Jifunze kwanza kupika "ubusara" pia jifunze kuandaa kichuri,tena kile kiwekwacho pilipili kichaa.
huku siye hatunywagi chai wala sembe,msosi wetu mtama na kama una zamu ya kuchunga siku hiyo lazima upige kitu cha mtama mwekundu asubuhi.
Pia jifunze kuendesha baiskeli na pia jifunze kuita mbwa kwa miruzi.Jiandae kwenda kuchunga itakapobidi.Kisimani kuteka maji na mtungi wa lita50 kichwani ni kawaida kila siku alfajiri saa11.
So kabla ya kutaka kujua tabia zetu kwanza jitathimini kama utaweza hiyo style yetu ya maisha.
Na ninakuonya usije ukathubutu eti unamuandalia mwanaume wa kikurya chai ya rangi asubuhi na mkate,hizo kitu haturagi "mura" maana zinapunguza kasi ya gwaride la chumbani.
Siye asubuhi ni "KIDOGO" cha pundamlia tena kile cha kunuka na ugari wa mtama mwekundu pembeni lita1 ya maziwa mgando mtindi.
Hizo sijui cake,vitumbua,maandazi tupa kule bi dada.