Wanaume tuwe makini kudate na wadada wa kuanzia 27+

Wanaume tuwe makini kudate na wadada wa kuanzia 27+

Wadada wengi siku hizi haswa walio fika miaka 27 na kuendelea wanakuwa ni waoga sana wa kuachwa na uwoga wa maisha. Kiufupi wana kuwa desperate kiasi fulani.

Tusidanganyane ndoa kwa mwanamke ni kitu kikubwa sana. Kina mpa heshima katika jamii. Mwanamke anaye fika hadi umri wa miaka 30 bila ya kuolewa anaonekana kama alikuwa anauchezea ujana wake kwa kubadilisha wanaume. Ambao kwa namna moja au nyengine ina ukweli fulani.

Ushauri kwa vijana wenzangu tuwe makini sana kudate na hawa wanawake. Kama kweli umempenda kwa dhati basi vizuri lakini kama unapita tu bora umwambie ukweli. Wanawake wa rika hili wana kiu ya ndoa na kupata mtoto kwa hali ya juu.

Sisemi kwamba mwanamke anaye kuwa na 27+ kisa haja olewa ni mbaya hapana. Tena wengi wao wanakuwa ni watoto wa kishua, wanapesa zao na elimu zao. Swali linakuja nani ATAMFUNGA PAKA KENGELE. Maana itakuwa kama wewe ndo unaolewa sasa.

Ukidate na mwanamke wa umri wa 27+ kuwa makini haswa kama kwenu mko vizuri, hapo naongelea mwanamke kama anatokea familia ya chini au kawaida. Kama hutamzawadia mimba basi ndoa. Jipange kwa hayo mawili. Ukisema una test kama wamo au hawamo jua fika unajitafutia matatizo.

Kama hauko tayari kuingia kwenye ndoa au kupata mtoto kaa mbali na wanawake wenye umri unaokaribia 30. Utanishukuru baadae.
Hey guys, stop dating for fun.

Why getting into relationship that takes you nowhere 😡😠😡
 
Seems like your mindset is still in the Stone Age Era. Let me break it down for you.

Wanawake siku hizi tumeelimika. Tunaenda na kasi ya maisha. Akili zetu zipo kimaendeleo zaidi. Tuna focus kwenye elimu, biashara na ajira ili kujiingizia kipato maisha yaende.

Bado tunapenda na kuheshimu ndoa, lakini Ni muhimu tuingie kwenye ndoa tukiwa na maisha yetu, na hela zetu. Hata tukiingia na kibanda chetu na kiusafiri Kuna tatizo kwani?

Kulewa na kuzaa kupo tu. Tusake maisha kwanza.
hapo ndo mnapojikuta mmeharibu Vibaya mno.

siwapangii Cha kufanya Ila Aina hiyo ya mwanamke nilishindwa kuishi nae Mimi.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hii nchi iliyojaa maskini hao watoto wa kishua unawaona wapi wewe? Mie kutwa nakutana na jobless wanaotafuta kazi wenye umri huo.

Au hata mtoto wa daktari kwako ni wa kishua!.... hapa naongelea mtoto wa kishua ni yule aliyemaliza chuo akaunganisha masters Ulaya au State...akarudi akasimamia biashara ya mzee au akatupwa kwenye taasisi nzuri...

Watoto wa kishua hukutani nao kijinga kijinga...tena wananyan'ganyanwa maofisini.
Nenda TRA au bank za NMB au CRDB utakutana na watoto wa kishua kibao.
Mtoto wa kishua sio mpaka awe na masters. Alafu watoto wa kishua sio wote wana mind kusoma sana.
Degree yake ina mtosha.
Watoto wa kishua wengi wanadate na vijana ambao sio type yao wengine hadi dereva bodaboda.
Kwahyo akikuona una muonekana na unasomeka na ukamletea stori za ndoa.
My friend you are in for it
 
Unahoja nzuri....

Hili hutokea mara nyingi kwa ambao hawakuendelea na shule.

Ila nyie mlioendelea na shule mkamaliza na degree wengi ni ngumu.

Wengi mnamaliza masomo tayari mna 25. Mnasota kitaa miaka 3 mwaka wa tano ndiyo mnakuwa stable.

Na nyie wengi wenu hamuoi darasa la saba mnao wafanyakzi wenzenu.

Umri wa huyo mfanyakazi haurudi nyuma....
Umeelezea kama una data zote lkn (?).... anyway, si lazima Me kuoa agemates.

Hakuna umri mbaya kwa mwanaume kujihusisha na mapenzi Kama akiwa kwenye 18-30. Maana katika huo umri mwanaume bado hajajipanga kimaisha unless kuwe na exception. Lakini kwa mwanamke ni sahihi maana hategemewi kuchangia material yoyote kwenye mahusiano ya ndoa.

Mwanaume kwanzia 30 na kwendelea ndio panakucha, stress za maisha zishapungua yaani kila kitu kina boom. Me hata awe na 40 bado ni muda sahihi wa kuoa Ila Ke akifika 30 Kama hajaolewa analo.
 
Wakiingizwa mkenge wewe inakuhusu nini?
Huo mkenge unaujua wewe??
Acha udada mtoto wa kiume
Dah imenibidi nicheke kweli hii mada kiboko
IMG_20200921_184644.jpg
 
Wenye akili wako busy na vitu vya maana huko
Ila hawa kajambanani kutwa kuandika utopolo kama wa mtoa mada.
Wenye akili kubwa hawawazi ka mleta mada anavowaza wanawaza vitu vikubwa, Yani mwanaume anawaza wanawake kuolewa je wanawake wote wa ukoo wake wameolewa, Hana kazi za kumkeep busy huko aliko
 
Nenda TRA au bank za NMB au CRDB utakutana na watoto wa kishua kibao.
Mtoto wa kishua sio mpaka awe na masters. Alafu watoto wa kishua sio wote wana mind kusoma sana.
Degree yake ina mtosha.
Watoto wa kishua wengi wanadate na vijana ambao sio type yao wengine hadi dereva bodaboda.
Kwahyo akikuona una muonekana na unasomeka na ukamletea stori za ndoa.
My friend you are in for it
Basi umekutana na mateller watatu wanne...benki panavyovutia wakakuambia wao wa kishua.

27 sio umri mkubwa kwa wanawake usiwatishe....waache watimize ndoto zao.

Tena jua kabisa leo ukikutana na mwanamke akaonyesha hataki kuolewa ni haujakidhi vigezo vyake. Inamaanisha kwake wewe ni aheri asiolewe.
 
Ungesema "Wavulana tuwe makini kudate na wadada wa kuanzia 27+"

Sasa wanaume tusi-date na wadada wa 27+ kumbe ulitarajia tu-date na wenye umri upi?
[emoji7][emoji122]
First born agiza kinywaji nakuja kulipa
 
Wenye akili kubwa hawawazi ka mleta mada anavowaza wanawaza vitu vikubwa, Yani mwanaume anawaza wanawake kuolewa je wanawake wote wa ukoo wake wameolewa, Hana kazi za kumkeep busy huko aliko
Mtoa mada ni mtoto mdogo asiye na akili
 
Basi umekutana na mateller watatu wanne...benki panavyovutia wakakuambia wao wa kishua.

27 sio umri mkubwa kwa wanawake usiwatishe....waache watimize ndoto zao.

Tena jua kabisa leo ukikutana na mwanamke akaonyesha hataki kuolewa ni haujakidhi vigezo vyake. Inamaanisha kwake wewe ni aheri asiolewe.
Unadhani utafanya kazi benk bila connection.
Wakishua wanajulikana sio mpaka akwambie. Fanya tafiti boss ndo ujenge hoja.
Kuanzia 27 mentality ya mwanamke huanza kubadilika wengi wao hutaka kusetle na mwenza wao.
 
Umeelezea kama una data zote lkn (?).... anyway, si lazima Me kuoa agemates.

Hakuna umri mbaya kwa mwanaume kujihusisha na mapenzi Kama akiwa kwenye 18-30. Maana katika huo umri mwanaume bado hajajipanga kimaisha unless kuwe na exception. Lakini kwa mwanamke ni sahihi maana hategemewi kuchangia material yoyote kwenye mahusiano ya ndoa.

Mwanaume kwanzia 30 na kwendelea ndio panakucha, stress za maisha zishapungua yaani kila kitu kina boom. Me hata awe na 40 bado ni muda sahihi wa kuoa Ila Ke akifika 30 Kama hakaolewa analo.

Umenipoteza maana umeleta mapya ambayo sikuqoute.
 
Back
Top Bottom