Hii ya umbeya nadhani kimtaa imekuwepo siku zote maana ukifuatilia vijiwe vya kahawa au mabar, zinazoongelewa nyingi ni habari za watu.
Tofauti na wanawake, wanaume hakuna kawaida ya kufitinishana na kuzungukana lakini pia dhima ya story huwa ni kwenye kujenga Ila kwa wanawake mfano masaloon, huwa wanasengenya kama sehemu ya kujifurahisha lakini pia kubomoana ndio maana kuzushiana na kuzungukana huwa kwingi.
Mwisho wa yote badala ya kusakama hiki kizazi kipya, lazma mjiulize nyie vizazi vilivyopita, je, mlivyokuzwa ndivyo mlivyowakuza hawa mnaowasema leo hii. Kama mlishindwa, hamuoni kuwa mnapaswa kuona aibu kwa kushuhudia kufeli kwa malezi yenu kama mababa na makaka kuliko kujificha kwenye kichaka cha lawama..
Kwa nini msijisakame wazazi wa siku hizi kwa kushindwa malezi na si kuwatupia lawama zote vijana wa siku hizi