Wanaume tupewe nini?

Wanaume tupewe nini?

Last edited by a moderator:
Habarini,

Kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wanaume tuliowengi juu ya tabia ya wanawake walio wengi kupenda kuomba hela kutoka kwa wanaume.

Lakini cha kushangaza ni kwamba kuna rafiki yangu kipenzi ambaye ana Girlfriend wake ambaye amefikia hatua ya kutomthamini wala kumpenda kabisa sio labda kwa sababu anatabia mbaya au laa ila ni kwa sababu rafiki yake wa kike sio mpenda pesa

Yani tangu wawe katika mahusiano wana muda kama miezi 6 inakaribia ila huyu msichana hajawahi kumuomba pesa kwa shida yeyote ile. Yani hata wakitoka mwanamke huwa mambo karibu mengi anagharamia.

Kuna muda jamaa anajisikia weak saana eti kwa sababu tuu hajawahi kumgharamia wakiwa pamoja au katika mahitaji yake mfano kusuka n.k

Akimletea zawadi za gharama binti huwa anashukuru ila huwa anamhurumia kwa kumwambia hupaswi kufanya hivyo. Wala sipendi wewe kuingia gharama kwa sababu yangu.

Kuna kipindi huwa anamlazimishia kumpa pesa, binti wa watu huwa anakataa kabisa. Jamaa anachojaribu huwa ni kumpa kwa lazima na pia huwa anampa kwa njia ya kumuachia bila ya yeye kujua.

Ila pamoja na binti huyu kutokuwa na tabia ya kupenda pesa kutoka kwa boyfriend wake yupo loyal kwa mpenzi wake na nlipomuuliza rafiki yangu huyu iether kama anadharau au kutokumheshimu binti wa watu hana hayo yote ni mskivu mno.

Paka maamuzi ya mwisho jamaa anaamua kumpotezea binti huyu na kutomjali.

Kitu ambacho nimejiuliza bila kupata majibu kwa sisi wanaume hivi tunatatizo gani!?

Kumpa hela mwanamke ndio sababu ya kuwa confident kwa mwanamke? Kama huyu jamaa anavyodai

Kwanini wanaume tunashindwa kuthamini wanawake wa aina hii!?
Wabarikiwe wanawake wa aina hii kwakweli maana ni wachache mno.

Pia wale wapenda pesa salam kwenu, maana mnaweza achwa kama huyu binti kisa tuu hamuombi pesa.

Sio wanaume....Ni huyo rafiki yako HAJIAMINI.
 
Kutakuwa na la zaidi ya hilo sema tu hapend kuexpose mambo yake
 
sumbai....
Namaanisha "necha" ya mwanaume ni kuhudumia, kumbuka mwanaume ni mlinzi na mlishi mkuu wa familia. Hususan wanaume wa kiafrika. Na necha ya wanawaje kutafuta ulinzi kwa mwanaume...kuwa na mwanaume ambaye anajua atamlinda na kumtunza yeye na watoto

Sasa kama mkitoka out bills zote mdada ana clear...hajawahi kukuomba hata hela ya saluni..... ukienda kwake kuko vizuri mara tano zaidi yako. Anachohitaji ni liwazo ty...kila mwanaume akijututumua mdada hastuki....

Hapo mwanume Atapata wapi confidence???? .... lazima mwisho wa siku 1. Akinbie au 2. Atafute mchepuko utakaojaza nafasi

Hapa ndipo huwa nakosa kupaelewa kwa kweli...inamaana mwanamke asipotaka hela yako mwanaume unshindwa kujiamini.?

Kinachokufanya ujiamini mbele ya mwanamke ni mwanaume kumpa pesa mwaname?
BADILI TABIA unasema that is how african men are! ! !!

Kwa hiyo kwa vile mwanaume hajifil confident mbele mwanamke asiyetaka pesa basi ni halali kumpotezea mwanamke wa aina hiyo.?
atoto... njoo unipe ufafanuzi

Kaka mdogo mito ni halali kumwacha mwanamke wa aina hii?
 
Last edited by a moderator:
Kutakuwa na la zaidi ya hilo sema tu hapend kuexpose mambo yake

Labda kweli ila kitu alichosisitiza ni juu ya mwanamke kutotaka hela yake...ndo kero kubwa
Hizo nyingine kwake sio inshu
 
sumbai....
Namaanisha "necha" ya mwanaume ni kuhudumia, kumbuka mwanaume ni mlinzi na mlishi mkuu wa familia. Hususan wanaume wa kiafrika. Na necha ya wanawaje kutafuta ulinzi kwa mwanaume...kuwa na mwanaume ambaye anajua atamlinda na kumtunza yeye na watoto

Sasa kama mkitoka out bills zote mdada ana clear...hajawahi kukuomba hata hela ya saluni..... ukienda kwake kuko vizuri mara tano zaidi yako. Anachohitaji ni liwazo ty...kila mwanaume akijututumua mdada hastuki....

Hapo mwanume Atapata wapi confidence???? .... lazima mwisho wa siku 1. Akinbie au 2. Atafute mchepuko utakaojaza nafasi

Kweli kwa mentality hizi za kiafrika basi tuna tatizo kabisaa naona.

Na hii pia inaweza kujistify unyonyaji wa wanawake.
 
Last edited by a moderator:
Sio tatizo bana na wala wanawake sio wanyonyaji.....

Ni vile jamii yetu imetengeneza hilo...

Kweli kwa mentality hizi za kiafrika basi tuna tatizo kabisaa naona.

Na hii pia inaweza kujistify unyonyaji wa wanawake.
 
RRONDO kwa hiyo kiroho safi tuuu,
Kujiamini asilimia mia.....

Wakati dada yangu BADILI TABIA anasema ni umarioo.. eti

Kivipi umarioo? Nijuavyo umarioo ni kupenda kuhudumiwa na mwanamke. Kwani rafiki yako kaomba ahudumiwe? Anajitahidi kuhudumia gf anamwambia asante au sihitaji tatizo nini. Yeye aendelee kumnunulia zawadi tatizo kazoea kuhonga ndio apewe. Ukizoea vya kunyonga vya kuchinja huwezi.

Mimi napenda sana wanawake jkama huyo nachukia sana ombaomba na kwa kusema hivyo zawadi nanunua na tukienda out nagharamia kila kitu na msaada natoa ikibidi,ila ombaomba hawa kwa kweli NO!!!
 
sumbai....
Namaanisha "necha" ya mwanaume ni kuhudumia, kumbuka mwanaume ni mlinzi na mlishi mkuu wa familia. Hususan wanaume wa kiafrika. Na necha ya wanawaje kutafuta ulinzi kwa mwanaume...kuwa na mwanaume ambaye anajua atamlinda na kumtunza yeye na watoto

Sasa kama mkitoka out bills zote mdada ana clear...hajawahi kukuomba hata hela ya saluni..... ukienda kwake kuko vizuri mara tano zaidi yako. Anachohitaji ni liwazo ty...kila mwanaume akijututumua mdada hastuki....

Hapo mwanume Atapata wapi confidence????
.... lazima mwisho wa siku 1. Akinbie au 2. Atafute mchepuko utakaojaza nafasi

hio ya kung'ang'ania hadi bills kidoogo itafanya mtu ujisikie vibaya....lakini kama mwanamke kakuzidi kipato kosa lake nini? umkimbie ukatafute masikini? huko ndio kutojiamini.
 
Back
Top Bottom