Mung Chris
JF-Expert Member
- Sep 12, 2017
- 3,391
- 3,849
Wakuu nimetembelewa na rafiki yangu mwenyeji wa Dare s salaam, sasa kanikuta nipo kwenye harakati za machopochopo maana nimetoka kwenye mishemishe njaa kali sana, nimepika ugali na mboga nimemaliza tumekula tukapumzika kama dka 20 hivi, nikaosha vyombo na kudeki jikoni, eti ananiambiaje, anasema sisi wanaume wa arusha hatuna aibu na nimabaili kuajiri wafanya kazi, anasema wao wanaume wa Dar asilimia 99 hawapiki huwa wanakula kwa mama ntilie, migahawa na vibanda vya chips mana ni vingi kila mahali, nikamwambia tumezoea kujipikia na hatuoni aibu kutoka nje kumwaga maji machafu endapo huna jiko la ndani, sisi kula hotelini sio sana na kupika nyumbani sio adhabu basi amecheka sanaaaa, anasema wanaume wa Dar wanaogopa kupika kutokana na sababu kama 4 hivi
1. Joto kali sana, ukipika unatokwa na jasho vibaya mno,
2. Akikutwa na demu akiwa anapika ni aibu sana kwake au hata majirani wakimuona
watasema ni bahili
3. Anasema ni aibu kwa mwanaume wa Dar kuosha sufuria lenye ukoko wa ugali
4. Anasema wanaume wa Dar ni aibu kuwa buzy unaosha vyombo kila siku mchana na jioni au muda unapokuwepo nyumbani haswa wasio na self na jiko la ndani wanaogopa kuonekana wakimwaga maji machafu nje…
Ebu tumalize huu ubishi naomba mje mnisaidiewa Arusha tumeshakomaa mabanda ya chips hatunaga mengi mtaani na kila mahali huenda ndo maana huwa tumezoe kula zetu Kambale na Mberege na mihogo.
Karibuni