Gaga
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 4,558
- 1,970
Leo kabla sijarudi home nilikaa na marafiki kama sita mahala kupoteza muda ,kuna mmoja wetu akasema mume wake kila akifika home anamwangalia kama mkewe kalala na yeye anajifanya kalala. kwa vile giza anamwona mumewe anahangaika kuficha wallet hadi sometimes chini ya kapet, chooni na wakati mwingine chini ya kitanda.
wakiamka asubuhi mke anamwambia mumewe kuna vitu vinahitajika kununua mume anamwoshesha kwenye dressing table kwamba ana kiasi kile tu anachokiona, wakati mwingine akirudi na akianza kukoroma yule dada anaangalia kule alikoficha anakuta anazo pesa, then anaacha vilevile,akiamka akimwambia majukumu majibu ni yaleyale kujifanya hana pesa wakati anazo.
Mimi niliona kitu cha ajabu sababu unafichaje halafu chumbani, kwa nini usiache kwa gari au ofisini.Wadada wawili walimuunga mkono wakasema ni kweli wanaume wengine wanatabia hiyo hadi mmoja wao aliamua kumfundisha adabu mumewe alipoficha tu yeye akachukua zote kulipokucha wanaenda kazini anamwona anatafuta akauchuna hadi jioni ndio alimrudishia na kumwambia amwamini asiwe anafichaficha pesa au wallet
sasa swali langu kwa wanaume wa jf ni kweli huwa mnafanya hivyo? na mnafanya kwa manufaa ya nani?Ni nini kinapelekea mtu kuamua kufichaficha kihivyo