Wanaume tunafeli wapi juu ya watoto tuliowazaa

Wanaume tunafeli wapi juu ya watoto tuliowazaa

bongo dili

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2015
Posts
12,350
Reaction score
25,180
Naongea hili baada ya kuachana na dogo wa miaka 22 kanifata nimpe ramani ya maisha kumdadisi kaniambia Baba na mama yake hawaishi pamoja kitambo.

Baba Hana sauti kwa mama wa kambo akiomba msaada wowote wa kuendelezwa baba anamsikiliza mama wa kambo.Baba anasema Hana hela wakati watoto wa mama wa kambo wanasoma shule hizi ghali za kulipia.

Dogo anaishi na baba yake na mama wa kambo pia chakula kwa masimango.

Ushauri inakuaje Bi Mdogo anakuwa na nguvu ya kukupangia juu ya watoto aliowakuta tayari usaidie au usisaidie. Kumbuka awakujileta wenyewe Duniani.

Hata Kama mlishindwana na mama zao kwann uwe mgumu kumsaidia mwanao ambae hausiki na tofaut zenu Kama wazazi.

Ingefaa watu waishi pamoja kwa faida ya afya ya akili ya watoto lakini ndio hivyo.

Kumbuka Pana kesho
 
Pana vijana watatu Leo ni watu wakubwa sana kwenye utumishi wa kiume wawili wa kike mmoja.

Baba yao alikua mpangaji wetu lakini mateso na manyanyaso walipata toka kwa mama wa kambo, Chakula kwa asilimia kubwa walitegemea kwetu.

Leo ni wakurugenzi mahali huku baba Yao yupo alijenga mahali napita kwake pamechoka, watoto wa mama wa kambo nao wapo tu hakuna mwenye afadhali,mama wa kambo kachoka.

Unaemfanyia ubaya Leo utamuhitaji kesho
 
Hapo ndo umuhimu wa wahenga unapotanabaika.....fimbo ya mbali...

Mzee anaangalia huduma zote anazostahili kupata kama mwanaume na babu mtarajiwa, zinapatikana kwa huyo mke wake wa sasa!

Anaanza kufikiria kama muajiriwa, security ya kazi( yeye sasa ni ya uzee wake, akiona upweke hauwezi hata nukta)

Kama ndio njia pekee ya kujipatia huduma zote za kijamii kama shule, malazi, chakula, afya n.k ni kutoka kwa baba, basi ni KUKUBALI kuwa HOUSEBOY kwa mama wa kambo kwa muda wote unaotaka kuweka sawa mambo yako.

Kinyume chake, utakuwa unapambana na mother nature.
 
b9c51590-0fff-472d-9866-860cc7af8482.jpg
 
Huyu Nabali mwanaume mpumbavu. Huyu chalii ndo atakuja kumstiri baba kitambo kijacho... Tunza hii kumbukumbu
 
Kuna mwana naye yupo hivyo hivyo na tena mke wake licha ya kwamba ndio mwenye sauti ndani ila pia ni kicheche.

Mara kadhaa washkaji wamemkuta mke wa jamaa anaruka na vibopa wa mtaa.

Ila kila wakijaribu kumfikishia taarifa mwana ili afanye maamuzi sahihi, mwana amekuwa snitch anamwambia wife wake kuwa "fulani na fulani kanambia kuwa alikukuta upo na fulani ila watakuwa waongo tu wale"

Uko zako road unapishana na shemeji unamsalimia anaanza kukuporomoshea matusi kuwa unataka umwalibie ndoa yake.
 
Baba akisha kua na watoto, haijalishi amewazaa na nani au wapi.....
1. Lazima walelewe ndani ya nyumba moja.
2. Lazima walelewe wote kwa haki na usawa.
3. Lazima watambulike kama watoto halali kwa mke wa huyo baba yao.
Ukiona baba hana maamuzi ama sauti kwa mkewe, basi huyo ni baba mpumbavu kama wababa walio acha watoto wao walelewe na wanaume wengine.
 
Kuna walimwengu huwa wanajisahau mno katika maisha kuhisi kuwa wataishi milele.
True mfano Pana liboss moja limewanyanyasa sana watumishi linastaafu October watumishi hao hao aliowanyanyasa eti anawaomba mchango wa kufanya sherehe ya kumuaga.
Unaowaona hawafai Leo kesho utawahitaji
 
Back
Top Bottom