Lizzy, siwezi kukuambia ubaya wa generalisation and judgement, b'cause nimesha kuona mara nyingi ukiwauliza watu kwa nini wanafanya hivo (hasa pale wanapojiuliza kuhusu mila ya kichaga).
Kila kabila na mila yake. Na wamaasai walijenga mila yao kufatana na maisha na mazingira walo kua nayo huko nyuma. Maisha yenyewe yalikua ni ya ufugaji na mazingira yalikua ni mazingira ya savanah.
Katika mazingira hayo hatari zilikua nyingi mno, toka kwa vinyama vya porini au toka kwa clans zingine za kimaasai. kwa hivo walihitaji kugawa kazi za ndani kwa mtindo huu: mwanamke afanye shughuli zote atakazo weza ili mwanaume aweze ku-concentrate katika kuilinda familia yake tokana na dangers hizo. Pia wanaume walikua wanawinda vinyama na kuongeza variety katika chakula cha nyumbani.
Sasa kutokana na 'promotion' ya sekta ya utalii, serikali imegeuza eneo lao asili kua eneo la utalii na wenyewe wamelazimika kubadili mfumo wa maisha from what I have just described hapo juu kugeuka walinzi (that is what they were raised to do). Expropriation hii ilifanyik bila compensation, bila reinsertion na bila msaada wowote wa training, finance au aina yoyote ile kuhakikisha wana-adapt in their new environment. Unaweza kusema kua muda umefika kwa wamaasai ku-revise taratibu zao, na nakubaliana na wewe but it takes time and lots of eeffort toka kwao na toka kwa serikali pia to change it.
I know of one maasai man, na anafanya kazi nzuri tu. But haikutokea by coincidence. Alisaidiwa kwa namna moja au nyingine. Babu yake alisomeshwa na serikali, akawa mwalimu na baba yake alisomeshwa na serikali pia akaingia jeshini na kuendelea hadi ngazi za juu. hiyo 'exposure' ilichangia katika uamuzi wa baba yao kuwapeleka watoto wake wote shule na leo wote wana masomo, wana kazi na wanaendesha maisha kama westerns walivo taka tuendeshe maisha.
Hata hivo turudi kwa hao maasai ambao unazungumzia, yani wale walio porwa eneo zao na kutelekezwa mahala ambapo walishindwa kabisa kuendelea kuhishi kama mila yao ilivo wafunza: are you sure they are useles to their household? labda nikuulize suali moja tu, then tutaendelea from there: Nini kazi ya simba dume?