Wanaume wambea wanazidi kuongezeka kwa kasi ya 5G

Hili tatizo ni kubwa mno,ukiona wanaume wako kijiwenu asubuhi mpk jioni mara kwa mara tambua hapo masengenyo yanayopigwa sio ya kitoto...kuna mahali niliwahi ishi,jioni moja nikasema ngoja nikapate elimu mpya ya maisha kwenye kijiwe kimoja cha vijana mchanganyiko wa umri(watu wazima na vijana),..mada nilizokuta pale na kusema watu..tangu ile siku nili azimia nikitoka kwenye majukumu yangu ni nyumbani...bora nikae hapo kutwa nicheki TV...kibaya huyu anayemsengenya mwenzie kazidiwa mbali kimaisha...ukiwa na changamoto ya kimaisha Muombe Mungu wako akusaidie...kinyume na hapo utakua bango la matangazo either ofisini au mtaani kwako.
 
Binafsi, nafkiri tatizo kubwa ni Mazingira ya makuzi ya mtoto.

Mbili, ni Tamaa na kujipendekeza: hii inasababisha kuongea mambo ya kiumbe umbea mbele ya mtu au kundi la watu.

Wanaume tumebaki wachache na kila siku nawaambia hawa wanawake waache maringo.. ipo siku watakosa wa kuwapump.
 
Ulimalizia story?
 
Hakika vijiweni badala ya kupata madini ni masengenyo na umbea tu. Hakuna jipya
 
Si mna usasa mwingi, mnamuacha mtoto aamue chochote atakacho.
Toto la kiume la miaka 10 linaita momy na dady kwa mideko wewe unaona sawa.

Mitoto ya sasa haina michezo yoyote zaidi ya ipad, iimenenepa makalio na kuota vitambi vya broila.

Mnajidai mna malezi ya kisasa eti mtoto hachapwi wala hafokewi ila anaelekezwa tu.
 
Mtoa mada.. kuna huu Uzi. Naamini Kama kuna wachangiaji wakiume humo ujue ndio wale waleee uliokuwa unasema Mwili wa kiume matendo ya Kike. Kapitieni hata comments mtaona kuna shida. Mwanaume unaanzaje kufatilia muvi za wakorea? Tena DRAMA? mkiitwa machoko mnamaindi.

 
[emoji28][emoji28]inaogopesha kuwa mzazi wa mtoto wa kiume,Mungu tusaidie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…