Siku hizi imekuwa desturi kwa baadhi ya wanaume kuvamia fasheni na tabia za kike hadi inaleta wasiwasi. Unamkuta mwanaume kipande cha baba amevaa kipochi cha kike anazurura nacho mtaani hadi unashangaa huyu jamaa vipi? Amerogwa, ni shoga au amezidiwa na homoni za kike?
Hivi hawa wanaume wanaovaa vipochi, tena wanamechisha kabisa, na kutoka navyo mitaani wana nini lakini jamani? Kwanini mtu uvae vitu vya kike? Wengine wanafikia hatua ya kuvaa bangili mikononi mwao. Lakini kuna wanaoenda mbali zaidi hadi kutoga masikio na pua na kuvaa hereni na vipini, mtawalia. Au unamkuta mwanaume kajichafua tatoo mwili mzima utadhani mwali kajipamba kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa ndoa. Je, tukisema kwamba hawa wanaume wana homoni za kike au ushoga tutakuwa tumekosea?
Inashangaza na kusikitisha unakutana na mwanaume kajipaka marashi yananuka mtaa mzima. Yaani unapishana naye unakwenda hatua zaidi ya 100 bado unasikia harufu ya marashi? Ukiwabana watu wa aina hii watakuambia eti wamejipaka marashi ya kiume. Ebo!
Kana kwamba haya yote hayatoshi, kuna wimbi kubwa la wanaume wanaotaka kuhalalisha uvaaji wa bukta na kuingia nazo mitaani. Hivi mwanaume mzima unavaaje bukta unaenda nayo hadi sokoni na kwenye maeneo ya mikusanyiko ya watu na bado unajiona uko sawa? Kama kawaida yao, ukiwauliza kwanini wanafanya hivi watakuambia wanavaa bukta za kiume sio pensi za kike. Kama vipi basi watengenezewa na K za kiume wawe wanagawa uroda, isiwe taabu.
Nchi hii ina baadhi ya wanaume wa ovyo na wenye tabia na akili za kike na kishoga kuliko kawaida. Serikali isipoingilia kati na kupiga marufuku huu ushenzi, miaka michache ijayo tutakuwa na taifa la ovyo sana.