Ni bora ukaweka wazi Muosha Rungu aka Dj Sepetu, wewe ilikuwa katika kundi gani...!?
Huku Mikoani (kama ulivyosema ulikuwa Dom) wanawake wenye tabia hii, kufungia Mwanaume au Kijana ndani, kummiliki na kumfadhili kwa kila kitu, wengi hufanya hivi kwa sababu ya wivu, na hii ni baada ya kubaini mapenzi anayopewa/anayopata kutoka kwa mwenzie ni zaidi ya yale ya "Mwanaume Mashine".
Tumesikia taarifa nyingi tu kutoka katika Jiji la wala Chipsi na Mayai (Jiji la watoto wa Mama) vijana wa kiume wakifungiwa ndani na Majimama na hatimaye kugeuzwa na kuwa Malioo...!
Tumesikia taarifa za Vijana kukubali kufungiwa ndani, hata kama kufungiwa huko kutaambatana na yeye (kijana) kugeuzwa Houseboy, akifanya kazi za kutumwa kama kuosha vyombo, kufua nguo (mpaka za ndani) kugeuzwa dereva wa kumpeleka "Boss lady" Saloon, Super market n.k.
Tungependa Muosha rungu, ufunguke zaidi, ni kadhia gani nyingine au changamoto gani ulikutana nazo wakati huo Umefungiwa ndani.
Kwa kile ninacho fahamu mimi, ni kero tupu utakazo kumbana nazo, moja wapo ikiwa ni KUUZA UHURU WAKO.....!!
Sent using
Jamii Forums mobile app