Wanaume wa Dar naombeni ufafanuzi kuna jambo hapa

Wanaume wa Dar naombeni ufafanuzi kuna jambo hapa

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Wakuu nimetembelewa na rafiki yangu mwenyeji wa Dare s salaam, sasa kanikuta nipo kwenye harakati za machopochopo maana nimetoka kwenye mishemishe njaa kali sana, nimepika ugali na mboga nimemaliza tumekula tukapumzika kama dka 20 hivi, nikaosha vyombo na kudeki jikoni, eti ananiambiaje, anasema sisi wanaume wa arusha hatuna aibu na nimabaili kuajiri wafanya kazi, anasema wao wanaume wa Dar asilimia 99 hawapiki huwa wanakula kwa mama ntilie, migahawa na vibanda vya chips mana ni vingi kila mahali, nikamwambia tumezoea kujipikia na hatuoni aibu kutoka nje kumwaga maji machafu endapo huna jiko la ndani, sisi kula hotelini sio sana na kupika nyumbani sio adhabu basi amecheka sanaaaa, anasema wanaume wa Dar wanaogopa kupika kutokana na sababu kama 4 hivi

1. Joto kali sana, ukipika unatokwa na jasho vibaya mno,

2. Akikutwa na demu akiwa anapika ni aibu sana kwake au hata majirani wakimuona
watasema ni bahili

3. Anasema ni aibu kwa mwanaume wa Dar kuosha sufuria lenye ukoko wa ugali

4. Anasema wanaume wa Dar ni aibu kuwa buzy unaosha vyombo kila siku mchana na jioni au muda unapokuwepo nyumbani haswa wasio na self na jiko la ndani wanaogopa kuonekana wakimwaga maji machafu nje…

Ebu tumalize huu ubishi naomba mje mnisaidiewa Arusha tumeshakomaa mabanda ya chips hatunaga mengi mtaani na kila mahali huenda ndo maana huwa tumezoe kula zetu Kambale na Mberege na mihogo.

Karibuni
 
Kweli hatufanyi hayo mambo hasa tukiwa kwa nyumba za kupanga
 
Mimi naendaga kula pande na pua ya noah kwa Bonge kule mchongomani (cheka ung'atwe) kwa mawala

Haters kama nawaona.
 
Sometimes nanyinyi mnaomabiwa hizo stori za kijinga nawewe unakaa unasikiliza basi ujue kakuzarau
 
Huku mjini watu wapo bize kutafuta hela. Hatuna muda wa kupika na tunaheshimu biashara za watu ndio maana tunaamua kugawana kipato. Huko mkoani hayo mambo hayapo ukitoka kazini huna pakwenda huku ukitoka kazini kuna mambo kibao ya kufanya muda wa kukaa kupika hatuna. Tukisema tuamue kupika dada zenu wa mikoani maarufu kama mabeki 3 watakosa ajira mjini acha tugawane kipato.
 
Toa sababu yako ya msingi, kwa hiyo mnawaonea wake zenu mkioa mnawatwika mizigo kuwa wao ndio kazi yao sio
Kila kitu kipo kama ulivyovikuta ukienda kombo tuh utaonekana wa ajabu...we jikute uko kama wao afu uanze kukuna nazi kibarazan mara paap wasikiliza taarab uku wapika
 
Kila kitu kipo kama ulivyovikuta ukienda kombo tuh utaonekana wa ajabu...we jikute uko kama wao afu uanze kukuna nazi kibarazan mara paap wasikiliza taarab uku wapika
uzuri ni kwamna waarusha wengi na wameru natuna mazoea ya kukuna nazi au kula vyakula vyenye nazi ni swala jipya sana mara nyingi huwa tunapika kawaida sana ndo maana huwezi kuja kwangu ukasikia napikia nazi mapaka nakua mama yangu hajui habari ya nazi
 
Nendeni Dodoma huko, kuna ndugu yenu wa UDOM kakutwa na umauti kwa kutumia Viagra!
 
Mtoa mada ndo km alivokufanyia mkuu,kazi kubwa hapo alifanya ww ndo housegal, umechelewa kuelewa.mentality ya umkoa inawatesa
 
sasa kanikuta nipo kwenye harakati za machopochopo maana nimetoka kwenye mishemishe njaa kali
Red =MAPOCHOPOCHO
Hilo neno tu limekushinda kuandika sijui huko jikoni kwenyewe ulipokuja kujinasibu hapa [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
 
Red =MAPOCHOPOCHO
Hilo neno tu limekushinda kuandika sijui huko jikoni kwenyewe ulipokuja kujinasibu hapa [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
ahaha typing error
 
Wanaume wa dar wanaogopa kupika coz wataungua [emoji2][emoji2]
 
Back
Top Bottom