Wanaume wa Tanzania na romance

Wanaume wa Tanzania na romance

Utakuta ndoa ni ya mtu wa karibu na mnatakiwa wote muwepo. Nyumba hizi zinaficha mengi sana kuna jamaa niliwahi kuwaona wametoana out wenyewe pale Girrafe Hotel sijui walikuja kusuluisha ugomvi basi walikaa pale hawakuongea mwanzo mwisho na baada ya m/mke kumaliza chakula akamwambia jamaa maliza haraka tuondoke jamaa akamwambia usini-force kula haraka kilichofuata yule dada akabeba funguo za gari akanyanyuka akamwambia utanikuta kwenye gari. Yule m/ume alikasirika halafu watu kibao waliona ile movie ilivyoenda baadae akaagiza mzinga wa konyagi kubwa akaunywa kama juice ulivyoisha akatoka kumfuata mwenza wake kwenye gari


...halafu si ajabu ndoa yenyewe ina miaka 3 tu na ni ile tuliyoichangia mamilioni kuisherehesha! :mmph:
 
Matatizo ya kuoa/kuolewa kwa kufuata mkumbo, matokeo yake mnachokana baada ya mwezi mmoja!
 
Wengine tukifanya hivyo tunaishia kuambiwa, "Wale nao wanajidai sana kuonyesha mapenzi yao hadharani." You can't win when it comes to love. Damned if you do it, damned if you don't :blah:
 
asalaam aleykum wanajamvi, kuna jambo huwa linanitatiza saaana kuhusu ndoa nyingi (si zote) za kitanzania.
Hivi kuenda na mke wako kwenye sherehe na kukaa nae ni kinyume cha maadili yetu???
Kumshika mke wako mkono mbele ya watu hata kama watoto wapo ni kinyume cha maadili yetu??? au ni kuwafundisha watoto wawapende na kuwathamini wenzi wao pindi wa kiwa wakubwa???
Kumuweka mke wako mbele kuliko marafiki na ndugu mfano: Rafiki anakuambia muende somewhere kuhave fun ukimwambia uko busy na wife ni kinyume na maadili?? kuna jambo lingine linanishangaza saaaaana, siku ya harusi tunashikana mikono kanisani, tunakula keki moja tena twalishana na mdomo, tunadance ziro distance mbele ya umati lakini baada ya hapo yote yanakuwa KINYUME NA MAADILI, hapo kanisani kila mtu anakaa upande wake, kushikana mikono kushney,kwenye sherehe kama hamjuani no kudence no romance, no what, naombeni wanaume hapa jamvini mniambie why this is happening.... Je mnajua howmuch your wives wanapenda romance??? I can assure you women love romance more than anything else, we love displaying affection kwenye public japo kwa mipaka. Plz wanaume naombeni views zenu on this.

kama hay yafanyika kwenye ndoa za "vijana" basi pole zao.

ila kama umeyaona kwa wale watu wa "longi" basi wasamehe tu, kwani wengi wao ni mapokeo.
enzi hizo mambo ya kushikana mikono au/na kubusiana panapo kadamnasi yalikuwa yanaonekana kwenye
sinema, hivyo wengi wa wazee wenzagu wakachukulia kwamba kufanya hivyo ni usanii (acting) tu na wala sio
masuala ya ukweli. kilichofuata wife au husband akitaka kushikana mikono anaonekana anataka kufanya usanii.
hata watazamaji walikuwa wakisema "hawa nao! jaani wanafanya usanii hadharini" fyuuuu (msonyo)
 
tatizo wanaume wa kitanzania eti ukiwa bize na wife washkaji wanakwambia mwanamke anakuendesha,anyway mi kama nataka unibebe unikumbatie unikiss anywhere u must do,thats the meaning of love,love has no limitation ch muhimu ni kuangalia tu mpo katika situation gani

Big up! Your stuff makes sense. Sasa sijui wanataka uwe busy na nani?Ndio maana watu wengi wanatabia ya ku-cheat kwa sababu wanashindwa kupalilia mapenzi katika ndoa zao na kuishia kushikwa masikio na nyumba ndogo´huko hawafurukuti, watafanya yote ambayo kwa mke wake anaona aibu kuyafanya. Jamani, mapenzi kwa sehemu kubwa yanajengwa na ya vitu vidogo vidogo yakiwemo hayo ya kushikana, kukaa pamoja mbele ya watu n.k
 
ukumbuke manjonjo ya kusikana mikono,kisses na mau mkioana..uwe romantic kwa kifupi kwa huyo bibie:A S wink:

Loh laaziz ulipotelea wapi siku mbili hizi?Safari hii nimekuwekea na Avatar kabisa unione nilivyo.Naomba usiogope wala kukemea katika jina la Yesu
 
hivi vitu ni tamaduni tu unajua tofauti yetu na wazungu ni kwamba wazungu wanaonyesha mapenzi kwa vitendo kabisa kama mtu kafurahi anaonyesha kwa vitendo ila sisi waafrika tuko tofauti kutokana na tamaduni zetu utakuta mtu anampenda sana mwenzi wake lakini kuonyesha wazi anaogopa kutokana na tamaduni zetu hata kwenye harusi utakuta MC ndio anawaongoza au padre na sheikh kuwa unaweza kufunua shela na kumbusu au mchum mchum mwaaa baada ya hapo inachobaki ni wivu tu na kuulizana mbona umechelewa ulipitia wapi au mbona nimekutumia msg hujajibu yaani mapenzi yetu yanaonekana kwa wivu wivu tu na si kwa vitendo

na siku ukijifanya kubusu busu kwenye sherehe za kikazi au harusi (zakualikwa) mkitoka hapo kama sio gazeti la udaku kuwatoa front page basi ujue ndio itakuwa discussion kwa waalikwa wote

mapenzi ya kiafrika na kibongo yana miundo mbinu yake tofauti na sinema na movie za Marichuy, tunayaweza wenyewe

unafiki unatuponza tunatakiwa tubadilike, lakini nyumba ndogo zinzshikwa hadi kiuno bila kuona aibu yoyote ile
 
Kwamimi nisiye kwenye ndoa najaribu kuangalia hapa nitachangia vipi? any way siyo lazima nichangie:A S 13:

kaini ezan mbona hututendei haki watu wengine bana!sasa hiyo Avatar yako si ni makusudi kabisa hayo unatutendea watoto wa wenzio!kwanini utuweke majaribuni bana?????
 
Big up! Your stuff makes sense. Sasa sijui wanataka uwe busy na nani?Ndio maana watu wengi wanatabia ya ku-cheat kwa sababu wanashindwa kupalilia mapenzi katika ndoa zao na kuishia kushikwa masikio na nyumba ndogo´huko hawafurukuti, watafanya yote ambayo kwa mke wake anaona aibu kuyafanya. Jamani, mapenzi kwa sehemu kubwa yanajengwa na ya vitu vidogo vidogo yakiwemo hayo ya kushikana, kukaa pamoja mbele ya watu n.k

mengine hayaombeki kwa wake zetu mkuu!sasa kama una kiu na kisamvu cha kopo utafanyaje???lazima ukaitafute ugenini
 
mie sisubirigi afanye, nikijickia kufanya nafanya vyovyote vile ninavyojickia bila kuvunja sheria, c wangu bwana bac nipo nae free na anatakiwa nae ajibu mapigo kama hataki kec....na kweli kwenye wedding mabusu kibao ngoja leo mpo kwenye cjui party ya ofc, yupo busy na colleagues, hapo hapo na mie ndio nabana.

Wee nyamayao unaonekana hujatulia kabisaaaaa!!!!, utaacha kufanya. Kwa taarifa yako tu mambo ya kuonyeshana hufanywa faraghani na sio hadharani
 
mengine hayaombeki kwa wake zetu mkuu!sasa kama una kiu na kisamvu cha kopo utafanyaje???lazima ukaitafute ugenini[/QUOTE

:tonguez: duh haya mmambo matamu hayapatikani ndani na visusio usisahau mzee maana ukijaribu tu na vikao vya ukoo vitaitwa wakati ye anatoa hukooooooooooooo
 
Loh laaziz ulipotelea wapi siku mbili hizi?Safari hii nimekuwekea na Avatar kabisa unione nilivyo.Naomba usiogope wala kukemea katika jina la Yesu

Jamani hebu shindwa kwa jina la Yesu!..huyo paka na hiyo mimacho leo hata sitoki ndani usiku huu nisije nikakutana nae bure!!..kwanini umejiita Paka?
Mie nipo ,mikiki ya maisha ndo napambana na JF nikiwa free ndo naingia..thanx d🙂))
 
Jamani hebu shindwa kwa jina la Yesu!..huyo paka na hiyo mimacho leo hata sitoki ndani usiku huu nisije nikakutana nae bure!!..kwanini umejiita Paka?
Mie nipo ,mikiki ya maisha ndo napambana na JF nikiwa free ndo naingia..thanx d🙂))

Shabash! kama maneno matamu basi nimesikia leo,nitalala usingizi mnono kweli,haya bana siku nyingine ukiwa free njoo PM basi tucheze baikoko.
 
Shabash! kama maneno matamu basi nimesikia leo,nitalala usingizi mnono kweli,haya bana siku nyingine ukiwa free njoo PM basi tucheze baikoko.

Kweli wewe Paka mana uko tofauti, usiku watu wanalala wewe ndo uko matembezini!..hizo PM mie situmii kwa sababu maalum,zaidi ya majukwaa ya JF ni hapahapa kwa keyboard!!Njozi njema paka blaki
 
Kweli wewe Paka mana uko tofauti, usiku watu wanalala wewe ndo uko matembezini!..hizo PM mie situmii kwa sababu maalum,zaidi ya majukwaa ya JF ni hapahapa kwa keyboard!!Njozi njema paka blaki



Lah kaaaaz kwelikweli ,sasa hapahapa baikoko tutachezaje na watu kibao wanatutizama.Anyway nashukuru kwa kunitakia njozi njema lakini mie ndio kumekucha sasa.
 
mengine hayaombeki kwa wake zetu mkuu!sasa kama una kiu na kisamvu cha kopo utafanyaje???lazima ukaitafute ugenini

Mkuu Bacha,furaha na manjonjo ya ndoa hayaji automatically bali hutengenezwa!Kwani huko ugenini yamewezekana vipi na kwa mamsapu yasiwezekane?Watu wengi katika ndoa (ndivyo ninavyo amini) huwa hawazungumzii suala la mapenzi (how to make love in an enjoyable way) wanaishia kula aina moja ya chakula kila siku, mwishowe chakula kinakinai na kuanza kutafuta nje. We hujiulizi nini kinachowafanya watu watoke nje ya ndoa zao?Na hata akitoka na huyu leo, kesho anataka kutoka na mwingine. Sababu kubwa ni vionjo(test) kila wakati anataka kuonja akiamini chakula hiki ni kitamu zaidi kuliko kile wakati ukweli ni kwamba chakula ni kile kile ila viungo na utayarishwaji ndio unatofautiana. Mfundishe mwenzako kupika mapishi mbalimbali, kila siku chakula kitanoga wala hutataka kula kwa jirani.Halafu kwa jirani hakuna uhakika unaweza ukala SUMU bure ambayo haina antidot
 
Back
Top Bottom