Wanaume wa JF, single mothers waliwafanyia nini?

Wanaume wa JF, single mothers waliwafanyia nini?

Sikuwahi kudhani kuwa single mom ni issue mpaka pale niliposhuhudia single mom akimkataa single mom aliyetakiwa kuolewa na mwanae. Pia, nimeshuhudia wamama (mom na shangazi(nao ni masingo moms)) wakimkataza kijana wao asioe single mom na kuahidi kumpa laana kama asipotii maelekezo yao.
Binafsi, sina tatizo na single mothers. Hawana baya.
 
Hellow JF,

Kuna baadhi ya wanaume humu wanapenda sana kuwadis single mother. Jamani usimhukumu mtu eti kwa vile tu ana mtoto na hajaolewa sawa japo yatakiwa mtoto azaliwe katika ndoa but inapotokea kazaliwa pasipo ndoa haitakiwi kumlaumu mtu wala kumuongelea vibaya kwa kitu kama hicho.

Everything happens for a reason na ni bora anayezaa hata kama hayupo ndani ya ndoa kuliko anayefanya abortion kisa tu kapata mimba then bado hajaolewa au mwanaume kamkimbia.

Kuna watu wanaongea maneno makali sana kuhusu single mother, kweli hakuna anaependa kuwa single mother but Mungu akikubariki mtoto ni kushukuru sana sababu mtoto ni baraka kubwa sana haijalishi umempata katika mazingira gani. Kuna watu wapo kwenye ndoa but hawana furaha kwa kukosa watoto.

Pia hata ukizaa kama kuolewa kupo utaolewa tu, mtoto sio kikwazo. Wangapi wamezaa na wameolewa tena na vijana ambao hawana hata mtoto? Mtu akikupenda hatajali kusema una mtoto. Upendo wa kweli hauchagui.

Msiwaongelee vibaya single mothers, Mungu anawaona
[HASHTAG]#kigodoro[/HASHTAG].
Anna Deo
 
Back
Top Bottom