USHAURI WA BURE KWENU KINAMAMA MSIOTOSHEKA: Mara zote manung'uniko yenu yamekosa mashiko kwa sababu mnaoleta janga la mzee kulala ni nyie wenyewe. Hamjui hatari gani mnazileta kwenye miili ya waume zenu na hiyo mimafuta mnayojaza kwenye vyakula na mineno mibaya inayotoka vinywani mwenu inavyonyong'onyeza. Sijui nani aliwaambia kutia mimafuta mingi kwenye vyakula ndio upishi.
Mkuu nafikiri imemtosha kabisa ushauri huu.
La pili, mkae mkijua kile kifaa sio kijiti kikavu kwamba kimeumbwa kigumu vile. Kile kinasimama kwa hisia. Sasa kama unanuka vitunguu au jasho unategemea appetite ya mr itatoka wapi? Hapo nikikuuliza vyakula vinavyoleta nguvu na kuamsha ari utaniambia huvijui, kwa hiyo hata huyu unayemlalamikia hapa hapewi almonds wala chai ya saa kumi na karanga. Mmekaa kudai haki tu bila kutimiza wajibu, ebo!
Mimi wife wangu kafundishwa bana, akiona nadhorota tu anabadili diet yangu. Chai ya jioni na korosho, ndizi mbivu sana, asali na tangawizi kama kawaida. Huwa kuna wakati mwenyewe anajuta kujifanya fundi kwa shughuli nzito anayoipata. Jifunzeni nutrition sio kulalamika tu huku wenyewe mnatulisha sembe na miwali daily, eti tukimbie. Nikimbie kwani nimefumaniwa?!