo jitokeza mtu wa kumuoa maana aliniambia sad story Sana pia about her life kwakweli nilipewa muda nijifikilie then nimpe jibu.
Kwakweli nilishindwa nitoe jibu gani lakini bibie akaniambia hata ukikataa nimeamua kukupenda nakiri waziwazi kwenye maisha yangu huyu dada alinipenda ule upendo wengi wao wanausikia tu kwa majirani jamani nilipendwa .
Mpaka Kila nikijitazama nilivyo na mrembo alivyo machozi yananilenga lenga
Kutongozwa kupo na huwa mara nyingi sio kwa bahati mbaya.
 
Sisi wanaume makauzu sidhani kama kuna mwanamke wa kujitokeza kututongoza [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kutongozwa raha Nyie hata ukisema hela ya guest huna atalipa yeye [emoji853][emoji853]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…