Wanaume Ukraine waacha kwenda masokoni,mikahawani,shughulini na sehemu za ibada kuogopa kukamatwa kupelekwa mstari wa mbele

Wanaume Ukraine waacha kwenda masokoni,mikahawani,shughulini na sehemu za ibada kuogopa kukamatwa kupelekwa mstari wa mbele

Kuwafanya wapigane inataka ufundi wa hali juu sana.Ni kama Urusi kuwafanya chambo ili Ukraine isithubutu kushambulia upande wa Urusi.
 
Kuna mambo mengine ni ya kutumia akili tu Ukraine kwa sasa alitakiwa asalimu tu amri yaishe wawekeane makubaliano tu ya kuheshimiana.

Huwezi kukubali wananchi wako waumie wazidi kufa kisa uzalendo wa hivyo hapana.
Hana uwezo wa kuamua,Zele alishauza uhuru wa Ukraine siku nyingi.
 
  • Ukrein si nchi huru tena, hata ile 'ladha' ya kuwa ndani ya bara la Ulaya inapotea.
  • Ni heri Raisi V. Zelesky ajitose kwenye tindikali kuliko kuendelea kushuhudia 'kazi mbovu' aliyoasisi.
 
Kaka Serhiy na dada Tania walikatisha kufanya harusi yao ufukweni mwa bahari wakihofia hali mbaya ya hewa.Hata walipoingia kwenye ukumbi walikoalkwa wageni kushuhudia harusi yao bado waligundua hali isiyo rafiki kwa furaha yao.Viti zaidi ya nusu vilikuwa ni vitupu ikiwa na maana waliohudhuria ni zaidi kidogo ya robo

.Baadae walijua ni kwanini imekuwa hivyo baada ya kupata ujumbe nyingi zilizotoa udhuru kutoka kwa marafiki na familia, zikisema hawangeweza kuhudhuria kutokana na hofu ya vikosi vya kuandikisha watu kwenda vitani ambavyo sasa huwa vinavinjari kila sehemu yenye mikusanyiko na hata mitaani.

Hali hiyo imeikumba Ukraine baada ya askari wake wengi kufariki vitani au kupata majeraha mabaya.Jambo hilo limewafanya wanaume wachache waliobaki kuamua kujificha wakiwa hawako tayari tena kwenda vitani kupambana na Urusi.

Conscription squads send Ukrainian men into hiding

Walianza Russia kwanza kuajiri vijana wenye umri wa miaka 18-50 waliwagongea milango kwa nguvu wasaini mikataba ya kwenda vitani licha ya wengine kukiri hawajuwi kupigana na hawajawahi ata kusikia mlio wa bunduki Putini akawashika na kuwapeleka machinjioni, wafungwa pia wote waliswekwa vitani hadi Mtanzania 1 pia aliuwawa akipigana upande wa russia. na juzi juzi Wagner wametangaza offer kwa mtu yeyote ajiunge na jeshi lao ili akasaidie kupigana upande wa Putin.

Ukraine toka siku 1 wananchi na raia walijitokea kulinda nchi yao baada ya uvamizi kutoka Russia, kuna Wa-Ukraine ambao walikuwa wanaishi nchi mbali mbali duniani toka siku ya kwanza walirudi kwao kupigania nchi yao hivyo sio ajabu, ajabu ipo kwa Putini ambaye alijitanata yeye ni super power ana jeshi bora zaidi duniani

Ni wiki iliyopita tu Urusi walitangaza offer kwa nchini Cuba kwa anayetaka kujiunga na jeshi lao ili akasaidie kupigana mpaka rais wa Cuba akafoka sana na kusema hakuna mwananchi wake ata mmoja atakayemruhusu kwenda machinjioni russia
 
Kwanini raisi wa Cuba akafoka pamoja na urafiki wote huo na Putin.Mbona Kima hata hiyana kama hiyo.
Sijui raisi mama yetu atasemaje na sisi vijana wa bongo tukipewa hiyo fursa.Wapo wengine wanaweza kwenda kupigana kwa ahadi ya kurudi na wajane 4 tu wa kiukraine.
 
Back
Top Bottom