Wanaume Ukraine waacha kwenda masokoni,mikahawani,shughulini na sehemu za ibada kuogopa kukamatwa kupelekwa mstari wa mbele

Wanaume Ukraine waacha kwenda masokoni,mikahawani,shughulini na sehemu za ibada kuogopa kukamatwa kupelekwa mstari wa mbele

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Kaka Serhiy na dada Tania walikatisha kufanya harusi yao ufukweni mwa bahari wakihofia hali mbaya ya hewa.Hata walipoingia kwenye ukumbi walikoalkwa wageni kushuhudia harusi yao bado waligundua hali isiyo rafiki kwa furaha yao.Viti zaidi ya nusu vilikuwa ni vitupu ikiwa na maana waliohudhuria ni zaidi kidogo ya robo

.Baadae walijua ni kwanini imekuwa hivyo baada ya kupata ujumbe nyingi zilizotoa udhuru kutoka kwa marafiki na familia, zikisema hawangeweza kuhudhuria kutokana na hofu ya vikosi vya kuandikisha watu kwenda vitani ambavyo sasa huwa vinavinjari kila sehemu yenye mikusanyiko na hata mitaani.

Hali hiyo imeikumba Ukraine baada ya askari wake wengi kufariki vitani au kupata majeraha mabaya.Jambo hilo limewafanya wanaume wachache waliobaki kuamua kujificha wakiwa hawako tayari tena kwenda vitani kupambana na Urusi.

Conscription squads send Ukrainian men into hiding

Kaka Serhiy na dada Tania walikatisha kufanya harusi yao ufukweni mwa bahari wakihofia hali mbaya ya hewa.Hata walipoingia kwenye ukumbi walikoalkwa wageni kushuhudia harusi yao bado waligundua hali isiyo rafiki kwa furaha yao.
Vitu zaidi ya nusu vilikuwa ni vitupu ikiwa na maana waliohudhuria ni zaidi kidogo ya robo.Baadae walijua ni kwanini imekuwa hivyo baada ya kupata ujumbe nyingi zilizotoa udhuru kutoka kwa marafiki na familia zikisema hawangeweza kuhudhuria kutokana na hofu ya vikosi vya kuandikisha watu kwenda vitani ambavyo sasa huwa vinavinjari kila sehemu yenye mikusanyiko na hata mitaani.
Hali hiyo imeikumba Ukraine baada ya askari wake wengi kufariki vitani au kupata majeraha mabaya na hivyo kuwafanya wanaume wachache waliobaki kuamua kujificha wakiwa hawako tayari tena kwenda vitani kupambana na Urusi.

Conscription squads send Ukrainian men into hiding

Kuna mambo mengine ni ya kutumia akili tu Ukraine kwa sasa alitakiwa asalimu tu amri yaishe wawekeane makubaliano tu ya kuheshimiana.

Huwezi kukubali wananchi wako waumie wazidi kufa kisa uzalendo wa hivyo hapana.
 
Huyo zele mnayemulaumu kwa sasa anaweza kuwa kama mateka tu atafanya na kuongea anachoambiwa. Mabeberu wakimuachia huru aidha atajisalimisha mapema sana kwenye mapatano au atawahishwa mapema sana kuiaga dunia
 
Halafu watu kama hao ndo unawapa zile ndege, huku akicheki putin kaweka fungu,,,,hapo anatoroka fasta na chenji anapata ya kuanzia maisha,,,unapewa usafiri wa bure na noti juu.......hao jamaa kwa sasa hawataki kwenda kupigana na mrusi sema ndo hakuna namna rais nae anapokea command tu toka kwa wakubwa, hii ndo shida ya kua na viongozi vibaraka
 
Kuna mambo mengine ni ya kutumia akili tu Ukraine kwa sasa alitakiwa asalimu tu amri yaishe wawekeane makubaliano tu ya kuheshimiana.

Huwezi kukubali wananchi wako waumie wazidi kufa kisa uzalendo wa hivyo hapana.
Kisa kutaka kujiunga na NATO.kwa faida ipi ?
 
Kaka Serhiy na dada Tania walikatisha kufanya harusi yao ufukweni mwa bahari wakihofia hali mbaya ya hewa.Hata walipoingia kwenye ukumbi walikoalkwa wageni kushuhudia harusi yao bado waligundua hali isiyo rafiki kwa furaha yao.
Viti zaidi ya nusu vilikuwa ni vitupu ikiwa na maana waliohudhuria ni zaidi kidogo ya robo.Baadae walijua ni kwanini imekuwa hivyo baada ya kupata ujumbe nyingi zilizotoa udhuru kutoka kwa marafiki na familia, zikisema hawangeweza kuhudhuria kutokana na hofu ya vikosi vya kuandikisha watu kwenda vitani ambavyo sasa huwa vinavinjari kila sehemu yenye mikusanyiko na hata mitaani.
Hali hiyo imeikumba Ukraine baada ya askari wake wengi kufariki vitani au kupata majeraha mabaya.Jambo hilo limewafanya wanaume wachache waliobaki kuamua kujificha wakiwa hawako tayari tena kwenda vitani kupambana na Urusi.

Conscription squads send Ukrainian men into hiding

vita sio nzuri, hao wanajeshi wa Urusi wanakula madawa ya kuondoa utu , wanakwenda kama mazombi hawaogopi kufa, ila waukraine wengi wana akili za kawaida lazima waogope kutiwa,kwenye jeneza mapema
 
Hizi habari za kwamba ukraine wanaume wameisha mbona kama za muda mrefu lkn tunaona vita inaendelea tu.
Vinaendelea kwa shida sana.
Waliokuwa na hamasa za kizalendo mwanzoni mwa vita walipelelekwa na wote waliisha.Wakafuata askari wenyewe wa jeshi nao wakaisha.Sasa ni hao wanakamatwa kwa nguvu ambao nao wanaisha.
 
Sio kweli shekhe
Baba mchungaji ,Dunia Pana hii.
Screenshot_20240620-194455.png
 
Back
Top Bottom